habari wanajamvi, mimi nina simu ya kichina imeandikwa samsung,ni screen touch na unapoiwasha au kuizima inaleta animated word SMTEL. Hii simu nilifanikiwa kuiunganishia internet za zantel,vodacom na airtel kwa njia ya direct wap connections(ie wap phone model & send to 15300). Hivyo kwa kutumia built-in browser naweza kuingia kwenye web pages mbalimbali ikiwemo JF. msaada ninaouomba ni iwapo kuna mtu anafahamu link yoyote ambapo naweza kupata applications za simu particulary simu za kichina anisaidie ama maujanja yeyote juu ya simu za kichina. Naomba kuwasilisha