Msaada!!. Tuna mtoto wa miezi minne, unfortunately imenasa.

Je uzazi wa ngapi? Ila hapo mzembe ni Mwanamke kwanini alikubali kukupa? Wakati wa clinic hukupewa elimu ya ulezi na afya ya mama na mtoto ? Unless uwe ulimbaka lakini Kama aliridhia mwenyewe kukupa basi asikilaumu sana ingawa na Wewe ulizidi! Angalieni Roho ya kukataliwa isijemnyemelea aliyetumboni!
 
Ni nchi ya Ethiopia yenye watoto wengi ambao huzaliwa Kwa Wazazi kupanga na kukubaliana kuzaa lakini nchi zilizobaki Watu wake wengi hujizalia tu bila plan! Ili mradi wako Kwenye ndoa mama akishika ujauzito poa lakini hakuna plan wala nini!
 
Hatapata madhara yoyote. Na baada ya hapo muwe mnatumia kondom lasivyo mtaziflash kila mwezi.


RubiiKimimi
 
Hapo Mwanamke ndo anatakiwa ajielewe zaidi sababu mwisho wa Siku yeye ndo waku suffer the consequences! Huku anyonyeshe, huku kuna aliyetumboni clinic za wote wa nje na watumboni, tena bora iwe imemjia vizuri asitapike wala kuumwaumwa! Kama ni mfanyakazi ndo hivyo! Kama mwanaume alimuomba akampa Kwa ridhaa Yake bila mwanaume kutumia nguvu (kumbaka) basi Mwanamke ndo hajielewi bado sasa ajifunze Kwa makosa! Hata hivyo Kwa kuwa Mwenyezi Mungu yupo basi atamfanyia wepesi ktk hayo yote In Sha Allah!
 
Hiyo ni kawaida mkuu,mtoto aendelee kunyonya baada ya mwaka mwingine ataingia duniani
 
Sio jambo jema kwa wanandoa kutoa ujauzito kwa sababu kama hii uliyoitaja wewe! Ukiendekeza huu mchezo, mkeo anaweza akajenga mazoea. Iko siku mkeo atapata ujauzito lakini mkakosana tu kidogo au yeye akawa hapendi kuwa na ujauzito basi akautoa na kukudanganya kuwa ujauzito huo umeharibika!

Kwa sasa mkeo amnyonyeshe mtoto kwa miezi hata 6 ijayo ili huyu wa sasa afikishe mwaka mmoja halafu amwachishe! Wakati huo mama ujauzito wake utakuwa unaelekea au umefika miez 6. Kwa mda huo sidahani kama huyu mtoto atapata athali yoyote!


Kumbuka, hali hii haijakukuta peke yako, ni wanandoa wengi hukumbwa na tatizo kama hili hasa kwa mtoto wa kwanza na wa pili!

Kila la kheri!
Ushauri bora kabisa.kinachofuata ni kugawa attention yao kwa uangalifu kwa huyo wa kwanza mara mtoto wa pili atakapozaliwa ili mkubwa asiwe rebellious.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hapa mwenzangu anasononeka sana, nimerudi home around saa 2 usiku huu naona mtu kaingia chumbani wakati najiandaa kuingia bafuni ghafla mtu anapigamagoti analia huku ananionyesha kipimo daah, nikachukulia kawaida nikamwambia relax tupange tufanyeje, hanielewi anasema mimi ndio nimesababisha na ninarohongumu sana isiyo ya kibinadamu kwa jinsi ninavyo chukulia kawaida hiliswala.

Nahisi inaweza ikamsumbua sana, kwa mawazo, hana raha kabisa ndio mana nawaza labda nitafute kidonge nii blowout.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu msifanye hivyo jaman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu viongozi wa dini haina mantiki hata wazazi hakuna mantiki waende tu kwa dr.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushauri murua kabisa huu! Viongozi wa dini wala wazazi hawana utaalamu na mambo ya afya! Ni madaktari pekee watakao msaidia kuondoa hofu aliyonayo!

Binafsi nimeshuhudia watu kadhaa wakibeba ujauzito mapema sana (within six months) Kwa bahati mbaya na hadi sasa watoto wana afya njema kabisa!

Ni vema mdau ukampeleka mkeo Kwa daktari Kwa Ushauri zaidi na ikiwezekana mpeleke hospitali tofauti tofauti kadhaa atakapo pata ushauri unaofanana atajengeka kisaikolojia sana na atakuwa na confidence ya kuli handle!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama alivyosema mdau hapo juu nendeni kwa doctor . Kuna Jirani yangu yeye alipata mimba mtoto akiwa na miezi 2. Alitaka kuchanganyikiwa, walienda kwa doctor . Alimshauri aendelee kumnyonyesha mtoto na aongeze upendo. Alipojifungua alishauriwa aendelee kuwanyonyesha watoto wote, mpaka huyu mdogo atakapo fika umri wa kunyonya sana. Kwakweli watoto wake hawakupata shida yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom