Msaada tafadhali. Nataka kubadilisha jina la umiliki wa gari yaani ownership.

Kiganda

Senior Member
Oct 3, 2011
130
13
Nina gari nilinunua kwa mtu miaka mitano iliyopita. Muda wote huo nilikuwa sijabadili kutoka jina la muuzaji kwenda jina langu. Hivi juzi rafiki yangu kaniambia kwamba nikienda tu kubadili jina kuna faini hutozwa kwa kila mwezi niliochelewa tokea pale niliponunua hadi leo. Jamani mwenye ufahamu wa hilo msaada tafadhali.
 
Hakuna faini yoyote ya kila mwezi!
Ila kwenye masuala ya mauzo hua serikali (Tra) ina mkono wake,
Hapo ndio wajanja wa mjini unawaona wanakutengenezea mkataba "mzuri" wa mauziano ambapo hutolipa ada kubwa
 
Asante mkuu.
 
Hakuna faini, isipokuwa kama aliyekuuzia alikuwa kalisajili kama gari la kubebea abiria halafu we ukawa unalitumia bila kujua. Hapo mze itabidi utoboke kisawasawa. Lakini ni rahisi sana, kwa hapa dar ni zoezi la muda mfupi tu.
 
Faini inakuwepo kama risiti aliyokupa/hati ya malipo inaunesha tarehe ya nyuma zaidi ya mwezi! So mtafute/tafuta doc inayoonesha umenunua recently; don't even mention kuwa umenunua 5 month ago. Kuchelewa mwezi mmoja wanacharge 25% ya transfer charges, then kila mwezi unavyoongezeka wanacharge 10% more.
 
Nina gari nilinunua kwa mtu miaka mitano iliyopita. Muda wote huo nilikuwa sijabadili kutoka jina la muuzaji kwenda jina langu. Hivi juzi rafiki yangu kaniambia kwamba nikienda tu kubadili jina kuna faini hutozwa kwa kila mwezi niliochelewa tokea pale niliponunua hadi leo. Jamani mwenye ufahamu wa hilo msaada tafadhali.

Yuko sahihi; ujanja ni kuandikiwa risiti mpya yenye tarehe mpya! Hope hujaingia mkenge already kwa kupeleka an old receipt!
 
Hakuna faini yoyote ya kila mwezi!
Ila kwenye masuala ya mauzo hua serikali (Tra) ina mkono wake,
Hapo ndio wajanja wa mjini unawaona wanakutengenezea mkataba "mzuri" wa mauziano ambapo hutolipa ada kubwa

Mnapotosha mwenzenu; faini ipo! Mimi nimegongwa juzi tu; option sikuwa nayo kwani niliponunua ni registred tax payer na riceipt ilionesha nimenunua Aug 2011
 
Back
Top Bottom