Msaada: Simu yangu ina tatizo la "Ghost touch" na sijawahi hata kuidondosha

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,764
2,000
Hii simu naitumia ni miezi mitano sasa sijawahi hata kuidondosha ukiiona kama mpya kabisa ila imeanza kuwa na tatizo la kutach ukibonyeza mbili inabonyeza tatu

Ukislide kwa juu inaslide kwa chini imekua ni shida wakati mwingine inaanza kujibonyeza tu unakuta ishafika watsaap

Nimerestore simu hamna kitu

Nilidhani labda ni protector nikaitoa nikatumia bila protector lakini wapi nimeweka protector mpya naona mchezo ndo huo huo

Wakati mnasolve vipi hili tatizo?

Pili ikipata moto sana inakua na tatizo la kutokea kwa chenga kwenye kioo screen flickering/screen blinkinh yaani km zile chenga za deki za kizamani za mikanda wakati unapeleka mkanda mbele...then inatokea inapotea
 
zous

JF-Expert Member
Sep 25, 2017
466
1,000
Tatizo ushalijua kua cm inaji touch .njia ni moja peleka kwa fundi hakuna kingine waeza fanya
 
Darren2019

JF-Expert Member
Nov 23, 2019
684
1,000
Narudia tena, taja aina ya simu vinginevyo uzi utajaa stori tu. Hii itasaidia walioexperience waweze kuchangia.
Mfano me natumia Samsung tangu nianze kumiliki smartphone unafikiri ntachangia nini kwenye mada inayohusu iphone?
Kuna mambo ya kuzingatia km kampuni, toleo la simu, operating system, aina ya kioo n.k
 
Opay m1 lte ipo kama samsung a01
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom