Msaada: Taratibu za kufata kwa aliyepotelewa na cheti

Sir Hemedi

Senior Member
Sep 28, 2016
112
120
Hatua gani za kuchukua baada ya kupotelewa na cheti cha form IV na kushindwa kuviona.
 
Nenda polisi wakupe loss report then tangaza gazetini kata kipande cha tangazo nenda necta watakupa replacement certificate. Process yote TSh 100,000
 
msaada unahitajika!
Unaenda polisi, kituo kikubwa kwa eneo ulilopo, utaandika loss report gharama ni 500 utapewa risiti.

Utaenda kwenye ofisi za gazeti la serikali utawaonesha hiyo ripoti ya polisi (ili wajiridhishe) utatoa tangazo, gharama haizidi 25,000.

Kisha utakata ukurasa mzima wa hilo gazeti wenye tangazo lako unaenda nalo NECTA.
Pale utagewa form, utaijaza utaenda kulipia 100,000 (mimi haikua cheti cha o level sijui kama gharama zinafanana) wana wakala pale pale.

Kuna vitambulisho utatoa kopi pamoja na hilo gazeti, vyote utaunganisha kwenye hiyo fomu na kuwarudishia kisha utasubiri kwa miezi 3 ndiyo utaenda kuchukua cheti chako.

Ila kitakua na neno 'Duplicate' kwa juu. Pia hii inafanya kazi kwa waliohitimu kuanzia 2005 kuja mbele.
 
Back
Top Bottom