Mkuu unapatikana mkoa gani kwanza maana hao nyoka wanafaida sana kuliko hayo mayai ebu niambie unapatikana wapi nikupe dili la nyoka!Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.
Ninafuga kuku wa kienyeji hapa shambani kwangu. Kwa kweli kuku wanastawi vizuri na nilishaanza kufurahia matunda ya jasho langu, lakini ghafla nilianza kuona mayai yakipungua wakati kuku wanataga kila siku. Niliamini pasipo na shaka itakuwa nyoka. Hivi majuzi tukafanikiwa kumdaka nyoka mkubwa akiwa amemvamia kuku anayelalia. Kuku alianza kupiga kelele usiku ndipo tulipokurupuka na kwenda kuangalia, tukamkuta ameshameza mayai mawili tayari. Tulifanikiwa kumwua huyo nyoka.
Lakini hata baada ya kumwua huyo nyoka, bado mayai yameendelea kupungua. Pamoja na jitihada za kumwaga mafuta ya taa mlangoni na maeneo yanayozunguka nyumba lakini ufanisi ni mdogo. Hii mbinu ya kumvizia nayo ni ya kubahatisha. Je naweza kutumia mtego gani kuwamaliza nyoka shambani mwangu? Au nitumie dawa gani?
unapaka kwenye mayai na kuku wote unawapakaUnatumiaje hyo oil chafu? Unapaka kwenye mayai ama...?
Nyoka hawali chakula kila siku.. Akila akishiba anawez Kukaa wiki mbili adi miiezi miwili kulingana na nyoka..
Sasa inabidi uchunguze kuna kiasi gani cha nyoka waliopo shambani kwako
Hilo litakuwa joka la kibisaHuyo ni nyoka MTU
Hapo naona sio nyoka bali kuna mtu anaiba hayo mayai
Nilikuwa na kuku wengi sana na kulikuwa na joka kubwa sana ambalo ni la miaka lakini hata siku moja hajala mayai
Na ni msaidizi mzuri sana kwa vibaka kwani wanajua uwepo wake hapo na hawasogei
Asubuhi huwa anaota jua kwenye barabara ya kuingilia shambani
We achana na nyoka mwizi yupo hapo mvizie tu
Sent from my iPhone using Tapatalk
Ni ngumu kugundua kiukweli..ila ni mara chache sana eneo la nyumbani kuwa na nyoka wengi.. Kwa kawaida anaweza akawa mmoja au wawili tu(dume na jike) ata wakizaa au kutotoa vile vitoto vinaenda kutafuta maisha mbali na hapo
Mjomba huyo ni nyoka mtu anayeishi hapo shamba....otherwise atakuwa ni kenge siyo nyoka huyoKama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.
Ninafuga kuku wa kienyeji hapa shambani kwangu. Kwa kweli kuku wanastawi vizuri na nilishaanza kufurahia matunda ya jasho langu, lakini ghafla nilianza kuona mayai yakipungua wakati kuku wanataga kila siku. Niliamini pasipo na shaka itakuwa nyoka. Hivi majuzi tukafanikiwa kumdaka nyoka mkubwa akiwa amemvamia kuku anayelalia. Kuku alianza kupiga kelele usiku ndipo tulipokurupuka na kwenda kuangalia, tukamkuta ameshameza mayai mawili tayari. Tulifanikiwa kumwua huyo nyoka.
Lakini hata baada ya kumwua huyo nyoka, bado mayai yameendelea kupungua. Pamoja na jitihada za kumwaga mafuta ya taa mlangoni na maeneo yanayozunguka nyumba lakini ufanisi ni mdogo. Hii mbinu ya kumvizia nayo ni ya kubahatisha. Je naweza kutumia mtego gani kuwamaliza nyoka shambani mwangu? Au nitumie dawa gani?
Hivi nawaza nikichukua yai nikatoboa kidogo nikaingiza sumu ya panya. Huyo nyoka atakula? Hebu jaribu hii. Toboa kwa ustadhi ingiza sumu ndani ya yake. Pia wanasema ukilichemsha yai halafu umamtegea. Kwa kuwa analimeza halitakaa lipasuke au kuyeyuka na atakufa.
Mkuu kama ukitoboa ni lazima kuku uwafungie kwanza eneo lingine mpaka yai limezwe. Ila pia ukilichemsha ndiyo imara kabisa maana haliyeyuki. Ni lazima afe tu.Yai ukilitoboa tu linaliwa na kuku.. sasa ukiweka sumu kwenye yai basi umetega kuku wako mwenyewe