Msaada: Nitumie mbinu ipi ili watoto wapende kujisomea?

Dada yangu alibuni mbinu za kununua A, yaani mtoto anaepata A analipwa kiasi alichokubaliana na wazazi.
Ananiambia kuna mmoja alikuja na A 6. Fikiria kama mlikubaliana A moja ni laki moja!

Lakini alifanikiwa.
hata baba yangu alitumia hii njiaa! leo hii ninakula matundaa hayoo
 
Habari zenu,

Niende moja kwa moja kwenye mada. Kuna watoto hapa maskani. Hawataki hata kusoma wala kujisomea, yani wakitoka shule Tv na wao, wao na TV.

Yaani ukiwaambia wakasome hawataki yan mpaka waamie wenyewe. Ukiwaambia walajisomee wanaona kama unawatibulia ratiba yao.
Hata mtihan ukikaribia hawasomi na mitihan hawakuonyeshi.

Mmoja yupo form 2 mwingine darasa la 5 mwungine 7 meingine 3. Nifanyaje maana muda mwingine nachoka mpaka najisemea kimoyomoyo wasome au wasisome watajua wenyewe.

Kumbuka hawa ni watoto wa ndugu zangu wameletwa hapa niwasimamie wasome lakini wao wanaleta ujinga

NB: Nimehitimu chuo mwaka huu UDOM
Wewe mwenyewe hujisomei unategemea mtoto ajisomee nn?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom