Msaada please ! Assistant Lecture/ Lecturer. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada please ! Assistant Lecture/ Lecturer.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Misosi, Oct 25, 2010.

 1. M

  Misosi Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Salaam! Naombeni msaada wa information kuhusu faida na hasara za kufanya kazi kama Assistant Lecturer au Lecturer pia ningeomba mwenye data anisaidie salary scale ya Assistant Lecturer(M.Sc holder) na Lecturer (PhD holder) na kama kuna malupulupu yoyote katika kazi hizi please. Kiufupi ninataraji kuhitimu masomo yangu kwa M.Sc na ningependa kufanya hii kazi lakini kama mjuavyo ni muhimu kufanya utafiti kwanza. Ahsante nategemea mawazo yenu wana JF.
   
 2. S

  Seekype Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Faida moja wapo unapata muda lukuki wakufanya mambo yako mengine...
  Ukiwa sharp unapata consultancies za kutosha na zinalipa
  Mshahara ni mdogo ukibahatika sana una 1M take home per month
   
 3. M

  Misosi Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Nashukuru kwa msaada wa information Mkuu.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kazi ya ualimu haina marupurupu mkuu.....na wala consultancies usifikiri ni rahisi kuzipata....lazima uwe na mtandao wa wenye nazo vinginevyo utaishi kwa mshahara tu.
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ukija kufundisha sahau neno malupulupu ikimaanisha marupurupu.
   
 6. Catagena

  Catagena Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimsingi, marupurup kama mwalimu wa chuo kikuu hakuna, na kwa junior staff kuishi kwa kutegemea mshahara is a common business. Cha msingi, kama unataka kujiunga na universities, njoo upate muda wa kuffanya mabo yako..lakini marupurupu sahau..ukitaka marupurupu nenda wizarani..huko ndiko ziliko pesa zisizo na wenyewe, na kuzila ni kiasi cha kuandika worklan tu, hata kama unachokwenda kufanya hakina tija inayolingana na pesa uliyochukua.
   
 7. M

  Matarese JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ah mwanangu mbona umempendelea! yaani akija na MSC yake ataanzia PUTS 13, wakilamba kodi almost 30% na PPF, atabakiwa na kama 800,000 tu. Kwa ufupi ndugu yangu ukiwa junior staff (TA, AL,L) andika maumivu tu!
   
 8. M

  Misosi Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Nashukuru sana Mkuu, ila hujanidokeza mshahara ni kiasi gani kwa mfano kwa Assistant Lecturer (basic / take home), vipi kuhusu house allowance hampewi? na je hamna safari zozote za hata kwenda kufundisha vyuo vingine? Kundi lipi hasa ndiyo junior staff? nashukuru Mkuu, natumai utanisaidia maswali hayo bila kunichoka.
   
 9. M

  Misosi Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Nashukuru Mkuu! kumbe hata L ni ktk kundi la junior stsff??!!! hivi huyu si ni PhD holder au??...
   
 10. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nadhani wengine hata hawafaham wanajibu nini. Mshahara kwa AL ni roughly 1.1 net. Hapo tayari kila kitu. Ukikaa kwa muda kwenye AL utafikisha 1.3 net. Kwa L ni 1.7 net. Kuhusu marupurupu huwa yapo, inategemea na ww tu ufanyaji wako kazi. Kuna kazi nyingi saana za ziada zinalipwa. Kwa University junior ni TA and AL.
   
 11. P

  Pax JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mshahara mpya Gross ni around 1.5m, take home kama 1.1. Marupurupu yapo kama unakuwa unasimamia fields au kazi nyingine zozote zinazohusiana na taasisi yako. Inategemea na MSc ya nini lakini unaweza pia kufanya kazi kwenye Insitution nyingine ukaongeza kipato chako. Ukiwa na projects ndio vizuri zaidi na pia ukiwa na consultancies.

  Kila mtu ana bahati zake so better try and see, kama huridhiki si unajiondokea bwana
   
 12. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nadhani mshahara wa assitant lecturer ni more than 1.4 m. wakikata mazagazaga yao mwisho wa mwezi unamkabidhi mkeo 1m azipangie matumizi.
   
 13. L

  Lady JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  "Bolded" Aisee kuna wanaume wangapi kama wewe!!
   
 14. M

  Matarese JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35

  Teh teh, Du hii kali!, unanikumbusha wimbo mmoja sikumbuki bendi gani walikuwa wanaimba " mshahara nikipata, bajeti apange yeye, anajenga nyumba kwao mimim kwangu........"
   
 15. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kubwa la kwanza: Malengo yako nini? Pesa au Career? or both?

  Ukiwa kwenye University cha kwanza ni kusoma, kufanya research. if you dont publish you perish.

  Ukiingia na MSc. ni kuanza kutafuta shule uanze PhD maana ukikaa sana kama AL wanakutimua kwa mujibu wa sheria zao.

  Advantages:
  1. Kusoma na research projects
  2. Consultancies depending on your field

  Hautapata pesa kwa faster kama mtaani but in a long runner kama aim yako ni PhD, prof.................... this is the right place. Pesa zitakuja as you climb the ladder.
  Karibu
   
Loading...