Msaada: Taratibu za kwenda kujitambulisha kupata uchumba

MulRZGM

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
1,015
746
Wakuu mbali mbali habarini za mchana,

Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha katika siku ya leo, Kama title ijielezavyo, ni hatua zipi ama nini kinatakiwa kufanyika ili nikajitambulishe.

Msaada wenu, naomba niweze fanikisha hili swala.

Karibuni!
 
Wakuu mbali mbali habarin za mchana, tumshukuru mwenyez mungu kwa kutufikisha ktk siku ya leo! Kama title ijielezavyo, ni hatua zp ama nn kinatakiwa kufanyika ili nikajitambulishe kwa kina flora then awe mchumba wangu? Msaada wenu naomba niweze fanikisha hili swala... Karibuni!
Samahani mkuu flora yule Wa mbasha?
 
mkuu huwa inaanza posa,lkn baada ya makubaliano kwanza kati yako na unayetaka kumchumbia,then unatafuta watu wawili wa heshima mmoja ni vizuri akawa anaifahamu familia unayopeleka posa ili iwe rahisi kupokelewa na mwingine mtu yeyote wa heshima wa kumpa kampani mpeleka posa,ikishapelekwa wakiikubali,hao washenga wako watakuletea majibu ya nini cha kufanya,though mara nyingi huwaga inaambatana na mahari,lakini kwa mila nyingi hapa tanzania huwaga zinafanana,kama nikikosea wajuzi zaidi watatusahihisha,kuna vitu vinaorodheshwa ambavyo kwa haraka haraka lazima uwenavyo,
1)mkaja wa mama(100,000=)na kitenge ukiweza.
2)kifunga uchumba(100,000=)
3)mbuzi wawili
4)majembe mawili,
5)mashuka mawili,
6)mablanketi mawili,
hivyo hapo juu ni vitu basic na ni lazima uvilipe vyote,
then na mahari ambayo huwa inaweza kuwa ni mifugo au pesa kutokana na mazingira ya unapoenda kuposa,
mimi kidogo naelewa ivo hope itakupa mwanga,wengine wataongezea,
pia hii mara nyingi ni kwa wakristo,wenzetu waislam nasikia hili suala huwa linakuwa cheap kidogo..
 
Nashukuru mkuu, ila me nataka nianze uchumba kwanza... Thus ndo nahitaj kufaham vitu gan vya kufanyika, au kwa maana nyingine nataka nkajitambulishe kwa kina flora ... Then mahali + ndoa bdae, upo apo mkuu?
 
Mkuu mm kwa uelewa wangu uchumba ni hali ya kua pamoja mkitazamiana kwa ajili ya kuoana na hatulipii uchumba kwa uelewa wng naeleweza hvyo ila watakuja walionauzoefu nayo watakufukulia mengi zaidi
 
Wakuu mbali mbali habarini za mchana,

Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha katika siku ya leo, Kama title ijielezavyo, ni hatua zipi ama nini kinatakiwa kufanyika ili nikajitambulishe.

Msaada wenu, naomba niweze fanikisha hili swala.

Karibuni!

Taratibu za kwenda kujitambulisha zinategemeana Kabila MMOJA na jingine au taratibu utakozoelekezwa kupitia kwa Michumba WAKO, taratibu za kawaida, unamuandaa mshenga na baadhi ya ndugu na huyo mshenga awe walau anafahamu mila au taratibu za lile Kabila, utaandika barua ya kuomba uchumba kwa wazazi wa binti, barua hii itapelekwa siku mnayoenda kujitambulisha ikiwa na kiasi kidogo cha fedha mf. 10,000/ - 50,000/= itasomwa na mshenga wa upande wa binti, ndipo watamuuliza binti Kama amekubaliana na Hilo, basi ikipitishwa unaruhusiwa, sasa hapa huwa kuna makubaliano baina yenu ninyi wachumba namba ya kuyaweka mambo sawa.....

Au unaweza kupeleka barua ya uchumba kwa shangazi wa mchumba WAKO akaipeleka kwa wazazi na wazazi wakaomba wakufahamu na kukuliza baadhi ya mambo ikawa imeisha.
 
Mm naona kama unajiforce kufanya kitu ambacho si cha maana sana.. Huyo demu si Uko naye na unatembea naye na anakuamini na wewe unamwamini.. Na labda baadhi ya ndg zake wanakujua.. Sasa upeleke barua kwa ajili ya kumridhisha kuwa utamwoa au? Muda ukifika Ukitaka kuoa.. Wewe peleka hiyo barua.. Maana ni afadhali mkitemana kusiwe na impact yoyote Kati yako wewe na family yake! Usidhani nipo hush Ila hii ni reality ya sasa.. Jitambulishe wakati issue za kuoa zipo karibu mkuu..!
 
Fact
 
Mkuu umenigusapo!
 
Back
Top Bottom