Msaada tafadhali: Chuchu kuuma

Habari za Eid wapendwa,

Naombeni ushauri kwa anayejua, ni nini kinasababisha chuchu kuuma, mwenzenu chuchu zinauma mno na kuwasha, kipindi cha nyuma zilikuwa zikiuma labda nikiwa MP lakini sasa hivi zinauma tu bila sababu, kwa wanawake wenzangu huwa mnakumbana na hii hali?

Naombeni msaada tafadhali;
cc: espy
Paprika
emmyta
Sakayo
Valentina
miss chaga
Miss Natafuta
Nifah
............
............
...........

Nawengine wotee ila kama wewe ni ke
Jibu
  • Kama ulivyo ulivyo eleza hapo juu kua ilikuw ni kipindi cha MP tu ila sasa ni muda wowote, bila shaka itakuwa ni tatizo la PMS (pre menstrual syndromes) na hili linasababishwa na hormone imbalance. Hii ina weza mtokea mwanamke yeyote ila mara nyingi zaiidi ukiongezeka uzito, panapotokea blockage ya hormone ndio inaleta hiii hali. for further info click Dr Luu
  • Dawa ya hormone inbalance ipo ni DM au pata tiba kwa tabibu aliye karibu nawe.
  • Kama unamuwasho punguzaa kuva bra zinazo bana sana, huweza kuzuia flow ya damu kupita na kusabisha muwasho. Pia inaweza leta vipele vya joto punguza kuvaa ukiwa maeneo ya nyumbani relax. Hii pia iko kwa wanaovaa taiti zakubana sana pindi wanapovua wanasikia muwasho both ke na me. Waafrica miili yetu ina joto sana.
Note
Nimeona watu waki-comment kuhusu kansa, kwa kansa ya titi nikutoe hofu kidogo iko hivi hakuna maumivu yeyote unayoweza kusikia kwa viashiria vya mwanzo hua ni uvimbe usio na maumivu kwa maelezo zaidi pitia hii tovuti ya serikali bofya


Ushauri
  • Pata tiba
  • Jitahidi kufanya mazoezi. Unaweza kuanza mazoezi madogo madogo anza kufanya kwa dk 2 kwa siku then unaongeza dk 5 hivyo hivyo unaongeza mpaka dk 30 na kuendelea; lengo nikutengeneza mazoea/tabia yakufanya mazoezi anza na streching kisha kukimbia 1km/day angalau siku 2 kwa wiki. Discipline inahitajika kwenye hili.
  • Kula organic foods, punguza ulaji wa vyakula nyama, mayai na maziwa.
  • kufunga/fasting pia ni tiba. Unaweza funga na ukwanywa maji tu kama itakusumbua kuacha kula kabisa.
Asante!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom