Msaada: Sijui ni ugonjwa au afya

Oxpower

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,139
2,991
habari ndugu zangu
naombeni ushauri na kujuzwa tafazali
ni takriban mwaka wa pili huu kila nikinywa maji natokwa na jasho sana,mwanzon jasho likikua linatoka kawaida tu lakini saiz naona hali inazidi,jasho linatoka kwa wingi saana,nmejaribu kuwauliza watu wangu wa karibu wanasema n afya,lakin nmekua sina iman na majibu yao kwakua wengine siwaon wakitoka jasho kama mimi.jamani naomba msaada wa kitaalam tafazali
 
Sijakataa hospitali zipo,lakin humu ndani kuna watu wa aina mbali mbali na wana ujuzi tofauti,wengine n madaktar na wengine pengine wanatatizo kama hili kwahiyo nmeweka hapa ili nipate ushaur wakitaalam na wa experience
 
Naishi dar,ila saiz shuguli zangu zote nafanyia kibaha
 
Anyway,sio kila kila mara mtu anapotokwa na jasho sana basi ana ugonjwa.Mara nyingi watu wanatokwa na jasho jingi bila ya sababu ya msingi.

Kwenye ngozi yetu kuna vijitezi vidogo vidogo vinavyotoshatoa jasho.Vinafanya hivyo kama njia ya kutoa nje taka mwili.Katika mazingira ya joto kama dar na of course kibaha kuna joto,kwa hiyo si ajabu mtu kutokwa jasho jingi.

Uweza kuuliza,ni kwanini inatokea tu unapokuwa umekunywa maji? Jibu ni kwamba,ktk mazingira ya joto mwili unafanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa joto la ndani ya mwili linabaki ktk viwango vyake vya kawaida badala ya kupanda ili kuendana na hali ya hewa.Sasa njia pekee ya kufanya hivyo ni kutoka jasho jingi na kuamsha kiu ya kunywa maji - maji ya baridi.Kwa hiyo basi,unapokuwa umekunywa maji ya baridi,unakuwa umewezesha mwili kufanya kazi yake sawa sawa - kupoza kiu na kwa kufanya hivyo unakuwa ni kama umeusaidia kupamp jasho jingi zaidi.

Chukulia mfano unapokula chakula cha moto..tumbo linakuwa limebeba kitu chenye joto kubwa kuliko joto la mwili,sasa ili kuhakikisha joto la mwili halipandi ili kufuata lile la chakula cha tumboni,basi mtu ataanza kutoka jasho na kusikia kiu.Na ndio maana kiu kinapozwa kwa maji ya baridi.

Swali lingine linawezakuwa,ni kwanini miaka yote hiyo hali hiyo haikuwepo? Jibu ni kwamba binadamu sio jiwe! Kunakuwa na mabadiliko kila siku inayoitwa siku.Watafiti wanasema,kuna wakati vijitezi vya jasho vinakuwa vinafanya kazi zaidi ya kawaida(hyperactive). Haijafahamika ni kwa nini inatokea hivyo,ila habari njema ni kwamba,inatokea hivyo bila ugonjwa wowote mwilini. Na mara nyingi hii hali baada ya muda hupotea yenyewe na hapa pia haijulikani ni kwa nini inapotea tena!
 
nashukuru sana kwa ufafanuzi,maelezo yako nmeyaelewa na wasiwasi wangu umeisha,shukran sana
 
Itakuwa matundu yako ya kutolea jasho yatakuwa yametanuka sana...kitaalamu tunaita TUNDULIPHOBIA huu ugonjwa hua hauna tiba zaidi ya kutembea uchi na kutokunywa kwa muda wa mwezi mpaka hayo matundu yatarudi katika hali ya kawaida.............
 
Back
Top Bottom