Msaada tutani: Gari inatikisika mtikisiko mkubwa mbele ya bonnet

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
10,269
6,836
Gari linatikisika kitu kizito mbele ya bonnet linapokuwa linatembea kwa spidi ya kuanzia km 80 kwa saa, na likiwa kwenye gia namba tano (gari ni manual).

Mwenye kujua hili ni tatizo gani atakuwa wa msaada sana.

Fundi wa gari amejaribu kubadilisha bush za mbele lakin bado lipo, fundi yeye alidhani pengine labda ni bush.

Vinginevyo, kingine alichoshauri fundi kifanyike ni wheel balancing, (ambayo kwa sasa bado haijafanyika) lakini mtikisiko anaoupata dereva anapokuwa anaendesha gari hilo pale tu linapokuwa limevuka spidi ya 80 km kwa saa, bado unampa dereva mashala kama tatizo hilo linaweza kusababishwa na wheel balancing.

Hata hivyo atafanya pia hiyo wheel balancing kulingana na ushauri wa fundi, ili aone kitatokea nini baada ya hapo.

Iwpo kamakuna mtu humu jukwaani mwenye mawazo tofauti na ya fundi wa gari hilo, msaada wake unahitajika kwa sana.

Halii hii imejitokeza kuanzia leo wakati mmiliki wake alipokuwa analifanyia majaribio baada ya kuwa amefanya zoezi la kuondoa hewa kwenye radiator ikiwa ni pamoja na kubadilisha coolant.

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
NYONGEZA MUHIMU:

Wakati wanalifanyia majaribio ili kujua ni nini kinasababisha mtikisiko huo, na baada ya kuwa tayari wameshafunga bush mpya
  • Wamebaini kuwa ikitokea mtu mmoja akakaa kwenye viti vya katikati (Gari ni 8-seater) na mtu huyu akawa amekaa katikatii ya kiti hicho cha katikati, gari inaweza kufikia km hata 100 bila mtikisiko
  • Still, mtu huyo akitoka nje ya gari, kiti cha katikati kikawa kiko wazi, gari inatikisika sawaswa na maelezo yaliyotolewa hapo juu
 
Angalia tyre zako za mbele, kuna tyre za kichina zinaumumka, jambo la pili angalia ball joints na tyre rod ends hizi huwa mtikisiko unahusiana na mwendo unaokwenda na mtikisisko unakuwa mkubwa kwenye lami kuliko rough roads.
Ingi
 
Angalia tyre zako za mbele,kuna tyre za kichina zinaumumka,jambo la pili angalia ball joints na tyre rod ends hizi huwa mtikisiko unahusiana na mwendo unaokwenda na mtikisisko unakuwa mkubwa kwenye lami kuliko rough roads.
Ingi
Tayari tatizo limeshakulikana, ni kubwa zaidi kuliko haya yaliyompelekea akauliza maswali hapa. Kuna "Special Engineering" imeshafanyika, na imefanyikia mahali pale pale anapoishi, ikiwa imekusudiwa kuwachafua mafundi wake wa Garage. bahati nzuri this time mafundi wamekuwa very safe, Mungu amewakinga vya kutosha
Ubarikiwe sana kwa ushauri
 
Tayari tatizo limeshakulikana, ni kubwa zaidi kuliko haya yaliyompelekea akauliza maswali hapa. Kuna "Special Engineering" imeshafanyika, na imefanyikia mahali pale pale anapoishi, ikiwa imekusudiwa kuwachafua mafundi wake wa Garage. bahati nzuri this time mafundi wamekuwa very safe, Mungu amewakinga vya kutosha
Ubarikiwe sana kwa ushauri
Mafundi wamekuwa safe kivipi mkuu? Ongeza nyama kidogo hapo.
 
Uzoefu wangu mdogo kwa upande wa Magari madogo (5 seaters)

1. Plugs za kuchoma mafuta kaziangalie
2. Ball joints

Zaidi zaidi nadhani plugs zako ziko na shida, ama zote ama baadhi

Check hizi kama zipo well functioning
 
Mm gari yangu iliwah kuwa na tatizo Hilo fund aligundua nati zinazofunga engine kwenye bodi zimekatika na taili moja ilikuwa imevimba. Angalia pia hivo
 
Mm gari yangu iliwah kuwa na tatizo Hilo fund aligundua nati zinazofunga engine kwenye bodi zimekatika na taili moja ilikuwa imevimba. Angalia pia hivo
Nilichokibaini ni kwamba injini aliyowekwa kwenye gari lbaada ya kuwa imetolewa ile iliyokuwepo awali, haikufungwa vizuri (mounting) na pia haikukazwa vizuri kwa sababu sehemu ilipofungiwa haikuwa rasmi kwa kazi hiyo. Vile vile uharaka wa wafungaji kwa sababu walikuwa wako kwenye mkakati maalumu, na kwa muda maalumu.

Hii ndiyo sababu inayopelekea injini hiyo kutikisika pindi inapofika kwenye spidi ya kuanzia km80+, inatikisika ikiwa kama inataka kutoka barabarani
 
Hua nazikataga enginr mounting za Hilux Surf aisee huo mtikisiko wake hauvumiliki hata kidogo
Sasa hivi nakuelewa. Walifanya mounting vibaya wakati wa kufunga ile engine mbadala waliyokuwa wameamua kuweka kwa sababu hawakuwa kwenye shimo.

Kwa muda huu, wanachoendelea kufanya ni kuwa wanabadilisha baadhi ya vifaa vya ndani ya gari ili viendane na ukuukuu wa engine waliyoweka, ndiyo kazi wanayofanya hadi leo

Kwa kifupi tu ni kwamba Gari ilitoka Japan ikiwa used lakini it was as good as new. Ilikuja ikiwa imetembea km147,000 tu wakati ni bonge la SUV with 4WD
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom