MSAADA Tafadhali: Mume ni HIV+, Mke ni HIV- na ana Mimba ya Miezi 4

Genecandy

JF-Expert Member
Dec 13, 2017
491
882
Habari Dears na Wadau wote:

Jamani nahitaji ushauri, Mdogo wangu ameolewa mwaka 1 ulopita anasema kabla hawajaoana na Mumewe walipima mara moja na wote wakaonekana Wapo negative!

Wameishi mpaka kipindi hiki alichokuja kushika ujauzito alipoenda kuanza 'Clinic' ikabidi aende na Mumewe katika kupima ikaonekana Mume ni positive na yeye ni negative!

Kachanganyikiwa kwasababu Hospitali wamewaambia inabidi Mume aanze dozi ili asije kumwambukiza toto na yeye mwanywe japo ndo wameishi kipindi chote wanasex bila kinga kama Mume na Mke lakini yaye ndio kasalimika

Jamani ushauri anaohitaji anasema anampenda sana Mumewe na Mwanaume anaonekana hayupo sawa toka apate hayo majibu sasa imebidi amwahidi kwamba hatomuacha ili amsaidie asije kufa kwa stress!

Dears na Wada naomba mumsaidie kimawazo ili aendelee kuishi na Mumewe bila hofu ya kuja kuambukizwa. Afanye nini katika life style ya sasa ya kuishi ili waendelee kuwa happy na yeye kutokuwa na hofu ili aendelee kumuhudumia Mumewe kama awali!

PS; Mumewe bado hajaanza kutumia dozi mpaka sasa na hawafanyi chochote kwa siku kadhaa sasa.

Asanteni!
 
kkkkkk,hapo kwanza mume aseme alipoutoa?hakuna solution itakayopatikanA bila hilo swali kujibiwa kwa uaminifu.

Wachache wanaweza kubeba mizigo ya wengine,binafsi mwanamke kapata ukimwi wakati mimi sina na mwanzo tulikuwa wote hatuna na kaupata kwa kutokuwa mwaminifu basi ndoa imeishia hapo.

NinA mistakes zangu kibao zinanitafuna hadi leo hii,siwezi beba mistakes za mtu kwenye maisha yangu..
 
Kama mke ni negative, mme ni positive ni wakati wa kuachana, na kama mme nimwelewa hapaswi muingiza mke kwenye majaribu ya maamuzi, amjengee uwezo na amuache mtoto wa watu!
hapo ndo anapolia haamini ktk kuachana anamuhurumia hajui afanyaje
 
kkkkkk,hapo kwanza mume aseme alipoutoa?hakuna solution itakayopatikanA bila hilo swali kujibiwa kwa uaminifu.

wachache wanaweza kubeba mizigo ya wengine,binafsi mwanamke kapata ukimwi wakati mimi sina na mwanzo tulikuwa wote hatuna na kaupata kwa kutokuwa mwaminifu basi ndoa imeishia hapo.

NinA mistakes zangu kibao zinanitafuna hadi leo hii,siwezi beba mistakes za mtu kwenye maisha yangu..
Mumewe kamwambia ukweli kuwa inawezekana kaupata kbla hawajakutana coz hajawahi kumcheat na mke anaamini the way wanavyoishi life style yao
 
Ukweli ni kwamba hapo hapawezi patikana suruhu ya kudumu tena mimi nashauri kila mtu abaki na 50 zake.
Dah inasikitisha sana nikivaa uhalisia kwa walivyopendana namhurumia mdgo wangu ukizingatia ndo ndoa ya usichana na mtt wa kwanza
 
Nasikiaga kuna watu hawana milango ya kuingiza vijidudu vya hiv aseeh yawezekana huyo mke ni mmoja wao.

Pia kuna couple zinaitwa 'discordant couple,' yaani mmoja ve+na mwingine ve- ila mtanange kama dawa na hakuna kuambukizana

Akapime tena yawezekana kuna makosa kwenye upimaji(rejea ile kesi ya mwanamama kenya/uganda)
 
Wadau kwa wenye ushauri namwachia muhusika ajibu mwnywe maswali na michango yenu kwa usahihi zaidi!
 
Nasikiaga kuna watu hawana milango ya kuingiza vijidudu vya hiv aseeh yawezekana huyo mke ni mmoja wao.

Pia kuna couple zinaitwa 'discordant couple,' yaani mmoja ve+na mwingine ve- ila mtanange kama dawa na hakuna kuambukizana

Akapime tena yawezekana kuna makosa kwenye upimaji(rejea ile kesi ya mwanamama kenya/uganda)
Asante mpndwa lkn wakt tunapima walitupima na vipimo viwili tofauti na majibu yakaja sawa yaani walipima na kipimo kile chembamba baadae wakarudi kile cha plastic ikawa hvyo hvyo!!lbda kusbr baada ya miezi 3 tena au kwenda hosptali tofauti
 
jaribuni kwenda hosp. nyingine madame, naamini yuko poa ni makosa ya kibinadamu tu kwenye upimaji
 
Dah inasikitisha sana nikivaa uhalisia kwa walivyopendana namhurumia mdgo wangu ukizingatia ndo ndoa ya usichana na mtt wa kwanza
Ujue nimeshauri kila mtu abaki na hamsin zake kwa sababu mimi mwenyewe nimepitia changa moto kama hiyo.

Mwisho wa siku ilifikia hatua mke wangu akifanya kosa ukimsema yeye anaona kama unamnyanyasa kwakua yeye ana maambukizi.

Kwakweli Kuna mengi sana yatajitokeza baadae kama wanandoa hao wataendelea kuishi pamoja kama mke na mume.
 
Mkwaha Hilo naliona pia mana mume wangu amekuwa mpole sana japo awali tulikuwa tukikosana but now hana say yoyote mbali na hilo tukija kwny kujikinga na maambukizi inabidi tufanyaje or ni kondom tu!?
 
Hiii inaitwa kutest sumu kwa kulamba. Madaktari wameshauri nini kuhusu ndoa kuendelea? Kama ni mimi jamaa akubali tu matokeo amuache binti wa watu. Maaana hapo kama jamaa ni mlevi atakuja kumuambukiza mapema tu!
 
Mkwaha Hilo naliona pia mana mume wangu amekuwa mpole sana japo awali tulikuwa tukikosana but now hana say yoyote mbali na hilo tukija kwny kujikinga na maambukizi inabidi tufanyaje or ni kondom tu!?
Kuna uwezekano wa kufanya mapenzi bila kutumia condom ila hadi mupate ushauri wa wataalam kwanza na hata kuzaa pia inawezekana na mtoto akawa hana maambukizi.
 
Hiii inaitwa kutest sumu kwa kulamba. Madaktari wameshauri nini kuhusu ndoa kuendelea? Kama ni mimi jamaa akubali tu matokeo amuache binti wa watu. Maaana hapo kama jamaa ni mlevi atakuja kumuambukiza mapema tu!
Wanasema tunaeza ishi ila ndo awe anatumia ARVs na kusex asiache manii ndani kama tunafanya bila kinga vile vile kuhakikisha nisiwe dry wkt wa sex but ninahofu sina imani
 
Vipimo vya HIV kabla ya ndoa wengi hawaviwekei maana lakini ukifanya kama maelekezo huwa mnagundua mapema kabla ya ndoa.

Pimeni mara 3 yaani kila baada ya 3 months mtagundua kitu.

Tuyaache hayo. Turudi kwenye mada. Je, wenzetu hawa ni wakristo?? Je, walifunga ndoa kanisani?? Kama ni hivyo, hawana cha kuwatenganisha hadi kifo.

Hakuna chochote watafanya kuwatenganisha. Iliyopo watumie kinga tu lakini kazi iendelee. Jamaa naye ale dozzz mapema asije tuachia mjane na kachanga.

Niliwahi andika humu kuwa; Waweza tembea na mwenye ukimwi ila ukabaki salama japo mlipiga peku peku. Huu ni mfano mwingine. Wanandoa hawa wamekuwa wakienda peku siku nyingi tu. Tena tangu ndoa hawajawahi tumia kinga. Kama sio kiherehere cha mama kwenda kliniki na mumeye wala wasingeli gundua hilo tatizo. Nadhani jamaa anajua kumuandaa mkewe kisawasawa ndo maana hakina michubuko hatari ya maambukizi.

Sasa;
Waambie wasiende peku tena. Wameshajigundua hivyo peku sasa baasi. Watumie kinga.

Jamaa aache stress za kijinga atulize mzuka aishi kwa matumaini atamuoza huyo mwanaye na siku zake zitakuwa nyingi. Akianza kuwaza kuwa anamwacha mke mzuri atakufa mapemaaa.
 
Back
Top Bottom