Utakatishaji fedha(Money laundering): Dhana iliyojificha kwa wengi!

Ni kitendo cha kuweka pesa "chafu", yaani zilizopatikana kiharamu katika mfumo halali ili kuficha chnazo chake haramu. Kwa mfano mtu anapata pesa kwa kuuza dawa za kulevya, kisha ananunua magari anakuja kuyauza. Hivyo ukimuuliza pesa anatoa wapi, atakwambia, nafanya biashara ya magari, lkn ukweli ni muuza unga.
 
Tafadhali husitumie tafsiri bali kukingana na namna Tanzania au sheria za Tz zilivyo,

Karibu

updates:
B. UTAKATISHAJI WA PESA
Nini maana ya UTAKATISHAJI WA PESA?
Hiki ni kitendo cha kuzichukua pesa chafu au pesa yoyete iliyotokana na uhalifu na kuifua ili ionekane safi kisha unaiingiza kwenye mzunguko wa uchumi. Mfano mzuri tu Waziri fulani anaenda kusaini mkataba na wawekezaji fulani kwenye HOTELI X.

Pindi anafanya hivyo anapewa bahasha ina cheki nono ya Bilioni kumi labda. Hali akijua kabisa kupokea ile cheki ni kitendo cha Rushwa na anweza kukamatwa baadae, waziri anaamua kuichukua ile pesa na kuipeleka kwenye mabenki ya nje au kuigawanya-gawanya kisha mtu anawekeza kwenye makampuni makubwa. (Shell Companies). Au kwa namna nyingine mtu anaweza tu akaweka kwenye akaunti ya mtu mwingine nje ya nchi na kisha pesa zinaweza kuja kama misaada.

Lakini mpaka sasa wenye uwezo wa kuficha pesa nje ya nchi ni wale tunaowaita BIG-FISH. Kwa hapa Tanzania wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa ndiyo wenye uwezo wa kusafirisha pesa kwenye mabenki ya nje (Transnational-Money Transfer).
Mheshimiwa raisi kwa hao unaofikiri pesa zimefichwa hapa nchini ni wachache sana;

Pesa chafu ipo kwenye mzunguko na inatumika kuwanunua wanasiasa na vyombo vya habari. Huu ndiyo ukweli mchungu; naamini njia yako ni njema sana kabisa lakini ingeweza kufanya kazi sana katika mazingira ya 90's na 80's.

Kwa sasa waharifu wengi wanapata pesa chafu kutokana na Rushwa, madawa ya kulevya, ujangiri, wizi , ulanguzi, kukwepa kodi na mengineyo mengi na pesa zao wanaziweka kwenye mzunguko na wala hawzifichi tena. Kadiri teknolojia na utawandawazi unakuwa na hivyo ndivyo uharifu nao unazidi kuwa wa juu (sophisticated).

Pesa hazifichwi NDANI tena, ZINAFICHWA KWENYE MZUNGUKO. Hizo pesa ndiyo zimenunua majumba na zinaendelea kujenga mengi huko MASAKI, MBEZI BEACH, UNUNIO, MSASANI, NJIRO,SAKINA etc.
Wataalamu kwa lugha ya kiingereza wanasema "INJECTING DIRTY MONEY INTO THE LEGAL ECONOMY".

Mwaka jana nilienda PCCB nikapata wasaha wa kufanya majadiliano na baadhi ya maofisa wakubwa pale. Wakanipa mifano mizuri tu kama THE TEGETA ESCROW SCANDAL na jinsi UTAKATISHAJI WA PESAULIVYOFANYIKA. Wale wahanga wa ile skandali kama Tundu Lissu alivyosema, kweli walibeba pesa kwenye Lumbesa, magunia na sanda lakini hawakuzificha ndani, walizificha kwenye mzunguko.

Nyingi zilitumika kukupigia wewe kampeni na nyingine zikanunua Dollar, Pound na Euro na kupelekwa nje ya nchi. Na hii ni moja ya sababu kubwa kabisa Shillingi kuanguka hapa nchini. Mheshimiwa raisi ni lazima ushauriwe vizuri kabisa kwamba tatizo siyo kuficha pesa ndani, tatizo ni kutakatisha pesa na kuziingiza tena kwenye mzunguko.

IGP Mstaafu ndugu Saidi Mwema kwenye Makala yake iitwayo "CURRENT SITUATION AND COUNTERMEASURES AGAINST MONEY LAUNDERING: TANZANIA’S EXPERIENCE". Amekiri kabisa kwamba Utakatishaji wa pesa ni moja ya kosa ambalo linaumiza uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa na mpaka sasa hakuna sheria sahihi ambazo zinaweza kulishinda tatizo.

Ni kosa linalofanywa na wataalamu waliojipanga wakipata msaada kutoka kwa Wansheria na Wanauchumi wazuri kwa nchi. Mwaka juzi tena Dr Edward Hossea alisema zaidi ya asilimia 30 ya pato la taifa inapotea kwenye rushwa na utakatishaji wa pesa. Lakini mheshimiwa hili mbona hujalitaja? Huu ndiyo ufichwaji wa pesa haswaaa hawa wanaoficha ndani ni vidagaa vidogo sana ndani ya bahari kubwa.
C. MTAZAMO WA KISHERIA.
Nisema kabisa hata wataalamu wa sheria wanakiri kuna tatizo kubwa kwenye sheria za nchi ambazo wajanja wamezitengeneza na kuacha nafasi (gaps; lacunae) ili waendelee kupiga pesa. Naamini kabisa kwa msaada wa BOT unaweza kubadilisha noti ya elfu kumi kwasababu hilo lipo ndani ya uwezo wako lakini nakuahidi hata hizo noti mpya zitafichwa tena (HUU NDIYO UKWELI MCHUNGU).

Ukisoma Sheria ya utakatishaji wa PESA au ANTI-MONEY LAUNDERING ACT of 2006 na marekebisho yake ya mwaka 2012 yameorodhesha makosa mengi sana yanosababisha Utakatishaji wa Pesa. Lakini mpaka leo hii pesa inazidi kutakatishwa na kuingizwa kwenye mzunguko.

Kwa kifupi sheria za nchi ni mbovu na haziwapi mawakili wetu uwanja mpana wa kuweza kuwashughulikia ipasavyo watakatisha pesa. Hivyo hata wewe ukichapisha pesa upya bado sheria haikupi nguvu ya kufanya hivyo. Nitakupa mfano mzuri kabisa katika hili. Mwaka 1983 na 1983 Marehemu Sokoine alianza mchakato wa kuwasaka wahujumu uchumi. Naye alikuwa ana nia njema kama wewe lakini kwa bahati mbaya safari yake iliishia hapo Morogoro.

Vijana wa UVCC ndiyo walileta hamasa kubwa kwa Sokoine. Aliwashughulikia sana wahujumu uchumi, watu wengi walifungwa sana lakini mwisho wa siku ikaja gundulika kwamba wanaoguswa ni Vidagaa na wale BIG-FISH waliendelea kupeta tu mtaaani. Alipojaribu kuwagusa hata sheria za CHAMA na NCHIziliwalinda. Inasemekana aliwataka hadi kuwafuata mawaziri wakuu wastaafu, wakubwa wengine pamoja na viongozi wa dini:Lakini ilishindikana, na kwanini kwasababu moja yeye hakuwa Raisi na mbili sheria ile ilikaa vibaya.

THE ECONOMIC SABOTEURS ACT ya 1984 ilitengeneza mahakama ya Mafisadi ya kwanza kabisa hapa nchini. Ilikaliwa na watu watatu wawili ambao ilikuwa siyo lazima wawe wanasheria. Mtu ulikuwa ukikamatwa moja kwa moja na pesa za taifa unapelekwa kwenye hiyo mahakama na unanyimwa haki ya kujitetea na wala huwi na wakili wako.

Wewe ni ndani tu: Kama ilivyo ada, BIG FISH waksema ule ni uvunjaji wa haki za binadamu hasahasa THE PRESUMPTION OF INNOCENCE and RIGHT TO LEGAL REPRESENTAION. Kweli njia za Sokoine zilivunja sana haki za binadamu lakini wengi walimpiga vitab siyo kwasababu wanajali haki za binadamu bali matumbo yao.

Ile sheria ilirekebishwa na kesi zikarudishwa Mahakama kuu na serikali ikaendlea kucheza Twisti pamoja na mafisadi. Kwa hivyo mheshimiwa raisi kjama anataka kufanya kitu kinachoeleweka ni lazima atambue kwanza tatizo ni Utakatishaji wa Pesa. (Money Laundering) kwasababu pesa ziko ndani ya mzunguko na kama kuficha wanazificha nje. Mimi naomba raisi asije akashindwa katika hili, alenge shabaha upande adui alipo.
D. NINI KIFANYIKE?
Mheshimiwa raisi ni lazima ajue kabisa kifungu kimoja cha sheria kinaweza kujenga au kubomoa nchi yetu. hadi mwaka 2000 nchi ya India ilikuwa inateswa sana na TATIZO la UTAKATISHAJI wa pesa. Walijaribu mbinu zote kama wewe lakini ikashindikana. Makanjanja walishajua kuficha hela USWIS huko. Kesi zilipopelekwa mahakamani mawakili walishindwa kuthibitisha wizi wowote ule kwasababu ushahidi walikuwa hawana. Pesa na mali zina majina mengine na huwezi kunyang'anya kwasababu ni kinyume cha sheria.

Kwenye SHERIA ZA USHAHIDI au THE LAW OF EVIDENCE, siku zote serikali ikipeleka kesi mahakamani ni lazima wao ndiyo wathibitishe kwamba mtu ni mwenye kosa. Mfano kama Mtu kaua inabidi waendesha mashitaka wathibitishe (Proof Beyond Reasonable Doubt) kwamba kweli mtu kaua hata kama alikamatwa na kisu muda huo. Ushahidi usipotosha mtu anaachiwa nje vizuri tu na hamuwezi kumgusa. Na hizi ndiyo sheria zetu hapa na duniani kote.

Kutokana na Ugumu wa kushughulikia kesi za utakatishaji wa pesa India mwaka 2000 ilipitisha sheria inayoutwa THE PREVENTION OF MONEY LAUNDERING ACT. Sheria hiyo ilikuwa ina mambo makuu mawili.
  1. Ilitengeneza mahakama maalumu ya kushughulikia utakatishaji wa pesa na rushwa.
  2. Ilibadilisha tamaduni ambayo Waingereza waliileta inayosema mwendesha mashitaka inabidi uthibithishe utakatishaji huo kwa kutoa ushahidi.
Kwenye hili la pili mtu ukikutwa na mali na ukwasi ambao hauelezeki basi mali zote na akaunti za bank zinafungwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa serikali. Mtuhumiwa atatakiwa yeye binafsi aeleze njia zipi alizotumia kupata utajiri huo. Kama mali ni zake basi ni lazima ataweza kuthibitisha na kama akishindwa serikali inanyang'anya hizo mali kwasababu zinakuwa hazina mtu.

Sheria hii ilipigwa sana vita lakini imesaidia India kwa kiasi kikubwa na hata Waingereza na nchi nyingine wemeiga. Mwanzoni walisema inavunja haki za binadamu lakini mwishowe ukweli ukabaki kwamba: Kama Pesa ni zako basi thibitisha. Mpaka sasa India imeshughulikia kesi za iutkatishaji wa pesa zaidi ya 1500 na kwa kiasi kikubwa zimezaa matunda chanya.

Tanzania yetu sheria ni mbovu na hata mawakili wetu hawajfundishwa vizuri kuhusiana na hili. Financial Intelligence Unit (F.I.U) bado wanahangaika na makesi mengi makubwa ambayo yanakaa mahakamani kwa zaidi ya miaka miwili. Na ukiangalia wezi bado wanapeta na mali zao na wananendelea kuwahonga majaji na mawakili.

Mwaka 2011 kama kumbukumbu zangu zimekaaa vizuri wakati DPP ni DR MBUKI FELESHI mwanasheria mkuu kutoka Bermuda alikuja kuwafundisha waendesha mashitaka wetu kuhusiana na hizo njia. Lakini cha kushangaza mpaka sasa serikali imekaa kimya kana kwamba mambo ni mazuri kumbe kuna uozo mwingi.
Yafuatayo ni mambo ya kufanya ili nchi ikabili makanjanja wanaoficha hela ndani ya mzunguko na nje ya nchi:
Badilisha sheria ANTI-MONEY LAUNDERING ACT of 2006 na iwe kama India na Uingereza. Mtuhumiwa atuthibitishie jinsi alivyopata pesa zake. Hata kama kuna majumba na magari huko MASAKI, NJIRO auSAKINA akishindwa kueleza jinsi gani ameyapata tunanyang'anya.

Pili,kuna sheria inaitwa MUTUAL ASSISTANCE ACT, inahisiana na nchi mbalimbali kushirikiana kupambana na masuala ya utakatishaji wa pesa na uhalifu mwingine. Nadhani ukienda Uingereza naUSWISI utasaidiwa kwasababu wao nao wamesaini THE UNITED NATIONS CONVENTION ON THE PREVENTION OF CORRUPTION of 2000.

Tanzania tuliipitisha tarehe 25 May 2005, Uingereza tarehe 9 February 2006 na USWISI tarehe 24 September 2009. Kisheria kama umesaini huu mkataba ni lazima nchi washirika msaidiane, mheshimiwa raisi unasubiri nini kuwafuata BIG FISH?

Tatu, PCCB na FIU wamenyimwa meno. Haiwezekani taasisi huru kama hizi wawe wahusika wakuu lakini ruhusa za kushughulikia kesi wanaenda kuomba kwa DPP. Hii haijakaa sawa hata kidogo. Tunajua DPP ni wa serikalini na kama makanjanja wakitaka kumtumia anaweza kuchelewesha au asiruhusu kesi ifike mahakamani.

Hivyo basi sheria kama THE CRIMINAL PROCEDURE ACT irekebishwe ili PCCB na Financial Intelligence Unit wawashugulikie makanjanja huko huko bila kwenda kwa DPP. Na angalizo, hizi idara inabidi ziwajibike kwa bunge na waziri husika ili kama kuna uhuni unafanyika UMMAH wa Watanzania tujue kabisa. Hapa utazuia mtafuruku uliowahi kutokea huko nyumba baina ya Dr Hossea na Feleshi ambao walitunishiana misuli huku pesa zetu zikiendelea kupigwa bila huruma.

Nne, tunaomba tume ya maadili iwe inachapisha mali za mawaziri wako kila baada ya miezi sita. Ili tujue maendeleo na mgongano wa kimaslahi ili siku waziri akikutwa na ukwasi asiseme ni vijisenti tu . Hilo sisi hatulikubali kabisa maana viongozi wa nchi hii wakistaafu wanasema mafao yao ndiyo yananua hadi maghorofa na migodi.

Hili linaleta ukakasi kabisa kwasababu hatujui kiasi cha mafao hayo yenye kuweza kununua mgodi au kununua mansion ya Billion 3 kando ya bahari halafu huyo huyo anajiita ni mtoto wa mkulima. Hapana, ni lazima tuambieane hivyo vijisenti wamevitoa wapi.

Namaliza kwa kusema hata kama Dr Edward Hossea alikuwa ni CABALIST wa PUBLIC ENEMIES. Kuna kitu kwenye kitabu chake CORRUPTION IN TANZANIA kinasema kwamba tusiegemee sana kwenye Sheria za Uingereza au COMMON LAW hasa kwenye kutoa ushahidi kwa makosa kama rushwa na utakatishaji wa pesa.

Ni lazima tubuni njia zetu sisi binafisi ambazo zitaweza kutatua matatizo yetu kama Watanzania na siyo kukimbilia sheria za wazungu ambazo zimetungwa mwaka 1947 kwa ajili ya watu wa Uingereza.

Mwaka 2012 FINANCIAL TASK FORCE (FATF) au kikosi kazi cha kupigana na rushwa na utakatishaji wa pesa cha kikundi cha nchi Tajiri saba hapa duniani au G7; kwenye mkutano wa mawaziri walitoa mapendekezo au 2012 FATF

RECOMMENDATIONS ambazo zilisema kwa uwazi kabisa njia raisi ya kushughulikia rushwa na utakatishaji wa pesa ni kumwambia mtuhumiwa athibitishe kwamba pesa zake ni za halali. Hapa nadhani utawapunguzia mzigo mawakili wetu na mwishowe wizi utapungua kwa kiasi. Wezi watanyang'anywa mali na huku wakijutia jela udhalimu waliotufanyia. Ukibadilisha sheria hatutategemea kusikia watu fulani fulani wakisema unavunja haki za binadamu wakati THIS IS JUST THE MATTER OF PROCEDURE.

Mkuu izzo unaweza kuongezea kitu hapa.

Natanguliza shukrani zangu.
Young Malcom.

Rejeo:Rais Magufuli, tatizo sio kuficha pesa ila utakatishaji - JamiiForums
 
Tuambie kwanza wewe unaelewaje..
Mimi navyofahamu ni kujipatia pesa kwa njia isiyo ya halali na kuileta kwenye mzunguko ulio wa halali..
Mfano ukifanya ujangili wa pembe za ndovu ukaemda kuziuza huko ukarudi na pesa ukafungua duka
 
Tafadhali husitumie tafsiri bali kukingana na namna Tanzania au sheria za Tz zilivyo,

Karibu
Kamuulize uyu ..kama ume mjua
tapatalk_1543609219191.jpeg
 
Duh! Umeshusha nondo haswa!
Hili suala la DPP nafikili ata yeye sometime halipendi pia unakuta mtu anakamtwa na meno ya tembo labda then unaambiwa upelelezi unaendelea! sasa muna peleleza nini wakati mumemkuta navyo kweupe kabisa!
 
Nimekuwa nikisikia jambo hili ika kiukweli sijaelewa ,karibuni kuchangia
Ninavyoelewa mimi ni kitendo cha kuingiza kwenye mzunguko fedha ambayo haikupatikana kihalali. Mfano pesa ambayo mtu ameipata kwa kuuza dawa za kulevya(ambayo ni kinyume na sheria) anaitengenezea mazingira fulani kama vile biashara au shughuli nyingine ambayo itaonekana km ile pesa imepatikana kwa namna hiyo ambayo ni halali. Wajuvi wataeleza vizuri zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kiswahili ndiyo hivyo kwa kingereza ni Money loundering.
Ni kitendo cha kufanya pesa haramu ( zilizopatikana kwa njia isiyo sahihi kuiweka kuwa sahihi).
Mfano unauza madawa ya kulevya , silaha pesa unazozipata ni haramu. Lakini unazisafisha kwa kupitia miradi vivuli au unazigawanya kwenye account za banks nk.
Nimejaribu in nutshell ila kama haujaelewa niambie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kiswahili ndiyo hivyo kwa kingereza ni Money loundering act.
Ni kitendo cha kufanya pesa haramu ( zilizopatikana kwa njia isiyo sahihi kuiweka kuwa sahihi).
Mfano unauza madawa ya kulevya , silaha pesa unazozipata ni haramu. Lakini unazisafisha kwa kupitia miradi vivuli au unazigawanya kwenye account za banks nk.
Nimejaribu in nutshell ila kama haujaelewa niambie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Money Loundering Act tenaaa. Hajaulizia sheria ya utakatishaji fedha. Ameulizia utakatishaji fedha tuuu
 
Kuzifanya pesa ulizozipata kwa njia haramu kuziingiza katika mzunguko halali.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom