Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 41,983
- 12,701
Katika vikao vya kifamilia wikiendi iliyopita kulikuwa na kesi iliyoletwa na kaka yetu mkubwa kwa wazee ili kupata ufumbuzi wa tatizo katika ndoa yake. Cha kushangaza wazee waliishia kucheka na kututaka vijana tuliokuwepo pale tumsaidie kaka, tukishindwa ndio tuwapelekee wao eti hilo lipo juu ya uwezo wetu. Tulibaki tumepigwa na butwaa na kikao kikafungwa hadi siku nyingine tena.
Kesi yenyewe ni kuwa jamaa mkewe hajisikii kabisa hamu ya kufanya mapenzi na jamaa anasema ni mwezi wa tatu hajapata haki yake ya ndoa. Na akiomba mchezo kwa mkewe inakuwa ni ugomvi na kuonyesha msisitizo muda wa kulala mkewe anapiga c...pi, tait, na jinzi na mkanda juu(hali ya hewa inaruhusu). Kwa kuwa hapa kuna wataalamu wa mambo haya nadhani tutapata japo pa kuanzia kwa ushauri utakaotolewa hapa.
Nawasilisha.