msaada tafadhali

Dec 4, 2010
18
0
Nimekutana na kipande cha utenzi kimenishinda kutafsiri kwa kiswahili rahisi, msaada please
Uwene wangapi watu wakwasi
walo wakiwaa kama shamasi
wamuluku dhana za adharusi
dhahabu na fedha wakhizinie

Nyumba zao mbake zikinawiri
kwa taa za koa na za sufuri
makiku yakele kama nahari
haiba na jaha iwazingie
 
kama ni kiswahili basi angalia visiwani na hata ngazija mkuu
 
Nimekutana na kipande cha utenzi kimenishinda kutafsiri kwa kiswahili rahisi, msaada please
Uwene wangapi watu wakwasi
walo wakiwaa kama shamasi
wamuluku dhana za adharusi
dhahabu na fedha wakhizinie

Nyumba zao mbake zikinawiri
kwa taa za koa na za sufuri
makiku yakele kama nahari
haiba na jaha iwazingie

Umewaona matajiri wangapi,
Wakiwaka kama jua
Wakimiliki dhana za kivita
dhahabu na fedha

Nyumba zao zikinawiri kwa heshima
Wakitembea kwa kujidai
haiba na jaha ikawazingira
 
Nyumba zao mbake zikinawiri
kwa taa za koa na za sufuri
makiku yakele kama nahari
haiba na jaha iwazingie

Umewaona matajiri wangapi,
Wakiwaka kama jua
Wakimiliki dhana za kivita
dhahabu na fedha

Nyumba zao zikinawiri kwa heshima
Wakitembea kwa kujidai
haiba na jaha ikawazingira

Hongera kwa kumudu kulainisha Kiswahili kilichotumika katika utenzi huu. Bila shaka utakuwa umeandikwa katika Kiswahili cha Lamu au Mvita. Hata hivyo,nafikiri umesahau kutafsiri ya maneno yaliyo kwenye nyekundu. Tumalizie tafadhali.
 
Aah Mammamia, ahsante kwa kunipa moyo, nipo najaribu tu maana iki ni Kiswahili cha kule Pate, Lamu. Unajuwa ili shairi ni la zamani sana, ni Utenzi wa Al-Inkishafi mtunzi ambaye anatuchorea taswira ya maisha ya anasa walivyoyaishi mamwinyi kabla ya kuanguka kwa Pate Lamu, uko Kenya. Twaelezwa kuhusu nyumba walizoishi zilizokuwa zinan'gara kwa taa na vito vya thamani.

Japokuwa mletaji kidogo amekosea kwenye kunakili. Shairi ni refu kiasi ila linasema Hivi

Nyumba zao mbake zikinawiri
kwa taa za kowa na za sufuri
Masiku yakele kama nahari
Haiba na jaha iwazingiye

Wapambiye sini ya kuteuwa
Na kula kikombe kinakishiwa
Kati watiziye kuzi za kowa
Katika mapambo yanawiriye

Tukirejea kwenye swali lako, hapo mshairi alikuwa anamaanisha taa za shaba (sufuri), zilizo changanywa na manukato (Kowa). Kama sitakuwa nimekosea...!
 
Ila neno Kowa ni aina ya Taa. Kama sikosei ni taa za chemli (chimney).
 
duh! kumbe mi sijui kiswahili kabisaaaa....maneno nimeyasoma but bulb haiwaki kichwani
 
Aah Mammamia, ahsante kwa kunipa moyo, nipo najaribu tu maana iki ni Kiswahili cha kule Pate, Lamu. Unajuwa ili shairi ni la zamani sana, ni Utenzi wa Al-Inkishafi mtunzi ambaye anatuchorea taswira ya maisha ya anasa walivyoyaishi mamwinyi kabla ya kuanguka kwa Pate Lamu, uko Kenya. Twaelezwa kuhusu nyumba walizoishi zilizokuwa zinan'gara kwa taa na vito vya thamani.

Japokuwa mletaji kidogo amekosea kwenye kunakili. Shairi ni refu kiasi ila linasema Hivi

Nyumba zao mbake zikinawiri
kwa taa za kowa na za sufuri
Masiku yakele kama nahari
Haiba na jaha iwazingiye

Wapambiye sini ya kuteuwa
Na kula kikombe kinakishiwa
Kati watiziye kuzi za kowa
Katika mapambo yanawiriye

Tukirejea kwenye swali lako, hapo mshairi alikuwa anamaanisha taa za shaba (sufuri), zilizo changanywa na manukato (Kowa). Kama sitakuwa nimekosea...!
ASANTE SANA X-PASTER, ni shairi zuri (baada ya kufafanuliwa).
 
Kwahiyo kinaitwa pia Kiswahili?
Na kama ni hivyo,vipo Viswahili vya aina ngapi wakuu?

Aina za uzungumzaji wa Kiswahili kunajulikana kama lahaja. Wakati wa ukoloni wa Uingereza kilichaguliwa kutumia Kiswahili cha Unguja (kiunguja) kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar. Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi uko Uganda.

Hivi leo lahaja zilizo orozeshwa rasmi ni hizi zifuatazo:

* Kiunguja: kisiwani Unguja (Tanzania) - kimekuwa msingi wa Kiswahili cha Kisasa.

* Kimrima: eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)

* Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)

* Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)

* Kimvita: eneo la "Mvita" au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya pili pamoja na Kiunguja.

* Kiamu: eneo la Lamu (Kenya)

* Kingwana: Kiswahili cha Kongo

* Shikomor: Kiswahili cha Komoro

* Shimaore: Shikomor cha Mayotte (Mahore)

* Shindzuani: Shikomor cha Anjouan (Komoro)

* Shingadzija: Shikomor cha Komoro Kuu

* Kimwani: Kaskazini ya Msumbiji na visiwa vya Kerimba

* Chimwiini: eneo la Barawa, kusini ya Somalia

* Sheng: Kiswahili cha mtaani Nairobi (Kenya) chenye maneno mengi ya asili ya Kiingereza, Gikuyu na lugha zingine za Kenya
 
Back
Top Bottom