Vangigula
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 808
- 2,538
Wasalamu.
Tuanze na assumption. Assume umeokota kiroba cha pesa chenye vibilioni kadhaa (1, 2, 3 ....), halafu ukaamua kutokuwa muungwana na kuziripoti police, tofauti kabisa na alichokifanya yule soldier wa Nigeria (kama sijakosea) wiki mbili tatu zilizopita.
(Nina imani wengi watakubaliana nami kwamba uungwana una mipaka yake). Swali la kwanza, ungezihifadhi wapi au kwa namna gani? Najua wengine wangesema wanahifadhi bank, wengine kuziweka kwa mzunguko wa biashara, wengine wangekula bata na kuzihifadhia tumboni, wengine wangechimbia chini.
Swali la pili, kama ki-account chako kilishazoea kuonja laki mbili tatu za salary, na baada ya siku tano kunakuwa empty, au hujawahi kabisa kumiliki account bank, zaidi ya accounts za Insta, Facebook na Mpesa, ambayo ina madeni ya TALA na Branch, je upepo ukikubadilikia fasta then ukatupia humo lets say millioni 500, he hutapewa kesi za utakatishaji pesa?
Swali langu la msingi ni kuwa kama nimepata pesa nyingi kwa mkupuo kwa njia zisizo rasmi, lakini halali, je sitapewa hizi case za kina Erickson? Sitosumbuliwa na wazee wa Financial Intelligence Unit nielezee nilikoipata kila shilingi? Ni kiasi gani cha fedha raia anaruhusiwa kuwa nacho bila ku-declare? Msaada wenu wakuu, maana hii ndoto ya kuokota 'fungu' naona inajirudia rudia.