Msaada: Tatizo la kutokupata hedhi wa muda mrefu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Tatizo la kutokupata hedhi wa muda mrefu

Discussion in 'JF Doctor' started by YETOOO, May 25, 2012.

 1. YETOOO

  YETOOO Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello JF Doctors,

  Nimekua na tatizo la kupata hedhi kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu bila kukoma,natumia njia mojawapo ya uzazi wa mpango na nilivyoweka mwanzoni nilipata tatizo hilo kwa muda wa miezi miwili mfululizo na nilivyoenda kwa Dr akaniambia ni kwa sababu ya kipandikizi ila itaisha.

  Kweli baada ya muda iliisha na nikawa naendelea na mfumo wa kawaida siku nne au tano namaliza.

  Imeendelea vizuri kwa muda wa miezi tisa sasa naona imeanza tena ni mwezi na nusu sasa inatoka bila kuacha ila huwa inapungua na kuongezeka. hii pia ni kwa sababu ya kipandikizi au kuna tatizo jingine?
   
 2. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Rudi kwa docta yule yule
   
 3. YETOOO

  YETOOO Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nivea Ahsante sana kwa ushauri wako
   
 4. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,278
  Likes Received: 2,953
  Trophy Points: 280
  Kuna dada alichoma sindano ikatoka mfululizo,alipokwenda kwa Dr alishauriwa azae tatizo litakwisha.Alipozaa lilikwisha kbs,nadhani ni vema kurudi kwa dr kwanza ili ajue na kuona njia nzuri kuondoa tatizo.Uwe na imani utapona.
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  toa kipandikizi, tumia njia ya kalenda, ndo njia pekee salaama
   
 6. p

  paja nono Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani nnawaombeni msaada. nna tatizo la kutokupata hedhi kwa wakati kwa mfano mwezi uliopita nimepata tarehe 20 mwezi ujao upite wote sipati mpaka mwezi mwengine pengine tarehe 7. jamani ni nini tatizo?
   
 7. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Je mzunguko wako ni wa siku 35,28 au 21?
   
 8. C

  Chondo New Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzunguko wako ni wa siku ngap?
   
 9. p

  paja nono Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli nashindwa ata kujua uhakika kutokana na tatizo hilo. siku nyengine zinafika siku 35 siku nyengine 42 ata nashindwa kujielewa. mana mara ya mwisho kupata ni tarehe 24 july.
   
 10. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  .

  Una umri wa miaka mingapi? Inawezekana ni 'menopause' inanyemelea. REJEA:
  http://www.34-menopause-symptoms.com/#irregularperiods
   
 11. p

  paja nono Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nna umri wa miaka 24, sijaolewa. iyo menopause ndio kitu gani naomba unielezee japo kwa ufupi kidogo mana si wengine tumekimbia shule.
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mkuu KAUMZA Pole sana kwa shemeji yetu hatoki hedhi dawa nitakupa za Tiba Mbadala jaribu mojawapo wa dawa zangu hizo 5 kwa kutumia kwa muda wa siku 3 kisha uje hapa unipe Feedback.

  DAWA ZA KUTEREMSHA HEDHI.

  Ikiwa hedhi imezuilika kwa kufikia umri wa kumaliza au ni kwasababu ya mimba, inafahamika lakini ikiwa si kwasababu mbili hizo basi hufanyiwa dawa na kuirudisha hedhi.

  1. Kunywa chai ya mdalasini.

  2. Mvuje ukinywewa pamoja na pilipilimanga huteremsha hedhi iliyo fungwa katika uzai au mapito yake.

  3. Manemane ukiponda na ukinywa siku tatu asubuhi kabla ya kula chakula

  4. Kitunguu Saumu na maganda yake huteremsha hedhi

  5. Kunywa maji yaliyochemshwa na Zaatari.

  Chanzo.MziziMkavu Mtaalam wa Sayansi za Kiafrika Tiba za Asili.
   
 13. Mwl.RCT

  Mwl.RCT Verified User

  #13
  Sep 5, 2013
  Joined: Jul 23, 2013
  Messages: 5,663
  Likes Received: 2,275
  Trophy Points: 280
  • Swali kwa Madaktari (linatokana na hii thread): "Je mwanamke asipopata kwa muda mrefu siku zake kuna madhara yeyote kiafya kwake?." Kama ilivyo kwa mpendwa wa mleta mada.
  Aksante
   
 14. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2013
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,695
  Likes Received: 8,230
  Trophy Points: 280
  Cc: MziziMkavu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kukosa Hedhi (Amenorrhea)

  [​IMG]

  Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo. Aidha suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo.


  Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary).


  Primary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti au nywele za kinena; au msichana anaweza kuwa na mabadiliko ya kubalehe lakini asipate hedhi.


  Secondary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi, na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi (menopause) na wala hatumii njia za uzazi wa mpango kama vile sindano au vidonge, na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa miezi mitatu au zaidi.


  Mwanamke hupataje hedhi?


  Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi, ni lazima matezi yake ya hypothalamus na pituitary pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya kike (ovaries) na mji wa mimba (uterus) vifanye kazi zake sawasawa.


  Hypothalamus huchochea tezi la pituitary kuzalisha hormone chochezi ya follicle au follicle-stimulating hormone (FSH) pamoja na homoni ya luteinizing (LH). Hizi FSH na LH kwa pamoja huchochea ovaries kuzalisha homoni za estrogen pamoja na progesterone. Kazi za estrogen na progesterone ni kusababisha mabadiliko katika ukuta wa uterus yaani endometrium ikiwepo kupata hedhi. Ili damu ya hedhi iweze kutoka nje, njia ya uzazi ya mwanamke haina budi kuwa huru yaani isiyo na matatizo yeyote yale.


  Amenorrhea husababishwa na nini?


  Visababishi vya amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke.


  Matatizo katika mfumo wa homoni: Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za hypothalamus, pituitary au ovary.

  Matatizo katika Hypothalamus: Matatizo katika hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na

  Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitary

  Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi. Ugonjwa huu

  hujulikana kama Kallmann syndrome
  Lishe duni na utapia mlo

  Uzito mdogo kuliko kawaida (kukonda kwa kupitiliza)

  Matatizo katika tezi ya Pituitary: Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na
  Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu au kwa kitaalamu Prolactinemia. Prolactin

  ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha. Hali ya kuwa na prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.

  Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya pituitary.

  Pituitary kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususani iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

  Kuharibika kwa tezi ya pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.
  Kuwa na historia ya kupata tiba ya mionzi inayohusisha tezi ya pituitary.

  Matatizo katika ovary: Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovaries ni pamoja na

  Kutozalishwa kabisa kwa mayai (Anovulation)

  Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu (Hyperandrogenemia)

  Ovary kuwa na vifukovifuko (Polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa

  Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovary kabla ya muda wake
  Ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner syndrome ambao humbatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida.

  Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia (genetic disease)
  Ukosefu wa kimaumbile wa ovary ambao hutokea wakati wa ukuaji

  Kufa kwa ovary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili
  Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri ovary

  Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango cha juu cha sukari aina ya galactose katika damu

  Matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi: Matatizo ya kimaumbile katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yanayoweza kusababisha ukosefu wa hedhi ni pamoja na

  Mwanamke/msichana kuzaliwa bila kuwa na uke, shingo ya uzazi au mji wa mimba (uterus)
  Kuta za uterus zinazotazamana kujishikiza pamoja

  Utando unaozunguka uke (hymen) kuziba kabisa na kukosekana kwa tundu la kupitishia damu ya hedhi (imperforate hymen)

  Kuwepo kwa utando unaokatiza katika uke unaozuia damu ya hedhi kushindwa kutoka
  Mabadiliko katika mwili wa mwanamke: Mambo yanayoweza kuathiri mwili wa mwanamke na kumfanya ashindwe kupata hedhi ni pamoja na

  Kula kiasi kidogo sana cha chakula kuliko kawaida au kula kupita kiasi
  Unene uliopitiliza au kupungua uzito/kukonda isivyo kawaida
  Uwepo wa magonjwa sugu kama kifua kikuu
  Utapiamlo
  Msongo wa mawazo
  Matumizi ya madawa ya kulevya

  Matumizi ya baadhi ya madawa hususani baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili
  Kuwa na hofu iliyopitiliza
  Kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi

  Dalili za Amenorrhea ni zipi?


  Kukosa hedhi siyo ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo kwa tatizo au ugonjwa fulani katika mwili. Kulingana na ugonjwa unaosababisha tatizo hili, kukosa hedhi kunaweza kuambatana pia na


  Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi, maumivu ya kichwa na matatizo katika kuona vitu ambavyo kwa pamoja vinaweza kuashiria uwepo wa uvimbe katika ubongo

  Mwanamke kuwa na nywele na vinyweleo vingi mwilini na kuota ndevu kama mwanaume hali inayoashiria kuwepo kwa wingi kwa homoni za kiume za androgen

  Ukavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku, au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatizo katika ovary
  Kuongezeka uzito kupita kiasi au kupungua kwa uzito isivyo kawaida
  Mwanamke kuwa na mhemko kuliko kawaida yaweza kuashiria kuwepo kwa matatizo ya kiakili na kisaikolojia
  Uchunguzi na vipimo


  Msichana yeyote aliyefikia umri wa kubalehe na kuvunja ungo na ambaye bado hajaanza kupata mabadiliko yeyote ya kubalehe katika mwili wake hana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Aidha msichana aliyefikia umri wa miaka 16 na ambaye bado hajaanza kupata hedhi anatakiwa pia kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


  Kwa wanawake waliokuwa wakipata hedhi kama kawaida lakini ghafla wakaacha kupata kwa muda wa miezi mitatu mfululizo au zaidi nao pia hawana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo hili.


  Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kuchunguza sababu za kukosa hedhi kwa mwanamke:


  Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha homoni za FSH, LH, TSH na prolactin ambazo uzalishwaji wake unachochewa na tezi ya pituitary, na pia kupima kiwango cha homoni ya estrogen inayozalishwa na ovary.

  Kipimo cha ultrasound ya nyonga kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo katika njia ya uzazi na pia kuchunguza hali ya ovary.

  CT scan au MRI ya kichwa kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo kwenye tezi ya pituitary au hypothalamus.

  Vipimo vya kufahamu ufanyaji kazi wa tezi ya thyroid

  Kupima damu ili kufahamu kiwango cha homoni ya prolactin katika damu
  Kuchunguza uterus kwa kutumia aina ya X-ray inayoitwa Hysterosalpingogram na kipimo kingine kiitwacho Hysteroscopy ambacho huchunguza chumba cha uterus.
  Matibabu ya kukosa hedhi


  Matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kufanyika nyumbani bila kuhitaji dawa, ingawa pia, kutegemeana na chanzo cha tatizo, yanaweza kuhitaji dawa na hata upasuaji wakati mwingine.

  Matibabu yasiyohitaji dawa


  Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo la kukosa hedhi kwa sababu ya kujinyima kula (wanaofanya dieting) na hivyo kupata upungufu wa virutubisho mwilini, wanashauriwa kula lishe bora.

  Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo hili la kukosa hedhi kwa sababu ya kuongezeka uzito kupitiliza, wanashauriwa kuwa makini katika aina ya vyakula wanavyokula ili kuwa na uzito unaotakiwa.

  Wanawake wanaokosa hedhi kwa sababu ya kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi wanashauriwa kujiwekea kiasi katika ufanyaji wao wa mazoezi.

  Iwapo kukosa hedhi kumesababishwa na msongo wa mawazo, ni jambo jema kutafuta njia za kushughulikia matatizo hayo na kuyatatua ili kuondoa msongo wa mawazo

  Inashauriwa kutokuvuta sigara na kuacha kunywa kunywa pombe.

  Matibabu yanayohitaji dawa: Matibabu ya kukosa hedhi hutegemea chanzo cha tatizo. Matibabu huelekezwa katika kutibu chanzo, na iwapo chanzo cha tatizo ni matatizo ya kimaumbile, upasuaji unaweza kufanyika. Kwa

  wanawake wenye matatizo ya kuwa na kiwango kingi cha prolactin, daktari anaweza kushauri matumizi ya dawa aina ya bromocriptine au pergolide. Kwa wanawake wenye upungufu wa homoni ya estrogen au wale

  wenye matatizo katika ovary zao, dawa zenye kurejesha homoni hiyo zaweza pia kutumika. Wakati mwingine dawa za uzazi wa mpango zaweza kutumika kurejesha mzunguko wa hedhi na pia kusaidia kuongeza kiwango cha homoni ya estrogen mwilini.

  Upasuaji: Upasuaji unaweza kufanywa iwapo kuna

  Uvimbe katika ubongo unaoathiri tezi ya pituitary na hypothalamus

  Matatizo katika njia ya uzazi ya mwanamke

  Je kukosa hedhi kunaweza kusababisha nisipate mtoto?


  Ikumbukwe kuwa, kukosa hedhi si ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo tatizo hivyo basi iwapo tatizo hilo lina uhusiano na kutunga mimba na kupata mtoto, uwezekano wa kupata mtoto utakuwa mdogo ikiwa tatizo hilo

  halitashughulikiwa. Matatizo kwenye tezi za pituitary, hypothalamus pamoja na ovary ambayo yana uhusiano

  mkubwa na kukosa hedhi, husababisha pia tatizo la ugumba. Iwapo matatizo hayo yatashughulikiwa ipasavyo, uwezekano wa kupata kupata hedhi na hatimaye kupata mimba huwa mkubwa.Kukosa Hedhi (Amenorrhea)

  Chanzo.https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/325245-kukosa-hedhi-amenorrhea.html
   
 16. gorgeousmimi

  gorgeousmimi JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2013
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 8,839
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Je anatumia dawa zozote za uzazi wa mpango?
  Mh hio PRIMOLUTE ni dawa inayotumiwa wa watu wanaopata hedhi isiyo na mpangilio(unregular mensturation)/mapungufu ya progesterone hormone na watu wanaodhamiria kusogeza siku za hedhi..Na hio dosage si sahihi vilevile haitakiwi kutumiwa kwa muda mrefu maximum ni siku 14.
  Hio CLOMID ni dawa ya kusaidia upate OVULATION(OVULATORY DYSFUNCTION IN WOMEN DESIRING PREGNANCY) inaweza kutumika incase of secondary amenorrhea na matumizi yake ni 50 mg daily for 5 days(from the 5.day of menstrual cycle if the pasient has menstruation).
  Since amejaribu hizo dawa mbili bila mafanikio anatakiwa apatiwe GONADOTROPINE-(follitropin alpha/follitropin beta/urofollitropin)..
   
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2013
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,532
  Trophy Points: 280
  Wakati ule nazaa ilikuwa nikijifungua nakaa miezi kama 24 kabla ya kuanza kupata siku tena. but was long time ago.
   
 18. gorgeousmimi

  gorgeousmimi JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2013
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 8,839
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Ehhh how old are you mamma?can i call you that?
   
 19. t

  thezila Member

  #19
  Sep 12, 2013
  Joined: Aug 4, 2013
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  na endapo anatumia dawa za uzazi wa mpango unamsaidiaje?
   
 20. m

  mama fulani Member

  #20
  Jan 27, 2014
  Joined: Aug 10, 2013
  Messages: 24
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wakuu. mimi ni mama ninaye nyonyesha mtoto wa miezi kumi sasa. nilianza kupata cku zangu mtoto alipokuwa na miezi miwili ila nimeshangaa ghafla mwezi huu cjapata cku zangu na si mjamzito.Niliugua typhoid mpaka sasa nipo kwenye dozi ya typhoid inaweza kuwa sababu? asanteni
   
Loading...