Msaada Tafadhali: Mkewe Hajisikii!!!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,701
Katika vikao vya kifamilia wikiendi iliyopita kulikuwa na kesi iliyoletwa na kaka yetu mkubwa kwa wazee ili kupata ufumbuzi wa tatizo katika ndoa yake. Cha kushangaza wazee waliishia kucheka na kututaka vijana tuliokuwepo pale tumsaidie kaka, tukishindwa ndio tuwapelekee wao eti hilo lipo juu ya uwezo wetu. Tulibaki tumepigwa na butwaa na kikao kikafungwa hadi siku nyingine tena.
Kesi yenyewe ni kuwa jamaa mkewe hajisikii kabisa hamu ya kufanya mapenzi na jamaa anasema ni mwezi wa tatu hajapata haki yake ya ndoa. Na akiomba mchezo kwa mkewe inakuwa ni ugomvi na kuonyesha msisitizo muda wa kulala mkewe anapiga c...pi, tait, na jinzi na mkanda juu(hali ya hewa inaruhusu). Kwa kuwa hapa kuna wataalamu wa mambo haya nadhani tutapata japo pa kuanzia kwa ushauri utakaotolewa hapa.
Nawasilisha.
 
Huko Katavi hawanyimi bana....! Vinginevyo, kuna walakini...! Mwambieni shem yenu awe muwazi ili mpate kutibu hali hiyo....!
 
Hayo ni matokeo ya tatizo lilopo ndani ya ndoa. Kaeni nao mmoja mmoja waeleze matatizo yao!
 
Huko Katavi hawanyimi bana....! Vinginevyo, kuna walakini...! Mwambieni shem yenu awe muwazi ili mpate kutibu hali hiyo....!
Bado huyo shem hajaulizwa kwa nini anamfanyia hivyo mwenzake. Hapo kwenye walakini sina uhakika.
 
I Corinthians 7:2-5
2 But since sexual immorality is occurring, each man should have sexual relations with his own wife, and each woman with her own husband. 3 The husband should fulfill his marital duty to his wife, and likewise the wife to her husband. 4 The wife does not have authority over her own body but yields it to her husband. In the same way, the husband does not have authority over his own body but yields it to his wife. 5 Do not deprive each other except perhaps by mutual consent and for a time, so that you may devote yourselves to prayer. Then come together again so that Satan will not tempt you because of your lack of self-control.
 
Katavi, inawezekana kuna kitu ambacho kimemkwaza huyo mama thus why hataki,jaribuni kukaa nae na mwongee nae peke yake anaweza kuwaeleza ambacho kimemsibu mpaka amechukua hayo maamuzi ya kugomea hiyo issue.
 
Amwambie anataka kuoa mke mwingine atakayemsaidia mahitaji ya kindoa hivyo anaomba ushauri kwa mkewe
 
Katavi, inawezekana kuna kitu ambacho kimemkwaza huyo mama thus why hataki,jaribuni kukaa nae na mwongee nae peke yake anaweza kuwaeleza ambacho kimemsibu mpaka amechukua hayo maamuzi ya kugomea hiyo issue.
Sasa kwa nini asimueleze mwenzake kama ni hivyo. Asante kwa ushauri tutalifanyia kazi.
 
I Corinthians 7:2-5
2 But since sexual immorality is occurring, each man should have sexual relations with his own wife, and each woman with her own husband. 3 The husband should fulfill his marital duty to his wife, and likewise the wife to her husband. 4 The wife does not have authority over her own body but yields it to her husband. In the same way, the husband does not have authority over his own body but yields it to his wife. 5 Do not deprive each other except perhaps by mutual consent and for a time, so that you may devote yourselves to prayer. Then come together again so that Satan will not tempt you because of your lack of self-control.

kwa jina la baba,na lamwana na la roho mtakatifu= AMEEEEEEEEEEEEEEEEEEEN
 
Lakini mke mwenyewe ni kuwa hana tatizo jingine lolote nikiwa na maana kuwa wanaishi vizuri kabisa na wanalea mtoto wao mmoja wa miaka mitatu kama kawaida, kiasi kwamba watu tulio nje tunaona kama hakuna tatizo. lakini kaka aliposhindwa ndio akaliwakilisha kwetu. Tatizo alilonalo mkewe ni kuwa hajisikii kufanya mapenzi!
 
wende hospital pengine mkewe hana hormones..

Kuna kila dalili kuwa ana tatizo hili. Kuna ndugu yetu mmoja kashauri atafute dawa kwa waganga wa kienyeji au za kichina huenda zitamsaidia ingawa hili halijaafikiwa bado.
 
aulize historia ya ,mkewe huenda alshawahi kuwa msagaji/msagwaji na uenda bado anaendelea nao
 
Pia yawezekana ni psychological disorders, anaweza akawa anahusisha tendo la ndoa na matukio yasiyo mazuri huko zamani (utotoni?). Madaktari watamsaidia.

Inawezekana, lakini mwanzo jamaa anasema mke alikuwa na ushirikiano wa hali ya juu wakati wa tendo lakini kadri muda ulivyokuwa unaenda ndio uwezo wake ukawa unapungua na mwisho akawa hataki kabisa. Lakini ni watu ambao wapo katika ndoa kwa muda wa miaka minne na wana mtoto mmoja.
 
Back
Top Bottom