Msaada; Sumu /dawa gani inafaa kuangamiza nzi?

Wakuu,

Naomba kujua dawa au simu ambayo itaangamiza nzi ndani na nje ya nyumba maana kipindi hiki cha mwisho wa mwaka naona kama ndio msimu wao wa kuongezeka sasa wamekua kero mno.

Naomba kujulishwa ni sumu gani nzuri ambayo haina madhara kwa binadamu

Asante.View attachment 1651652
Mkuu tafuta dawa ya ngao ya maji kisha pulizia kuta, nyavu za madirisha na kokote kule. ndani ya miezi mitatu nzi, mbu, mende na kadhalika wakigusa eneo ulilopulizia dawa wanakufa

kasheshe ni wapi unaipata hiyo dawa ya ngao. ukiipata pls tujuzane
 
Huo sasa ndio mtihani wenyewe
 
Wakuu,

Naomba kujua dawa au simu ambayo itaangamiza nzi ndani na nje ya nyumba maana kipindi hiki cha mwisho wa mwaka naona kama ndio msimu wao wa kuongezeka sasa wamekua kero mno.

Naomba kujulishwa ni sumu gani nzuri ambayo haina madhara kwa binadamu

Asante.View attachment 1651652
sababu ya Nzi, ni kuacha wazi yale mamifuko ya taka, halafu wengi huweka mifuko hiyo karibu na dirisha.

Kama unabisha angalia uone, kama hauna hayo mamifuko.
 
Sidhani kama dawa ipo ila kuna kakifaa nilikaona alibaba wanadai kana uwezo wa kuua mbua na Nzi lakini kwenye Giza

Ipo dawa moja hivi ya unga kiboko ukinyunyuzia dk 5 nyingi wanaanguka baada ya dk 10 nyumba nzima kimyaaa unafagia unapiga deki huwaoni hata siku mbili
 
Aiseeh mm nasumbuliwa na mende wadogo wadogo, yaan nimetumia rungu wamekataa, nimenunua vidonge wamekataa,
Mwenye kufaham dawa ya kuwaangamiza Hawa mende wadogo wadogo naomba anijuze
 
Inaitwaje hio dawa,bei yake na inapatikana wapi?
 
sababu ya Nzi, ni kuacha wazi yale mamifuko ya taka, halafu wengi huweka mifuko hiyo karibu na dirisha.

Kama unabisha angalia uone, kama hauna hayo mamifuko.

Halafu pia kama kuna mtu analala uchi wa mnyama basi anatakiwa awe anafua mara kwa mara.
Mkuu situmii hayo mavyombo ya taka unayosema,nina shimo la taka na lipo mbali tu na nyumba

Kuhusu watu wanaolala uchi kufua nguo sijaelewa vina uhusiano gani?
 
Aiseeh mm nasumbuliwa na mende wadogo wadogo, yaan nimetumia rungu wamekataa, nimenunua vidonge wamekataa,
Mwenye kufaham dawa ya kuwaangamiza Hawa mende wadogo wadogo naomba anijuze
Nenda maduka ya viatilifu kuna dawa inaitwa Lava(kama utaipata maana kuna kipindi ilipigwa marufuku ilikuwa inatoka nje haikusajiliwa) ukikosa ulizia dawa zingine zipo nzuri,ila inabidi uwe na chupa ya Ku spray,unaspray sehemu zote wanakojificha baada ya wiki unarudia na baada ya mwezi mmoja unarudia tena hapo itakuwa umewamaliza
 
Mkuu situmii hayo mavyombo ya taka unayosema,nina shimo la taka na lipo mbali tu na nyumba

Kuhusu watu wanaolala uchi kufua nguo sijaelewa vina uhusiano gani?
Kama upo dar, unyevu nyevu wa mwili unaweza sababisha uvundo kwenye godoro iwapo unaishi maeneo yenye joto kali na hauna AC.
Hiyo nayo ni reason.
 
Wakuu,

Naomba kujua dawa au simu ambayo itaangamiza nzi ndani na nje ya nyumba maana kipindi hiki cha mwisho wa mwaka naona kama ndio msimu wao wa kuongezeka sasa wamekua kero mno.

Naomba kujulishwa ni sumu gani nzuri ambayo haina madhara kwa binadamu

Asante.View attachment 1651652
Kwanini uwaue sasa, huwezi waelezea kistaarabu wakaondoka?
 
Back
Top Bottom