Msaada: Tangu juzi kuna jogoo anawika kila ikifika saa mbili na nusu usiku (2:30)

Kwani ni nani alisema jogoo sharti awike asubuhi au mchana, na kwamba akiwika muda mwingine mfano usiku siyo sawa?
Huyo jogoo ni mjanja siyo mfuata mkumbo...
 
Bora huyo anawika saa 2:30
Nlikua na jojoo anawika muda wote, yani akikurupuka tu anawika na sio mara moja, ana kelele balaa, sa tatu, nne, tano, saba, ye anawika tu nikaona isiwe shida!!!!
Ukaona isiwe shida.....ukamfanyaje?

Lakini kumbuka jogoo ndio alikuwa saa ya asili toka enzi na enzi. Yaani akiwika unajua hii itakuwa ni saa ngapi.
 
Hata hvyo unamoyo sana, umepata hadi mda wa kuja kuomba ushauri huku yani mimi siku ya kwanza kusikia inawika tuhh, kisuu moja kwa moja ili nipate supu
 
Jaribu kuangalia CIMOS battery huwa ni kifaa kinachotumika kutunza time huwa ikiisha inafanya apoteze majira kiko hapo kwenye sternum fungua ubadilishe uweke ya jogoo aliekufa. Usisahau kuleta mrejesho
 
Ukaona isiwe shida.....ukamfanyaje?

Lakini kumbuka jogoo ndio alikuwa saa ya asili toka enzi na enzi. Yaani akiwika unajua hii itakuwa ni saa ngapi.
Ilibidi nimle tu...
Aah anawika sana afu kwa masifa kelele nyingi
 
Huyo jogoo atakuwa amepotea majira, majogoo huwika kwa kufuatana yani mmoja akiwika ndio wengine wanafuata. Iliwahi kutokea hapa home tulikuwa tunasikiliza mchezo wa redio 'RTD' unaitwa Twende na Wakati alafu kuna jogoo aliwika kwenye redio basi na jogoo wa hapa home akapokea na akawa anawika ifikapo majira yale ya mchezo wa redio..
Kitu cha kufanya ni kutafuta jogoo mwingine ili atakapowika waende sawa... ha ha ha haaaaa, gari mbovu huvutwa na nzima


Hii imenichekesha Mkuu, teknolojia inaathiri nature
 
Kwahiyo wewe unafugia kuku sebuleni? Au mabanda ya kuku yapo unapolala na kusikilizia radio? Maana kama mjasiriamali unatakiwa kuwa na kuku wengi so lazima wajengewe sehemu tofauti mbali kidogo na unapolala.
Mkuu suala la usalama ni kitu cha msingi kwa mjasiriamali, jenga banda mita 100 kutoka unapolala alafu uamke asubuhi kama utawakuta..
 
Bora huyo anawika saa 2:30
Nlikua na jojoo anawika muda wote, yani akikurupuka tu anawika na sio mara moja, ana kelele balaa, sa tatu, nne, tano, saba, ye anawika tu nikaona isiwe shida!!!!
Jogoo wako huyo kama wa kwenye kitendawili au fumbo flani hivi.....kama vipi nikupe mji ututajie ni jogoo gani huyo asiekua na muda wa kuwika? Yaani yeye ni wakati wowote tu, iwe usiku au mchana!!?
 
Back
Top Bottom