Msaada tutani

Ghostx

Member
Oct 18, 2017
39
62
waungwana habari zenu.

natarajia kusafiri hivi karibuni kutoka Dar es salaam kwenda rukwa/sumbawanga na ni mara yangu ya kwanza kwenda huko.

Msaada ninaotaka kwenu ni kujua, ni basi gani zuri linalokwenda huko?
(nikisema zuri namaanisha sio bovu na lenye mwendo ambao hautatuweka mda mrefu barabarani)

Na nikitoka dar nitegemee kuingia rukwa saa ngapi?

Pia bei za rest house zikoje?, na ni rest house gani ni nzuri kwa kufikia mgeni kama mimi ambae natagemea kufanya mishe zangu palepale mjini?

kama kuna ushauri mwengine wowote usisite kunipa tafadhali.

Natanguliza shukran zangu kwenu.
 
Apande Golden Deer Gari iko poa na inafika muda huo huo,,,utapata faida ya kuchaji simu,huduma za maji na soda pia gari ndani mazingira safi

Majinja nilipanda j3 iliyopita sikushauri ni usafiri wa hivyo kama unaenda mbali maana hauna starehe
Majinnja express. Kufika ni 5-6 usiku
 
Apande Golden Deer Gari iko poa na inafika muda huo huo,,,utapata faida ya kuchaji simu,huduma za maji na soda pia gari ndani mazingira safi

Majinja nilipanda j3 iliyopita sikushauri ni usafiri wa hivyo kama unaenda mbali maana hauna starehe
shukran sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom