Jamani wana JF, naomba mnisaidie kwenye hili, kwani napata kizunguzungu tu. Hivi huu mvutano wa Waziri wa Ardhi na Mipango Miji na Huyu mmiliki wa kiwanja hiki kilichopangwa kiwe cha wazi, nani yu sahihi?? Huyu bwana kiburi hiki cha kujibizana na waziri kinatoka wapi? Nini hasa Power ya waziri au Wizara ki ujumla kwenye hili? President kama waziri anafanya kazi kumsaidia ananafasi gani kwenye hili? na je kama sheria ni kwamba Ardhi ni Mali ya Serikali na Rais anaweza kuichukua wakati wowote kwa manufaa ya umma, sasa kigugumizi kiko wapi kwenye hili? Au President akubaliani na uamuzi wa waziri? kama ni hivyo kwa nini wasimalizane wao kiofisi kimyakimya kabla ya waziri kuwavaa hawa jamaa? Aisee sielewi kabisa. hembu wan JF wenye ufahamu mzuri wa haya mambo mnisaidie