Msaada: Nini nifanye ili niweze kutatua tatizo la gari yangu aina ya Toyota Corolla Fielder

Farajamassawa

New Member
Apr 27, 2021
2
45
Habarini wapendwa kwema!!! Nina gari yangu aina ya Toyota corolla fielder shida kubwa kila nikiiwasha inawaka halafu inazimika nikirudia tena bado inazimika, ila ukiiwasha halafu ukaikanyangia moto hata kwa dk 3 mpk 5 ikishapata moto engine ndo inawaka.

Nimeshaipeleka kwa fundi lkn bado shida inajirudia

Naombeni mnisaidie sijui shida ni nini.
 
JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
1,057
2,000

Corolla Fielder ya mwaka gani? Throttle yake ni ya umeme au cable?
 
Pellman

Senior Member
Feb 13, 2017
125
250
Huenda sailensa iko chini.
Waliounda gari wasingeweka option ya "sailensa" ya chini kihivyo kama ikiwa chini kihivyo gari haifanyi kazi.

Kuna tatizo ambalo mafundi wetu wa Kiswahili wanalitatua kwa kupandisha juu "sailensa" wakidhani wamepata ufumbuzi.

Sawa na kuweka band-aid kwenye jeraha la risasi.

Na kwenye gari hakuna kitu kinaitwa "sailensa." Labda "idle." Kwa Kiswahili "muungurumo" au "mlio." Sema mlio wa gari uko chini.
 
JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
1,057
2,000
Waliounda gari wasinge set kuwe na option ya "sailensa" ya chini kihivyo kama ikiwa chini kihivyo gari haifanyi kazi.

Kuna tatizo ambalo mafundi wetu wa Kiswahili wanalitatua kwa kupandisha juu "sailensa" wakidhani wamepata ufumbuzi.

Sawa na kuweka band-aid kwenye jeraha la risasi.

Na pia sio sahihi kusema "sailensa." Usahihi ni "idle." Kwa Kiswahili "mlio" wa gari.
1. Mafundi wengi ukisema Idle speed hakuelewi.

2. Gari thrrole ya umeme siyo kila mtu anaweza kujipandishia tu idle speed. Ndio jibu langu lingine nikaandika hivi "huenda inahitaji kufanyiwa thrrottle learning ambayo inafanywa kwa mashine". Hii throttle learning inasaidia kuirudisha idle speed mahali inapitakiwa kuwa.

3. Throttle ya umeme hainaga Idle Air Control Valve. Hivyo kuharibika kwa sensor zingine kama ECT sensor au IAT sensor kunaweza pelekea tatizo kama hiyo aliloleta mtoa maada.
 
JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
1,057
2,000
Fundi niliempelekea amejaribu kupandisha sailensa lkn bado shida iko palepale

Inawezekana kati ya hizi sensor mbili kuna moja ina shida.

1. ECT sensor ambayo hupima joto la coolant.

2. IAT sensor ambayo hupima joto la hewa.

Kama hivyo viwili ni vizima basi gari yako inaweza kuwa na misi ambayo bado haijaset code bado.

Na diagnosis ya misi ambazo hazijaset code ni mpaka kuanalyse fuel trim ndo jibu linaweza patikana.
 
nawala

Member
Mar 21, 2020
40
125
Hiyo gar ina tatizo kama langu , juzi niliifanyia overhaul ndio sasa iko njema
Lakin kuna vitu hivi hapa

Hiyo 1. Angalia plugs km nzima
2. Angalia multi air flow sensor isafishe
3,angalia throstle body isafishe pale kuna sensor ambayo inafungua silensor na kuifunga ina ka head kwa mbele inatakiw kuzunguka kwhy safisha hiyo
4.angalia nozzle kama nzima
5,angalia usichanganye nyaya zinazoingia kwenye nozzle
6.angalia high voltage tube lead au wanaita coil ambazo zinapokea moto wa plugs km mbovu hiyo ndio mtindo wake,
7..angalia fuel pump kwenye tank km inauchafu kuna chujio mbili ndan ambayo haifunguki na kile cha nje safisha zote kwa air pressure
8,.check air filter iwe safi
9, badili gasket head ikiwa plugs zinaloa oil au coolant

10, kwa miaka 100 badili tu rings piston ,valve seal ,oil seals baada ya kuona moshi unatok nyuma mweupe au mweus ukiwa kweny motion.

Mungu akubariki
 
Yaani tatizo kama hilo ndio ufanye overhaul ya engine? Uliamua tu kuingia gharama ambazo hazikuwa na ulazima.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
32,022

Kaka samahani kidogo,najua engine huwa inapitia sehemu nne ili kukamilisha mzunguko mmoja ambapo sehemu hizo ni intake,compression,combustion pamoja na exhaust.

Sasa kuna kitu kimoja ambacho kinanitatiza akili yangu.Kwenye hiyo hatua ya kwanza ya intake piston huwa inashuka chini na valve zinafunguka ili oxygen inyonywe kwa ajili ya hatua ya pili ambayo ni compression.Kinachonitatiza ni kwamba ili kazi fulani ifanyike huwa kunahitajika nguvu/energy/power,sasa nguvu ambayo huwa inatumika kushusha hiyo piston chini ili hewa iweze kuingia kwenye chamber huwa inatoka wapi?Kumbuka kwenye hatua ya intake hata combustion bado kwa hiyo hakuna pressure inayoisukuma piston chini,sasa ni kitu gani huwa kinaisukuma piston kwenda chini ili valve zifunguke hewa iingie?
 
Mkuu kwanza sijui tutumie case study ya engine yenye cylinder ngapi?

Okay let say mfano cylinder 4 ambapo utakuwa na piston nne.

Ukiifungua cylinder head ya engine yenye piston 4, utaona piston mbili zinapokuwa juu basi kuna piston mbili zinakuwa chini.

Maana yake zile mbili za chini moja inakuwa kwenye power stroke moja inakuwa kwenye induction stroke. Na zile mbili za juu moja inakuwa kwenye exhaust stroke na nyingine inakuwa kwenye compression stroke.

Unachotakiwa kujua ni kwamba matundu yote manne hayachomi mafuta kwa mara moja. Kwenye kila mzunguko mmoja kuna tundu moja linachoma mafuta. Hivyo kwenye kila. mmoja kuna nguvu inayozalishwa.

Kinachosukuma piston zije chini ni mlipuko mkubwa sana unaotokea kwenye combustion chamber mara tu baada ya piston kumaliza kucompress mafuta na hewa/hewa.

Pia gari za diesel engine yake inakuwa na flywheel kubwa nyuma ya engine. Kazi yake ni kwa ajili ya kustore energy yaani ni lichuma fulani kubwa ambalo ukilizungusha speed kubwa halafu ukazima gari engine inaweza endelea kuzunguka kwa mizunguko kadhaa kwa sababu ya enery iliyokuwa stored pale.

Kuna zile mashine za diesel wanazitumia sana kupasua mbao maporini. Ile mashine upande mmoja ina chumba kubwa sana. Linaonekana kama mzigo lakini linaconserve sana energy.
 
Mkuu nimekuelewa fasta sana kwamba piston moja ikiwa chini nyingine inakuwa ipo juu tayari kwenye combustion stage ambapo ikisukumwa kurudi chini wakati wa combustion basi inanyanyua ile iliyopo chini kurudi juu kwa ajili ya kufanya combustion ili kunyanyua tena iliyopo chini na mzunguko unakuwa unaendelea.Sasa mkuu nilipokwama ni vipi engine ya piston/cylinder moja huwa inajiendesha?
 
Simply movingi parts za engine ni nzito hivyo muda ambao engine haizalishi nguvu nguvu ya kupush hivyo vitu inatokana na uzito wa hizo moving parts. Pia time kati ya power stroke moja na nyingine ni ndogo sana.

Mfano gari inapokuwa sailensa kila nozzle inatema mafuta kila baada ya 2 millisecond ambayo ni time ndogo sana.
 
Mkuu muda ambao engine haizalishi nguvu ndiyo muda ambao piston inatakiwa itumie nguvu nyingi sana kwenda juu kufanya kazi ya ku-compress mafuta pamoja na hewa(compression stage) kama maandalizi ya combustion.Sasa hizi free moving part za engine ambazo ni nzito huwa zinaweza kuzalisha nguvu ya kutosha ya kuweza kufanya hii kazi ngumu /kubwa ya compression?Kwa sababu hii kazi ya compression huwa inazalisha resistance kubwa sana inayopingana na kazi ya compression ambayo piston inafanya!
 
Hizo moving parts siyo kama zinazalisha nguvu. Ila kwa sababu zinazunguka tayari zinakuwa na energy ambayo ndio hutumika muda ambao nguvu haizalishwi.

Halafu usichukulie kwamba engine inakaa muda mrefu bila kuzalisha nguvu. Mfano engine ikiwa katika idle speed ya 650rpm maana yake kwa sekunde moja inafanya mizunguko 9.

Kwa Lugha rahisi engine ya piston nne, ndani ya sekunde moja mafuta yanachomwa mara 65.
 
Semahengere

JF-Expert Member
Nov 29, 2020
234
500
Habarini wapendwa kwema!!! Nina gari yangu aina ya Toyota corolla fielder shida kubwa kila nikiiwasha inawaka halafu inazimika nikirudia tena bado inazimika, ila ukiiwasha halafu ukaikanyangia moto hata kwa dk 3 mpk 5 ikishapata moto engine ndo inawaka.

Nimeshaipeleka kwa fundi lkn bado shida inajirudia

Naombeni mnisaidie sijui shida ni nini.
Poor pressure ya fuel pump
Badilisha hiyo tatizo litaisha
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom