Salahan
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,942
- 3,606
Habari wakuu!Kuota ndoto ni jambo la kawaida kwa mwanadamu ila hii imezoeleka na kujulikana kwamba huwa tunaota kimyakimya.Ikitokea mtu kuota kwa sauti basi ni mara chache sana na huwa ni sentensi fupifupi sana.Ila hili la rafiki yangu limekuwa tofauti.Yeye huota kwa sauti mara zote na huongea sentensi hadi tatu.
Kuna muda huamka na kukaa kabisa na kuongea angali yupo usingizini.Kama hujamuangalia ukaishia kuisikia sauti unaweza kuhisi anaongea kabisa na wewe na unaweza kumjibu ukijua mko pamoja kumbe mwamba ANAOTA.
Yeye anaijua hali yake mana siku ya kwanza kuwa nae (mara nyingi mimi ni mtu wa kukesha au kuchelewa kulala) asubuhi aliniuliza "NILIOTA SANA EEE" Nakumbuka nilimjibu "amnaaaa hujaota".Nilimjibu hivyo nikiamini yale Maswali na maneno ya usiku ni katika maongezi ya kawaida kumbe mwamba aliongea ndotoni.Hii ni kutokana na ugeni ila kumbe anajijua hali yake hivyo alitaka uthibitisho.
livyotokea siku za mbeleni ndio nikajua mwamba ANAOTA KWA SAUTI.Utamsikia akisema "Broo leo unakomaeeee","Vipi unakaza mwenyewe","Ahaa naona mambo yanaenda".....Sasa sentensi kama hizi mwanzoni nilikuwa namjibu nikiamini ananiuliza juu shughuli zangu usiku huo yeye akiwa amelala kumbe mwamba yuko usingizini.
Saa nyingine huongea mambo ya familia,kazi yaani mara nyingi ni vitu vyenye maana na uhalisia.Yaani naweza kusema mwamba akichepuka anaweza kuongea yote ndotoni.Yeye binafsi haipendi hali yake iyo japo kaambiwa na mama yake itaisha yenyewe.
Anatafuta msaada kuacha kuota kwa namna hii (kwa sauti).Wadau wa tiba asili,kisunna, kisayansi mnakaribishwa tumsaidie kijana.