Msaada tafadhali,binti kagundua mme mtarajiwa anaigiza ulokole, kumbe .......!

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,222
2,925
Habari zenu wapendwa,,kuna binti flan nampa jina la Jen,huyu jen na familia yao yote ni walokole,jen elimu yake ni ya form four na ana miaka 20 kwa sasa,wazazi wake ni wakulima tu na wana elimu ya darasa la saba na yeye ndio mtoto wa kwanza ana wadogo zake wawili.

Mwezi wa pili mwaka huu alikutana na jamaa mmoja maeneo ya kibaha akiwa anatoka kanisani mida ya saa mbili usiku kwa vile mvua ilikuwa inanyesha yule jamaa akapaki gari na kumpa lifti ktk maongezi yao jamaa akasema ni mgen sehemu ile yeye anaishi dar ni mfanya biashara wakapeana contact alipofika anaposhuka karibu na kwao jamaa akamshusha na kuendelea na safari zake.

Basi tangu siku ile jen akaendelea kuwasiliana na jamaa na wakawa marafiki akamkaribisha kanisani kwao jamaa akawa anakuja mpaka naye akaokoka baada ya miezi km mitatu jamaa kwa vile alijiweka karibu na wazee wa kanisa na kuwa anatoa misaada na akawa anaheshimika pale kanisani basi akawajulisha wazee kuwa amempenda yule binti na anataka kumuoa kwani ameonna anamfaa,Basi wazee wakakubali na mipango ya uchumba ikaanza kwa taratibu za kilokole.

Katika harakati zote hizo aliwaleta baadhi ya ndugu wa binti na kuwatambulisha kwa watu aliodai ni dada zake maeneo ya magomen ambapo alisema anaishi nao wale ndugu pamoja na jen waliamini na akawa anaenda kuwatembelea mara chache na jamaa akampeleka kkoo kwenye kwenye duka la nguo ambalo alisema ndio ofic yake na yy ndio mmiliki so akaaminika na kila kitu kikaenda sawa.

Harusi imepangwa kufungwa jmosi ijayo,sas juzi jmosi jamaa akaenda kumchukua mchumba wake waje mjini kukamilisha kununua baadhi ya vitu amabvyo walikuwa hawajakamilisha kwa ajili ya harusi,kabla ya kwenda madukani akampeleka hotelin maeneo ya magomen jen hakuwa na wasiwasi akashangaa jamaa kachukua chumba na kumtaka waingie ana maongezi jen anasema alianza kupata hofu ila akaingia jamaa akaagiza vinywaji na vyakula na kuanza kuongea ambapo jamaa alimwambia jen anataka wafanye mapnz ikiwa ni sehemu ya kufahamiana na itakuwa ni siri kati yao na kwa vile wameshapima afya na arusi ni wiki ijayo haina shida,jen akakataa basi jamaa wala hakulazimisha akamwomba anywe wine jen hajui wine na hajawahi kunywa akabembelezwa mpaka akanywa na akawa najisikia km kulala akajiegesha na jamaa akawa anachati kwenye komyuta na kunywa wine.

Jamaa akajua jen kalala kumbe hajalala na anaona na kusikia kila kitu hata jamaa alipokuwa anaongea na simu,basi kuna wakati jamaa akavua shati jeni akaona na kushangaa jamaa mwili mzima umejaa tatuu!basi akiwa anavua shati simu ya jamaa ikaita akawa anaongea na watu kuhusu biashara ila ktk maongezi akawa haelewi ni aina gani ya biashara na gafla jamaa akatoka kwenda kuongelea nje ya chumba jen akasogea mlangoni akasikia jamaa akimwambia huyo mtu kuwa karibia atatoka kwenye kifungo cha ulokole feki kwan arusi ni jmosi na akishaoa basi na ulokole ndio mwisho.

Jen aliposikia hivyo akachanganyikiwa na zile tatuu ndio zikammaliza kbs,na kurudi kitandani jamaa aliporudi jen akamwambia anajisikia kuumwa anaomba waondoke jamaa akakaataa ila jen alipoanza kulia jamaa akakubali na wakarudi kibaha hawakwenda madukani tena,alipofika kwao akawaambia wazazi na ndugu zake hakuna aliyeamini na wote wanamtetea jamaa,na wanachofanya ni kumwombea jen wasema kaingiwa na pepo,badala ya kutafakari na kutafuta suluhisho la tataizo.

Jana jen akaja kwa rafiki yake ambaye ni jiran yangu akamsimulia huo mkasa,wakaamua kwenda kule magomen kwa wale wifi zake ikabidi awaeleze lile tatizo wale wadada wakaingiwa na huruma wakamwabia ukweli kuwa yule wala sio ndugu yao ni rafiki wa kaka yao anayeishi nje ya nchi na anatumia chumba cha kaka yao na nimuuza unga hata hilo duka analosema ndio oficn kwake ni uongo na walishindwa kumwambia mapema coz hakutaka kuwa karibu nao na walionekana wanapendana na wakamwomba vyovyote atakavyoamua asiwataje kwan atawagombanisha mpaka kwa kaka yao ambae ndio km mzazi wao ndio anawalea hapa mjin!

Hapo ndio jen akachanganyikiwa,wakaamua kwenda na kule kkoo bahati mbaya wakakuta duka limefungwa kumbe hawaji kazin cku za jpili.mpaka hapo anawasiliana na mchumba vizuri tu bila kumjulisha wala kuonyesha tofauti yoyote,jana jion wakautana na jamaa maeneo ya ubungo akamrudisha kibaha,usiku ameongea na wazazi na baadhi ya ndugu hakuna anayemuelewa wanamuona muongo na wanamtetea jamaa,mpaka wazazi wakaanzisha maombi wanamwombea jen eti kaingiwa na pepo na wamemkataza asiondoke hm tena mpaka siku ya arusi.

Leo asubuhi imebidi nimpigie jiran yangu anambie kinachoendelea akanambia jen kampigia analia amechanganyikiwa na hamtaki tena huyo bwana,wazazi hawamwelewi kinachofanyika ni maombi tu na jamaa kwa vile ana pesa kawashika wazazi vizuri wanamkubalia kila analosema huyo jamaa yani wanamthamini kuliko hata jen,na baba kasema lzm ndoa ifungwe,sasa jen anahitaji msaada wa mawazo afanyeje yy hataki kuolewa tena baada ya kugundua jamaa ni tapeli tu,na wazazi wanataka aolewe,nyumbani haruhusiwi tena kutoka sasa hajui la kufanya amechanganyikiwa jirani yangu ameiomba tushirikiane namna ya kumsaidia jen hata kimawazo nami nimeamua kuwaletea wana jamii tunaomba mawazo yenu kwan jen anasema ni bora afe kuliko kuolewa na huyo mtu,wazazi hawajali wanafanya maombi tu na wanataka aolewe.
Nawasilisha.
 
mume mwema hutoka kwa mungu!! asife moyo ,aonyeshe msimamo wake wa kutokutaka kuendelea na hilo liuza udaga,awashawishi wazazi wake wamuelewe!
My dia shuhuli ndio iko hapo,wazazi na ndugu wanajua ni mlokole safi na mshiko alionao ndio kbs!
 
Duh! Jen ameharakisha sana. Miezi 3 ni michache sana kuweza kumuelewa mtu na kuamua kufunga nae ndoa. Kama angejipa muda zaidi wa kumchunguza jamaa angemuelewa na angeweza kumkimbia kabla hawajatangaziana ndoa.
Mwambie awaeleze wazazi ukweli kuhusu jamaa na awaombe muda zaidi wa kumchunguza. Kama vipi apange dili ajifanye mgonjwa mahututi siku mbili au moja kabla ya harusi.
Au amwambie jamaa ukweli aliogundua na amwambie hataki kuolewa nae. Mpe pole sana.
 
ndoa imekuwa ya kulazimishana amwite huyo kijana aeleze ukweli mbele ya wazazi wake.......huyo dada amepata ufunuo kabla ya harusi?........haitakuwa sahihi kuwa na ndoa inayokupa hofu/wasiwasi............kutokana na uchunguzi huo kijana ameokoka kinafki.........ikishindikana amkatae mbele ya madhabau!!!!!
 
halafu utakubali vp kuolewa na mtu mmejuana miezi 3. Akumbuke anaolewa yeye na si wazazi wake. Afanye maamuzi kwa kumshirikisha Mungu wake
 
Duh! Jen ameharakisha sana. Miezi 3 ni michache sana kuweza kumuelewa mtu na kuamua kufunga nae ndoa. Kama angejipa muda zaidi wa kumchunguza jamaa angemuelewa na angeweza kumkimbia kabla hawajatangaziana ndoa.
Mwambie awaeleze wazazi ukweli kuhusu jamaa na awaombe muda zaidi wa kumchunguza. Kama vipi apange dili ajifanye mgonjwa mahututi siku mbili au moja kabla ya harusi.
Au amwambie jamaa ukweli aliogundua na amwambie hataki kuolewa nae. Mpe pole sana.
Asante sisy,tatizo ni kwamba wale wazazi ulokole umewaingia kupita kiasi na jamaa alivyojidai ameokoka anahudhuria mpaka mikesha mbaya hapo ndio hata yy akamwamini, alfu kawa mdhamin wa familia anaprovide mahitaji yote.
Anataman kumwambia jamaa ukweli lkn je atakubali na keshatumia garama za kuandaa harusi na tayari wazazi wako upande wa jamaa itasaidia da husni?
Hapa labda hilo la kuugua au atoroke japo sina uhakika km atakuwa na ujasiri wa kutoroka!
 
ndoa imekuwa ya kulazimishana amwite huyo kijana aeleze ukweli mbele ya wazazi wake.......huyo dada amepata ufunuo kabla ya harusi?........haitakuwa sahihi kuwa na ndoa inayokupa hofu/wasiwasi............kutokana na uchunguzi huo kijana ameokoka kinafki.........ikishindikana amkatae mbele ya madhabau!!!!!
Yani uko sahihi kbs my dia,mungu amemwonyesha mapema na ndio maana anapata upinzani,na hili la kukataa mbele ya mchungaji nahisi litakuwa zuri km watamlazimisha mpaka siku ya harusi.
 
Asante sisy,tatizo ni kwamba wale wazazi ulokole umewaingia kupita kiasi na jamaa alivyojidai ameokoka anahudhuria mpaka mikesha mbaya hapo ndio hata yy akamwamini, alfu kawa mdhamin wa familia anaprovide mahitaji yote.
Anataman kumwambia jamaa ukweli lkn je atakubali na keshatumia garama za kuandaa harusi na tayari wazazi wako upande wa jamaa itasaidia da husni?
Hapa labda hilo la kuugua au atoroke japo sina uhakika km atakuwa na ujasiri wa kutoroka!

unajua sisty huyo mdada maamuzi yoyote atakayofanya risk yake ni kubwa ila maamuzi ya kuolewa na hilo balazuli risk ni kubwa zaidi.
Tena awe makini na mipango atayofanya maana huyo jamaa anaweza hata kumchinja. Mwambie asingizie tu ugonjwa na mipango yake aifanye kwa umakini. Akitoroka ni rahisi kukamatwa na hali itakuwa mbaya zaidi. Poleni tena.
 
Wewe na huyo jirani, fungeni safari mpaka huko Kibaha kwa Wazee wa kanisia muwajuze ukweli wa mambo haya ikibidi waihairishe shughuli hadi ukweli ujulikane.
Na kwa uhakika jamaa akijua dili lake limejulikana basi atakachofanya ni kuingia mitini, na hiyo ndio nusra yake Jen!
Chukua hatua sasa!
 
Asante sn,Uko sahihi sisy,kwanza inaonekana huyu mtu ana mtandao mkubwa na inawezekana ananjuana na watu wengi!
Kwa vile mda umeshaisha inabidi augue tu siku ya haruc ipite kwanza ndio mambo mengine yatajulikana badae!
 
Uko sahihi lkn kumbuka mtu tunayedili naye ni mbabe na ana uwezo na ana mtandao mkubwa,na tayari ameshatumia pesa yake mwenyewe kwa hiyo arusi na maandalizi yake,pili anachojua ni kwamba kila kitu chake ni siri,alafu na wazazi wanamuamini kupita kiasi huko kanisani pia wanamfahamu na wanmheshimu pia!
Kiukweli hili sio dogo la sie wawili kupambana nalo,hapa kinachotakiwa ni kutafuta sababu ya kutofungika kwa ndoa ili upatikane muda wa kuwafahamisha watu wote ukweli wa huyu mtu bila yeye kujua na ajikute anakataliwa na watu wote na sio huyu binti pekeyake!
 
Asante sn,Uko sahihi sisy,kwanza inaonekana huyu mtu ana mtandao mkubwa na inawezekana ananjuana na watu wengi!
Kwa vile mda umeshaisha inabidi augue tu siku ya haruc ipite kwanza ndio mambo mengine yatajulikana badae!

halafu isijekuwa huyo mtu ana mtandao mpaka jf.
 
Hii ntarudi kuisoma_kwa sasa niko busy kubrash na kushona viatu vya wateja wangu,...yaani ni ndefu
 
Back
Top Bottom