Msaada Tafadhali; aende chuo gani kwa matokeo haya?

Eternal_Life

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
812
1,672
Wakuu nina mdogo wangu wa kiume, amemaliza form 4 2016, kwa bahati mbaya matokeo yake hayakuwa mazuri na yanatia aibu sana(D tatu na C moja). Sasa dogo kazunguka na maisha ya mtaani kwa mwaka na kitu sasa.

Jana amekuja kwangu na kuniambia anaona maisha yamekuwa magumu sana na anataka kurudi shule asome (siyo kurudia form). Mimi niko tayari kumsaidia kurudi shule, tatizo linakuja sijui wapi pa kuanzia na hayo matokea yake ya form form.

Tafadhali mwenye kujua ninaweza kumpeleka chuo gani labda akaanza level ipi ili hatimaye apate nafasi ya kujiunga diploma na hatimaye degree.

Nawasilisha.
 
Mpeleke veta au gereji mkuu utona matunda yake mda sio mrefuu elimu yetu ya kumeza madesa na kumeza chandi haina msaada wowote katika maisha harisia.... mbaya zaid hakuna ajiri.... tunamaliza vyuo tunaanza maisha mapya ya mtaani.... elimu ya bongo so sad.... Ni ushauri tu
 
kabixa yaan mpeleke akapate ujuzi ila kurudia hakuna ishu kabixa elimu hii kumeza vitu vigumu at ze end unarudi Kitaa huna ajira upo upo tu.. i hate it
 
Mpeleke veta au gereji mkuu utona matunda yake mda sio mrefuu elimu yetu ya kumeza madesa na kumeza chandi haina msaada wowote katika maisha harisia.... mbaya zaid hakuna ajiri.... tunamaliza vyuo tunaanza maisha mapya ya mtaani.... elimu ya bongo so sad.... Ni ushauri tu
Wangu kapiga gereji na welding kwa miezi sita tu. Sasa hivi anajitegemea. Kurudia ni UZUZU
 
Back
Top Bottom