Jinsi ya kupangalia chumba cha kulala kiwe na mvuto zaidi

SAWEBOY

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
241
173
Wakuu wana JF,

Poleni kwa majuku ya kila siku.

Naombeni ushauri wenu, nimehamia hapa DSM na kuanza maisha, takribani week imepita. Nilijibanza kwa ndugu sasa nimepata vyumba 2 ambavyo ndo nategemea kuingia.

Pamoja na maandalizi mengine muhimu niliyoyafanya (vitu basic )bado kuna kitu kimoja kinanisumbua: Jinsi ambavyo chumba (sebule ) nitakavyo-ipamba ili mpenzi wangu akija kunitembelea anione nipo juu kiasi -ku-maintain status!

Naombeni ushauri wenu watu wataalam wa kupamba room au sitting room.

Vitu gani hasa ni muhimu vya kupendezesha?

Natanguliza shukrani wapendwa.
=========

Jinsi ya kuweka vizuri kitanda katika chumba cha kulala vidokezo muhimu kwa ajili ya kubuni mambo ya ndani
Unapaswa kujua jinsi ya kuweka kitanda ndani ya chumba cha kulala vizuri, kwa kuwa hii itaamua jinsi mpango utakavyogeuka na kama chumba kitakuwa na usawa.

Ni muhimu kuzingatia vipengele vya chumba na ushauri wa muhimu, ambao utakuwa rahisi kufanya uchaguzi sahihi. Pia unatakiwa kuwa na mweza ya pembeni ya kitanda.

Hizi ni dondoo chache za namna unavyoweza kupanga meza yako ya pembeni mwa kitanda, na kufanya chumba chako kivutie;

  • Tambua mtindo unaotaka kutumia kupamba meza yako ya pembeni; ukifahamu mtindo wako, itakusaidia kubuni ni muonekano wa namna gani unataka uwepo katika meza yako.
  • Ng’arisha kwa kuweka taa ya mezani; taa ya mezani ni moja yap ambo zuri la kuweka katika meza yako pembeni ya kitanda. Taa hiyo ina kazi nyingi mbali ya kupamba, lakini kama una tabia ya kuamka usiku, itakusaidia kukuangazia ili usije kujikwaa na kuanguka kwa kutoona.
  • Pamiliki kwa kuweka picha: uwekaji wa picha ni moja ya njia ya kupafanya paonekane ni sehemu yako binafsi. Unaweza kuweka picha zinazokukumbusha mambo mazuri ya familia. Unaweza pia kubadilisha na kuweka picha sanaa nzuri.
  • Weka trei ndogo: kwa ajili ya kuweka vitu vidogo vidogo pembeni ya kitanda chako. Trei ndogo ni timilifu kwa kutumia kupangia vitu kwenye meza ya pembeni mwa kitanda, ili kuepuka vitu kusambaa samba. Unaweza kuweka vitu vidogo vidogo kama herini, sarafu au vitu vingine vidogo.
  • Unaweza kuongeza nakshi kwa kuweka mmea pembeni ya kitanda kuongeza rangi; Kuweka mimea kwenye eneo lolote nyumbani huongeza uhai. Mimea kama ilivyo kwa taa ya mezani huongeza rangi na mvuto kwa muonekano mzima wa chumba. Kama wewe ni mtu usioweza kutunza mimea hai, basi weka mimea feki na hasa yakiwa ni maua.
  • Weka vipambo vidogo vizuri vya thamani; mapambo kama sanamu ndogo au saa vinaweza kufaa.
1593784958813.png

Michango ya wadau

Ku maintain status hakikisha upende kununua vitu quality, usijaze vitu vingi halafu vibovu... Basics za muhimu sebuleni kwa kijana wa kisasa ni Carpet, Sofa seats, TV & Deck, Pazia, Coffee table, Theatre system (si lazima but ni muhimu kwa entertainment) na Meza kwa ajili ya TV.

Hakikisha unaponunua/andaa vitu vi blend; blend in the sense kua unapokua/nunua vitu hivyo vya electronics hakikisha vinaendana rangi Vizuri, then unaangalia rangi ya ukuta wa hio sebule, unanunua pazia quality nzuri na rangi zilizopoa na za kiume kama coffee, beige, grey (kwa ufupi colours dark - usidhubutu sujui pink, yellow n.k). Mara nyingi coffe table nzuri za kisasa ni zile za kioo zenye stool zake, na hizi siku hizi zimeshuka sana bei sana i believe ukijipanga u can afford - miguu ya coffee table rangi ifanane na ya meza ya Tv.

Carpet nunua mwishoni, cause ni a guy mara nyingi nyie nafasi ya usafi ni finyu, nakushari dark colours; inaweza kua ya maua au michoro yenye rangi zote kama za pazia, sofa, meza n.k - ikiwa rangi moja walau iendane na pazia.. Carpet ikiwa dark colour itakusaidia coz ni nyumba ya vyumba viwili inamana lazima utapita sana hapo.

Kuepusha kuweka vitu kama glasses, sahani, jugs sehemu yoyote ya sebule ni vizuri ukachonga kimeza kidogo cha kuweka kona moja (hakikisha mgeni wako akiketi anakipa mgongo au ubavu) - hapo waweza funika na vitamba (zipo plastics but zinaonekana kama kitambaa) special kwa meza na water resistant. Hicho kitambaa cha plastic cha meza kiwe kinaendana walau na pazia. Hio meza waweza tumia kwa ajili ya kuweka all vyombo related things...

Good luk katika maandalizi... La ziada hizi mvua sisikudanganye fan muhimu.....
----
Chumba cha kulala ni mahali ambapo unapatumia wakati ukiwa umechoka na unahitaji utulivu na pumziko.

Ni mahali ambapo unahitaji kuondoa stress zote na kutuliza mwili na akili, vilevile ni mahali ambapo kwa wewe uliyeolewa unapata faragha ya kutosha kuwa na mume wako.

Kutokana na umuhimu wa chumba cha kulala basi ni vyema kikawa na mvuto utakaokufanya ujisikie vyema kuwa ndani yake namuonekano wake uchangie katika kukuondolea uchovu na stress.

Haipendezi kuona chumba kikiwa kimejaa makaratasi, magazeti na vitabu kila mahali bila mpangilio mzuri.

Weka vitabu na makaratasi yote mahali pamoja na kama unaweza kupata kabati na ukaviweka humo ili chumba kionekane nadhifu na sio kiwe kama maktaba.

Nguo ziwe zimepangwa vizuri kabatini au sandukuni na zile chafu zikae mahali pake kwenye kapu la nguo chafu. Usiache nguo zinaninginia kila mahali kwenye milango, madirisha, besele n.k maana inafanya chumba kiwe kimejaa na kuondoa mvuto.

Chumba cha kulala sio stoo hivyo haipendezi kuhifadhi vitu vya zamani chumbani kama viatu visivyovaliwa, nguo za watoto zisizovaliwa, miavuli, makoti ya mvua, toys za watoto n.k kama kuna ulazima wa kuhifadhi vitu hivi chumbani basi tafuta sanduku la bati na uviweke na kuhifadhi juu ya kabati au mvunguni ili kuondoa mlundikano wa vitu chumbani.

Kipambe chumba chako kwa maua na mapazia ya kuvutia. usipambe tu sebule na jikoni na kusahau chumba cha kulala.

Chumba kinaongezeka mvuto pale unapokipamba kwa maua na vessel nzuri, fremu za picha, mapazia mazuri na pia kapeti zuri la kuvutia. Unaweza weka picha yenu mkiwa honeymoon kwenye fremu na kuiweka mezani au ukutani na ikawa pambo zuri sana la chumbani kwenu.

Wekeza kenye mashuka mazuri na yenye kuvutia. Mashuka mazuri yanakufanya ujisikie vizuri unapokuwa chumbani na vilevile unapokuwa umelala.

Hakikisha unayafanyia usafi mara kwa mara na kuyabadilisha badilisha sio kila siku mashuka hayo hayo (kauka nikuvae). Wewe pia ni pambo mojawapo la chumba, hakikisha unakuwa na nguo nzuri za kulalia zenye kuvutia na kukufanya ujisikie vizuri na mwenye kuvutia.

Hasa kwa wale walioolewa ni vyema kuzingatia hili na kuepuka kuvaa ma-tsheti ya zamani na madela kila siku unapoenda kulala au unapokuwa umejipumzisha chumbani.
----
1. A COMFORTABLE RUG/ ZULIA
You need a rug /zulia inategemea unapenda la manyoya sana au la kawaida tu wengine wanapenda liwe chumba kizima wengine nusu tu ,either way ni wewe upendavyo tu. Zulia linaweza kuwa ndogo au kubwa wewe tu unavyopendezwa. Zile rugs zenye manyoya sanaa make sure unakuwa msafi usimwage mwage vitu vyenye maji maji maana yakiingiaga maji harufu yake utalichukia.

View attachment 576702

2. UWE NA MUONEKANO AU MANDHARI WA CHUMBA CHAKO
Wengi wanafikiri themes za bedroom ni kwa watoto peke ake la hasha hata kwa wakubwa pia,kuna wanaopenda romantic themes,all white etc.
Hapa naona huyu alipenda kuwe pa brownish flani hivi

3. MITO MINGI AU MICHACHE KADIRI UTAKAVYOPENDA
Hizi throw pillow ni a must have kwenye bedroom yako, kuna hapo za kurembea na za kulalia you need enough of them, ila kuna wengine wanapenda mingi inakuwa half of the bed ni mito tu,another day ntakuja waonyesha jinsi ya kuipanga.

4. SEHEMU YA KUKAA AU KUPUMZIKA AMBAYO SIO KITANDANI
Kitandani ni mahali pa kulala japo kuna wengine mwakaa ila tafuta kitu cha kukalia kama sofa kama hizo hapo juu au viti.

Wengine wanatumia ile space ya dirisha kujenga hapo droos kwa ajili ya kuhifadhia vitu na juu unaweka cushions na mito panatosha kukaa tena kuna view nzuri kama uko gorofani unaka hapo kusoma kitabu au kufikiria tu na kupanga mipango yako. viti pia vyapendeza

5. COLLECTION YA VITU UNAVYOVIPENDA
Ni vizuri kuwa na collection ya vitu vyako unavyopenda kuvitumia kama decor mfano vitabu mbalimbali
Kama na awards zako au decor zozote zile waweza tengenezea shelf kama hilo unaweka .

6. DROO AU VIKABATI VIDOGO VYA CHUMBANI
Umuhimu wa kuwa na a night stand mbali tu na kuwa ni decor pia waweza hifadhi vitu humo kama books,remotes ,taa ,weka hata maji ya kunywa kama huwa wanywa usiku.
Unaweza pia kwenye night stand ukaweka picha za familia yako au ya kwako ,flowers etc.

7. PICHA ILA SIO ZA WATU
Last week nliwaletea wall decor huko tulisema weka picha za familia ila huku chumbani weka tu za urembo au kitu kinacho ku Inspire zaidi. picha za flowers au wanyama pia

8. GODORO IMARA/QUALITY MATTRESS
Make sure una invest kwenye matress yenye quality nzuri.Utalala comfortable

9. ELEMENTS OF DRAMA
Chumba kidogo kiwe na drama mfano hizo bold colors kama hiyo red au hiyo picha nzurii ya lips
----

Muonekano wa mrundikano katika chumba kimoja

Hakuna ubaya wa kuishi kwenye chumba kimoja kama uko mwenyewe na ndio unaanza maisha ya kujitegemea. Cha muhimu ni kufahamu jinsi ya kupanga vitu vyako. Kuweza kuwa na mpangilio wa vitu mahali unapoishi au pengine popote mara nyingi inakuhitaji uwe na sehemu nyingi za kuhifadhia ambazo ni mashelfu, madroo na makabati.

Kitu kitakachofanya chumba kimoja kukosa mpangilio ni mrundikano. Mrundikano unafanya mahali paonekane pachafu, ondoa mrundikano kwenye chumba chako ambapo kitaonekana kuwa na nafasi na kisafi. Wewe mwenyewe utajisikia msafi na kujiona mwenye kupanga vitu vizuri. Sasa utaniuliza kuwa, chumba ni kidogo sasa nitapata wapi pa kuhifadhia pa ziada? Endelea kusoma utaelewa.

Nunua au tengeneza kitanda, meza na sofa vyenye maeneo ya kuhifadhia kwa chini. Vitu hivi vinawezesha kuweka mpangilio pale vinapokuwa na maeneo ya kuhifadhia, yaani kitanda au sofa ambalo mvunguni kuna droo za kuhifadhia. Vyote hivi ni jinsi ya kuongeza eneo la kuhifadhia kwenye chumba kimoja. Kimeza ambacho kina eneo la kuhifadhia kwa chini ni bora zaidi ya kile kitupu. Mantiki ni kuwa, nunua fenicha ambazo zitakidhi hitaji zaidi ya moja kwenye chumba chako.

Droo za kuhifadhia mvunguni mwa kitanda unaweza kuhifadhi vitu kama shuka, mito, taulo na blanketi za ziada. Droo za chini ya sofa, utafuta viatu vyako vizuri baada ya kutoka kazini na kuvihifadhi humo, na hata vile usivyovaa kila siku lakini bado unavihitaji.

Labda wewe ni mwanafunzi ama unafanya kazi na una mambo mengi yanayokuhitaji kujikumbusha, tundika umbao wa sponji kwa ajili ya kutobolea kwa pini vikaratasi vya ratiba, vipindi au mikutano yako ya wiki hiyo.

Hii itakusaidia kuondoa mrundikano wa karatasi kusambaa kila mahali kwenye meza hapo chumbani. Zile ratiba za wiki inayofuata zihifadhi kwenye droo hadi zitakapokaribia ndipo nazo unazitobolea kwenye ubao wako. Wakati huohuo ukifaili ama kutupa zile karatasi usizohitaji tena.

Kwenye chumba chako hicho kimoja weka kabati la nguo ambalo lina milango. Kwa ndani kwenye milango pigilia kulabu ambazo utatumia kutundika mikoba, mabegi na hata shanga na mikufu yako.

Ukubwa wa vitu unahusika kwenye chumba kimoja. Fenicha kwa mfano, sofa zitakavyokuwa kubwa ama viti vingi na nafasi nayo itaonekana finyu. Badala yake weka sofa la viti vitatu au viwili ambavyo kwakweli wewe na mgeni wako vinakutosha huhitaji zaidi. Pia michoro mikubwa eneo dogo inafanya sehemu ionekane ndogo.

Kwa mfano, kuwa na pazia na shuka zenye michoro mikubwa kwenye maisha ya chumba kimoja zitakifanya chumba chako kionekane kimerundikana. Aidha weka vitambaa vya rangi moja au vya maua madogodogo ambapo pia unatengeneza hisia za utulivu chumbani.

Ukiwa unaishi kwenye chumba kimoja uwe na vitu unavyohitaji kwa wakati husika tu. Huna haja ya kuwa na nguo, viatu na vyombo ambavyo huvitumii kwa wakati huo. Mrundikano wa vitu unavyotumia na usivyotumia utakuvuruga kiasi kwamba unashindwa kuona hata kile unachohitaji kutumia. Wengi wetu tunapenda kuhifadhi vitu tusivyotumia tena, labda ni kwa kuogopa kuwa huko mbeleni tutavihitaji tena au pengine ni hulka tuu. Ni busara kuondoa vizee ili kuacha nafasi kwa vipya. Kwaheri cha zamani na karibu kipya.

Kila utakaponunua kitu kipya na kuingiza kwenye chumba chako kiage kile cha zamnai. Kwa mfano kama umenunua ufagio mpya tupa ule wa zamani badala ya kuhifadhi yote miwili. Kama unadhani wa zamani haujaisha sana kwanini umenunua mpya sasa?

Kwa teknolojia inavyosonga mbele huja haja ya kuwa na picha nyingi za karatasi, badala yake unaweza kufremu chache na nyingine kuziacha kidigitali. Picha za kidigitali zinaweza kutizamwa zaidi kimtandao kwa kushirikisha ndugu, marafiki na wengine wengi ambao wasingeweza kuja kwako wazione kwenye albam ya picha za katatasi.

Kila wakati chumba chako kimoja kiwe kwenye mpoangilio. Kutumia dakika 15 asubuhi kuweka vitu vizuri na kutandika kitanda kitafanya maisha yako ya chumba kimoja yaonekane nadhifu kupita maelezo.
----
Nyumba ni urembo, nyumba ni mapambo, ili nyumba iweze kuvutia inahitaji mazingira yenye hadhi ambayo yanaweza kumvutia mtu kwa muonekano wake wa nje na ndani pia inaweza kumvutia mtu kutokana na rangi za chumba.

Watu wengi huweka mazingira safi jikoni, sebuleni na kusahau kuwa chumba cha kulala pia kinatakiwa kuwa safi muda wote kwani ni sehemu ambayo inatumiwa kwa mapumziko.

Ili kuweze kupumzika vizuri baada ya mizunguko ya kutwa nzima ni vizuri chumba kikawa katika muonekano mzuri ambapo sambamba na hilo uwepo mpangilio mzuri wa nguo na fenicha.

Chumba cha kulala hakitakiwi kuwa na vitu vingi, kinahitaki kuwa na hewa ya kutosha ili kumuwezesha mtumiaji kuweza kupata hewa safi pia inamsaidia mtumiaji kuweza kufanya usafi sehemu zote kutokana kuwepo kwa nafasi ya kutosha.

Epuka kujaza vitu vingi chumbani kama computer, meza viti, kapu la nguo chafu, kwani vitu hivyo vinaweza kuwekwa sehemu nyingine ya nyumba na chumba kubaki mahali pa kupumzika tu.

View attachment 632369 View attachment 632370
 
Ku maintain status hakikisha upende kununua vitu quality, usijaze vitu vingi halafu vibovu... Basics za muhimu sebuleni kwa kijana wa kisasa ni Carpet, Sofa seats, TV & Deck, Pazia, Coffee table, Theatre system (si lazima but ni muhimu kwa entertainment) na Meza kwa ajili ya TV.

Hakikisha unaponunua/andaa vitu vi blend; blend in the sense kua unapokua/nunua vitu hivyo vya electronics hakikisha vinaendana rangi Vizuri, then unaangalia rangi ya ukuta wa hio sebule, unanunua pazia quality nzuri na rangi zilizopoa na za kiume kama coffee, beige, grey (kwa ufupi colours dark - usidhubutu sujui pink, yellow n.k). Mara nyingi coffe table nzuri za kisasa ni zile za kioo zenye stool zake, na hizi siku hizi zimeshuka sana bei sana i believe ukijipanga u can afford - miguu ya coffee table rangi ifanane na ya meza ya Tv.

Carpet nunua mwishoni, cause ni a guy mara nyingi nyie nafasi ya usafi ni finyu, nakushari dark colours; inaweza kua ya maua au michoro yenye rangi zote kama za pazia, sofa, meza n.k - ikiwa rangi moja walau iendane na pazia.. Carpet ikiwa dark colour itakusaidia coz ni nyumba ya vyumba viwili inamana lazima utapita sana hapo.

Kuepusha kuweka vitu kama glasses, sahani, jugs sehemu yoyote ya sebule ni vizuri ukachonga kimeza kidogo cha kuweka kona moja (hakikisha mgeni wako akiketi anakipa mgongo au ubavu) - hapo waweza funika na vitamba (zipo plastics but zinaonekana kama kitambaa) special kwa meza na water resistant. Hicho kitambaa cha plastic cha meza kiwe kinaendana walau na pazia. Hio meza waweza tumia kwa ajili ya kuweka all vyombo related things...

Good luk katika maandalizi... La ziada hizi mvua sisikudanganye fan muhimu.....
 
Ku maintain status hakikisha upende kununua vitu quality, usijaze vitu vingi halafu vibovu... Basics za muhimu sebuleni kwa kijana wa kisasa ni Carpet, Sofa seats, TV & Deck, Pazia, Coffee table, Theatre system (si lazima but ni muhimu kwa entertainment) na Meza kwa ajili ya TV.

Hakikisha unaponunua/andaa vitu vi blend; blend in the sense kua unapokua/nunua vitu hivyo vya electronics hakikisha vinaendana rangi Vizuri, then unaangalia rangi ya ukuta wa hio sebule, unanunua pazia quality nzuri na rangi zilizopoa na za kiume kama coffee, beige, grey (kwa ufupi colours dark - usidhubutu sujui pink, yellow n.k). Mara nyingi coffe table nzuri za kisasa ni zile za kioo zenye stool zake, na hizi siku hizi zimeshuka sana bei sana i believe ukijipanga u can afford - miguu ya coffee table rangi ifanane na ya meza ya Tv.

Carpet nunua mwishoni, cause ni a guy mara nyingi nyie nafasi ya usafi ni finyu, nakushari dark colours; inaweza kua ya maua au michoro yenye rangi zote kama za pazia, sofa, meza n.k - ikiwa rangi moja walau iendane na pazia.. Carpet ikiwa dark colour itakusaidia coz ni nyumba ya vyumba viwili inamana lazima utapita sana hapo.

Kuepusha kuweka vitu kama glasses, sahani, jugs sehemu yoyote ya sebule ni vizuri ukachonga kimeza kidogo cha kuweka kona moja (hakikisha mgeni wako akiketi anakipa mgongo au ubavu) - hapo waweza funika na vitamba (zipo plastics but zinaonekana kama kitambaa) special kwa meza na water resistant. Hicho kitambaa cha plastic cha meza kiwe kinaendana walau na pazia. Hio meza waweza tumia kwa ajili ya kuweka all vyombo related things...

Good luk katika maandalizi... La ziada hizi mvua sisikudanganye fan muhimu.....

Dada Asha,

Nakushukuru sana kwa mchango wako, maana umenipa mambo matamu sana na naamini nitakapo yafanyia kazi basi dah room sebule yangu itapendeza sana.

Once again, nakushukuru sana kwa mchango wako juu ya hili jambo.
 
Subiri mahitaji..

Mkuu,

Ni mahitaji gani tena ? Si ndio nakusubiri wewe unihabarishe vema kuwa ninunue nini na madowido gani ili ni-ipendezeshe sebule , na hata chumba cha kulala !

Nakusubiri mpendwa kwa ajili ya ushauri wako ili mwenzio nisije chekwa akija kunitembelea nanihiiii!
 
Wakuu wana JF,

Poleni kwa majuku ya kila siku.

Naombeni ushauri wenu, nimehamia hapa DSM na kuanza maisha, takribani week imepita. Nilijibanza kwa ndugu sasa nimepata vyumba 2 ambavyo ndo nategemea kuingia.

Natanguliza shukrani wapendwa.

A yu sirias asee, kwanini usimsubiri huyo mpenzi wako mkapanga pamoja jinsi ya kupendezesha sebure yako?
 
Dada Asha,

Nakushukuru sana kwa mchango wako, maana umenipa mambo matamu sana na naamini nitakapo yafanyia kazi basi dah room sebule yangu itapendeza sana.

Once again, nakushukuru sana kwa mchango wako juu ya hili jambo.

Any time...
 
Wakuu wana JF,

Poleni kwa majuku ya kila siku.

Naombeni ushauri wenu, nimehamia hapa DSM na kuanza maisha, takribani week imepita. Nilijibanza kwa ndugu sasa nimepata vyumba 2 ambavyo ndo nategemea kuingia.

Pamoja na maandalizi mengine muhimu niliyoyafanya (vitu basic )bado kuna kitu kimoja kinanisumbua: Jinsi ambavyo chumba (sebule ) nitakavyo-ipamba ili mpenzi wangu akija kunitembelea anione nipo juu kiasi -ku-maintain status!

Naombeni ushauri wenu watu wataalam wa kupamba room au sitting room.

Vitu gani hasa ni muhimu vya kupendezesha?

Natanguliza shukrani wapendwa.

Nyie vijana wa siku hizi mna mambo kwelikweli. Utapamba nyumba weeeeeeee lakini mkifika kwenye 6x6 mnaanza kujitetea ooohhh ofisini ubusy ooohh najiskia malaria, ooh nimepata habari mbaya, ohh sijui nini vile!

Hayo unayotaka kufanya huenda rafiki yako yamemchosha machoni kwake. Kikubwa anachotaka kwako ni uanamume wako au usichana wako, full stop.

Mkitoka hapo ndipo mambo mengine yatafuata tena uzuri wake ni kwamba mkifanikisha yote hayo, hata ukipamba chumba chako hovyo, kitaonekana kizuri tu.
 
Wakuu wana JF,

Poleni kwa majuku ya kila siku.

Naombeni ushauri wenu, nimehamia hapa DSM na kuanza maisha, takribani week imepita. Nilijibanza kwa ndugu sasa nimepata vyumba 2 ambavyo ndo nategemea kuingia.

Pamoja na maandalizi mengine muhimu niliyoyafanya (vitu basic )bado kuna kitu kimoja kinanisumbua: Jinsi ambavyo chumba (sebule ) nitakavyo-ipamba ili mpenzi wangu akija kunitembelea anione nipo juu kiasi -ku-maintain status!

Naombeni ushauri wenu watu wataalam wa kupamba room au sitting room.

Vitu gani hasa ni muhimu vya kupendezesha?

Natanguliza shukrani wapendwa.

Kutoka kuwa jukwaa la watu makini na great thinkers hadi washauri wa wahamiaji na madalali !!!tunapotea taratibu!!
 
  • Thanks
Reactions: Iza
Huko chumbani usinunue kitanda kikuuubwa hadi mkose nafasi ya kupita. Nunua size ya kutosha ili chumba kiwe na hewa. Pia sio lazima ununue seti nzima ya makochi utajaza seble. Nunua kochi moja tu lenye 3 or 2 seats.
 
LENGO NI KUMFURAHISHA MCHUMBA WAKO! ILI NICHANGIE NAHITAJI DONDOO ZIFUATAZO tueleze ni wawapi (MJINI KIJIJINI, USWAHILINI, UZUNGUNI, MSOMI AU) ili uendane nae!
 
Uko tayari kulipia ushauri/kwaajili ya kazi hiyo?Na kama ni bure,basi ninaomba tukae chini na huyo mpenzi wako ili kujua nini angependelea paweje hapo maskani ili kuweza kumfurahisha.
 
Mkuu,

ni mahitaji gani tena ? Si ndio nakusubiri wewe unihabarishe vema kuwa ninunue nini na madowido gani ili ni-ipendezeshe sebule , na hata chumba cha kulala !

Nakusubiri mpendwa kwa ajili ya ushauri wako ili mwenzio nisije chekwa akija kunitembelea nanihiiii!

Wewe utakachokihitaji kwa wakati huo ndo utanunua ukitaka dressing table ukaona hakuna ndo ununue, ukitaka kioo hakuna ndo ukanunue, ukitaka kuangalia TV huna nenda dukani, ukiona unakanyaga chini kuna baridi nenda kanunue carpet, ukitaka kupika kuwasha mkaa au jiko la mchina unaona shida kanunue jiko la gesi upate urahisi na ukiaka chochote kwa wakati wowote ndo uende ukanunue kwa muda huo....sijui umenipata???
 
Nyie vijana wa siku hizi mna mambo kwelikweli. Utapamba nyumba weeeeeeee lakini mkifika kwenye 6x6 mnaanza kujitetea ooohhh ofisini ubusy ooohh najiskia malaria, ooh nimepata habari mbaya, ohh sijui nini vile!

Hayo unayotaka kufanya huenda rafiki yako yamemchosha machoni kwake. Kikubwa anachotaka kwako ni uanamume wako au usichana wako, full stop. Mkitoka hapo ndipo mambo mengine yatafuata tena uzuri wake ni kwamba mkifanikisha yote hayo, hata ukipamba chumba chako hovyo, kitaonekana kizuri tu.

Ha ha ha umenichekesha sana hapo kwenye bold
 
Back
Top Bottom