Msaada: Nyumba ya contemporary inavuja

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,386
9,658
Nilikuwa nazipenda sana nyumba za aina hii hadi nilipojionea kwa ndugu yangu.

Nyumba imeezekwa lakini inavunja sana Pembeni mwa mabati.

Afanyeje ili isivuje?

N.B: Pembeni ukuta umechimbwa ili kuingiza bati na kuzibwa kwa cement ya water proof.
 
Nilikuwa nazipenda sana nyumba za aina hii hadi nilipojionea kwa ndugu yangu.

Nyumba imeezekwa lakini inavunja sana Pembeni mwa mabati.

Afanyeje ili isivuje?

N.B: pembeni ukuta umechimbwa ili kuingiza bati na kuzibwa kwa cement ya water proof.
Mkuu contemporary kabla hujaijenga ilibidi uangalie site yako kama inareceive high rainfall maana itakusumbua sana hizi ni kwa ajili ya sehemu yenye mvua chache pia mafundi wanaoziwezea wako wachache sana inabidi hapo utafute fundi expert sio kila fundi anaweza kuzijenga
 
Nilikuwa nazipenda sana nyumba za aina hii hadi nilipojionea kwa ndugu yangu.

Nyumba imeezekwa lakini inavunja sana Pembeni mwa mabati.

Afanyeje ili isivuje?

N.B: pembeni ukuta umechimbwa ili kuingiza bati na kuzibwa kwa cement ya water proof.

Kuna sababu kwann injinia wa ujenzi anatumia miaka minne chuoni mpaka kuitwa injinia

Na kuna sababu kwann architect anatumia miaka mitano chuoni mpaka anapata degree...

Mkiambiwa mtumie wataalamu mnajidai wabishi.

Sasa gharama ya kuziba hiyo mivujo ndio gharama ungemlipa injinia kabla hujaanza ujenzi.
 
Kama jina lake lilivo na neno Temporary naamini ni swala la muda tu, Vilio vitaanza watu wamevamia sana huo ujenzi wa namna hio
Sio "temporary" ni "contemporary".

Mleta mada, aina hii ya roofing inafaa kwa sehemu zisizo na mvua nyingi. Roof yake inakua na slope ndogo, inayoweza kuvuja kama mvua zikiwa nyingi sana na hatua za water proofing hazikufanyika kwa usahihi.

Tafuta fundi mzoefu au mtaalam wa ujenzi. Atakagua hizo sehemu zinazovuja, then atakushauri nini kifanyike!
 
Ndo zipi hizo hebu tupiamo ka picha
unnamed.jpg
 
Sio "temporary" ni "contemporary".

Mleta mada, aina hii ya roofing inafaa kwa sehemu zisizo na mvua nyingi. Roof yake inakua na slope ndogo, inayoweza kuvuja kama mvua zikiwa nyingi sana na hatua za water proofing hazikufanyika kwa usahihi.

Tafuta fundi mzoefu au mtaalam wa ujenzi. Atakagua hizo sehemu zinazovuja, then atakushauri nini kifanyike!
Mkuu nisome vizuri nimesema kama Jina lake lilivo na neno Temporary meaning Temporary ni part pia ya jina ukiacha Conte
 
Back
Top Bottom