MSAADA: Tatizo la mabaka kwenye ngozi

SALOK

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
3,318
1,936
Habari wakuu...!!!

Heshima kwenu nyote, wadau na wapenzi wa jukwaa hili na JF's members wote kwa ujumla!!

Shukrani za dhati na za kipekee kwa wale wote wenye moyo wa kujitolea maarifa, ushauri, nasaha na kutiana moyo wa pole kutokana na matatizo/magonjwa ambayo huletwa humu. Ahsanteni sana endeleeni na mioyo hiyo hiyo ya kusaidia wengine
Ndugu zangu, leo hii naomba niwashirikishe tatizo nililonalo ikiwa ni ktk jitihada za kutafuta ufumbuzi.

Ndugu zangu katika siku za hivi karibuni nimepatwa na tatizo la ngozi, katika sehemu za kwapa la kulia kuna hali ya ngozi kubabuka ambapo sehemu zenye tatizo ngozi imekuwa nyeusi hali hiyo inaenda sambamba na muwasho pamoja na maumivu, muwasho unaoelekea kuwa katika hali ya utamu utamu hivi tatizo lilianzia shingoni upande wa nyuma ya shingo kulia, ikaja upande wa nyuma kushoto.

Hali hii ya mabaka kama haya iliwahi kunitokea wakati niko mdogo sana, nakumbuka bibi alisumbuka sana kunitibu kwa dawa za miti na majani tatizo lilikuja kunitokea tena kama miaka 12 iliyopita, lakini halikudumu sasa hivi limekuja kuibukia tena shingoni na kwapani.

Kinachonipa shaka ni je inawezekana ikawa ni dalili ya ukoma, je ukoma ni ktk magonjwa yanayorithishana?? Mama yake bibi mzaa baba na babu mzaa baba wote waliwahi kuugua ugonjwa wa ukoma.

Natanguliza shukrani za dhati

Picha nitazipandisha....


0a2f8901f07afe76f26664c04b735d67.jpg


Muathiriko kwapani...


aef74b87b02b20258a5a5be83ad2a816.jpg


908233c8d7e94f2d501eb58dd6918a1c.jpg


Hapo shingoni...
 
Asee mashikolo magine nenda hospital au kwa wataalamu wa tiba asilia.

Note:usiwe na mtizamo wa mambo ya kishirikina ni mabadiliko ya mwili tu
 
Hiyo ni fangasi tu mkuu!! Tafuta gentrisone au sodaderm then after one week lete mrejesho!!
 
Nikusaidie mkuu
1.Tafuta kilele cha majani ya mboga sugulia hapo asbh na jioni wkt wa kulala muda km wiki 2 utakuja kuniambia.

AU

2.tafuta kilele cha majani ya mvuma nyuki sugulia hapo wiki 2 utakuja kuniambia.

3.nyumbani wakiwa wanapika kwa kutumia kuni kuna baadhi ya kuni huwa zinatoa mapovu ss mkuu ile ni dawa kubwa sana chukua yale mapovu yasubirie yapoe kdg kisha jipake hiyo sehemu tumia wiki 1 utakuja kuniambia.

Note: Tumia Dawa moja kati ya hizo na sio zote kwa pamoja.

Wabillah tawfik fikisha kwa wengine na ww upate thawabu
 
Soma vzr post yangu iliyopita kwa maekeko utaniona na km una ttz jengine km najua Dawa nitakuelekeza ucjal tupo kusaidiana
 
Back
Top Bottom