Msaada: Ninawezaje kupokea pesa zaidi ya milioni 100 kutoka nje ya nchi kuja Tanzania

Habari.

Nahitaji msaada wa namna nitakavyoweza kupokea kiasi kikubwa cha pesa Tsh.100,000,000 kutoka nchi ya Afghanistan..... Njia nyingi za online transfer zinashindwa kutuma kiasi hicho cha pesa.

Nahitaji mawazo yenu.
Kwa mafungu je
 
Kama siyo chai, basi mtego huu....
Werevu muwe makini...

Mtu mwenye transaction ya 100M, usually siyo mgeni wa money transfers.

Kuna mtu anatafutwa au kitu chatafutwa..
Mie simooooooo...

Segerea kubaya! Wale wa njoo PM!

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Umeona enh! Manake ule utapeli wa kiboya nimeshangaa hadi miaka ya hivi sasa bado unaendelea!!! Sasa sijui wanampata nani!
Juzi kati nilijaza profile yangu kwenye mtandao wa Linkenld muda mchache akanifuata tapeli wa aina hiyo mpaka nikashangaa aisee ameichukuliaje profile yangu.​
Stori zilezile Baba aliacha $ za kutosha anataka kutransfer kwenye account yangu akatuma vipicha vya kijinga vyenye makeup.​
Nikasema ngoja nimchambulie online transfer zote mpaka ajione boya kabisa ajue kuwa kumbe hata waTZ siku hizi wapo uchumi wa kati!!!!.​
Kila nikimcheki Pm siku hizi kimya namkumbusha vipi achague njia itakayomfaa kati ya nilizomchambulia kimyaaa.​
Mwishowe nikamblock tu.​
Ila aliniacha na swali je Profile yangu ni ipo kilocal au Nchi ninayotoka?​
 
Bank wire itakuwa ni njia sahihi wa kiasi hicho cha pesa mkuu.
ila ni wazi unataka kutapeliwa, inakuaje mtu atake kukutumia kiasi hicho cha pesa halafu asijue akutumie kwa njia gani? Uko mbioni kutapeliwa kama Marehemu Dr.Shika hapo utaambiwa utume fees ya transfer kwa western union au money gram na ndiyo itakuwa mwisho wa kusikia hayo mamilion.
Yale yale ya baba yangu alikuwa afisa kwenye serikali ya Taliban, ana maela mengi aliuawa katika uvamizi wa srikali ya Marekani. Naataka nikutumie pesa halafu nije huko tuishe sote na unatumiwa na picha za mtoto wa kiatabu mtaaamu.
katoto kabichi kabisa ka kiarabu na wabongo tunavyopenda kuchakatana kuna kipindi 2010 kidogo niingie mkenge
 
Unatafuta kesi ya utakatishaji wa fedha. Kama ni biashara halali ingekuwa na documents zote kama za mauziano ya bidhaa au kitu kingine
 
Na utakatishaji pesa. Hapo hachomoki lazma akae ndani na pesa zake.
Hili suala la utakatishaji pesa mnali-mislead sana... haliendi hivyo! Yaani from nowhere awekwe ndani kisa tu pesa imetoka Afghanistan bila kuangalia imepitia kwenye channel zipi?
 
Juzi kati nilijaza profile yangu kwenye mtandao wa Linkenld muda mchache akanifuata tapeli wa aina hiyo mpaka nikashangaa aisee ameichukuliaje profile yangu.​
Stori zilezile Baba aliacha $ za kutosha anataka kutransfer kwenye account yangu akatuma vipicha vya kijinga vyenye makeup.​
Nikasema ngoja nimchambulie online transfer zote mpaka ajione boya kabisa ajue kuwa kumbe hata waTZ siku hizi wapo uchumi wa kati!!!!.​
Kila nikimcheki Pm siku hizi kimya namkumbusha vipi achague njia itakayomfaa kati ya nilizomchambulia kimyaaa.​
Mwishowe nikamblock tu.​
Ila aliniacha na swali je Profile yangu ni ipo kilocal au Nchi ninayotoka?​
Issue wala sio profile yako ipo vipi! Wale jamaa provided wana contacts zako, watakujaribu tu bila kujali profile yako inaonesha upo nchi gani!
 
Hili suala la utakatishaji pesa mnali-mislead sana... haliendi hivyo! Yaani from nowhere awekwe ndani kisa tu pesa imetoka Afghanistan bila kuangalia imepitia kwenye channel zipi?
mkuu kule arusha nazani mapaka leo kuna wakili yuko ndani alikutwa na ma bilioni hayaeleki ya nini jamaa wakasema yanahusiana na kuhamasisha ushoga waka m fix
 
mkuu kule arusha nazani mapaka leo kuna wakili yuko ndani alikutwa na ma bilioni hayaeleki ya nini jamaa wakasema yanahusiana na kuhamasisha ushoga waka m fix
Umeona hapo kwenye RED?! Hayaeleweki ya nini ndicho kilichomfanya awekwe ndani lakini sio kwa sababu ameingiziwa au amekutwa na hizo pesa!!

Kinachotokea ni hiki: Let's say wewe Kifinga kwa kawaida akaunti yako imeingiza pesa nyingi kwa mkupuo basi ni Credit ya TZS 5M.

Leo hii ukitumiwa pesa, let's say 50M, utaitwa ili utoe clarification; na haitajalisha ikiwa imetumwa kutoka Afghanistani, Iran, UK or USA... utaitwa tu!!

Lakini kubwa zaidi, kama aliyekutumia amefanya hivyo through the banking system, na huko alikotuma ana bank account (uwezekano mkubwa atakuwa nayo tu), basi bank ya huko tayari watakuwa "wanamfahamu" huyu "mteja" aliyekutumia wewe pesa vinginevyo, pesa ingepigwa stop huko huko!

Na kama nilivyosema kwenye post yangu ya awali, corresponding banks zinazoleta pesa TZ tena kutokea "Middle East" karibu zote kama sio zote zitakuwa ni benki za nchi magharibi, most likely benki za US, UK na German.

Hawawezi ku-route pesa zisizoeleweka zinatoka wapi!!

So, kwa issue hii: jamaa atapata taabu zaidi endapo ataletewa pesa kwa njia za panya na kisha anaenda kuzi-deposit benk! Lakini akitumiwa through the banking system, anaweza tu kuitwa ili aka-verify pesa zinatoka wapi, za matumizi gani, and all that!

Akijikanganya, ndo hapo kwenye RED... hazieleweki! Na kwa procedures kama hizo sio tu kama umetumiwa, hata ukienda ku-deposit wewe mwenyewe, utaulizwa tu! Ukishathibitisha kwamba pesa inatoka kwenye chanzo halali, na kwa matumizi halali, YANAISHA!

REMEMBER: Sio kila anayeishi Afghanistan ni gaidi/drug dealer au anajihusisha na ugaidi/drug trafficking! That being said, dunia haiwezi kuchukulia any money from Afghanistan is a dirty money!
 
katoto kabichi kabisa ka kiarabu na wabongo tunavyopenda kuchakatana kuna kipindi 2010 kidogo niingie mkenge
Hahahaha, yani huu wizi nilishashuhudia mtu anapigwa namtazama hivi hivi pasipo kusema neno maana ningesema ningeonekana namuonea donge. Jamaa alipigwa boom lake tukiwa chuo back in the days eti na anyedai yuko dakar senegal kambi ya wakimbizi.
 
Habari.

Nahitaji msaada wa namna nitakavyoweza kupokea kiasi kikubwa cha pesa Tsh.100,000,000 kutoka nchi ya Afghanistan..... Njia nyingi za online transfer zinashindwa kutuma kiasi hicho cha pesa.

Nahitaji mawazo yenu.
Vipi, ufadhili wa ugaidi au uchaguzi wa tundu?
 
Back
Top Bottom