Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Kwa yoyote anayejua dawa ya asili ya vidonda vya tumbo naomba anijuze tafadhari
Mkuu pole Sana aise mi Nilikuwa na vidonda vya tumbo vikali sana hadi nilifikiri nina cancer ya tumbo, Sasa Kuna dawa nilipewa kutoka Morogoro kwa sh 40 elfu tu nilielekezwa na mzee mmoja hapa yaani sisikii tena maumivu Niko vzr kabisa hii wiki ya pili Niko vzr.

Ngoja nisubiri Kama mwezi hivi au miezi miliwili ili nione Kama nimepona kweli au vitarudi tena then nitakwambia ukachukue pia hiyo dawa usije kuta ninepigwa nawewe ukapigwa pia.
 
Asali pia ni dawa unachanganya na kuna Dawa ya mti fulani hivi kwa kweli jina lake silijui ila ipo vizuri sana ,nilienda mkoani nikaenda mwenyewe kuchimba huo mzizi alafu inatwangwa inakuwa kama unga ndio unatumia ukishachanganya na Asali,upo maeneo gani nikupe bure kabisa hii dawa maana nilibakisha baada ya mgonjwa kuona amepona.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app

Yaani unapona kabisaaa?
 
Mkuu pole Sana aise mi Nilikuwa na vidonda vya tumbo vikali sana hadi nilifikiri nina cancer ya tumbo, Sasa Kuna dawa nilipewa kutoka Morogoro kwa sh 40 elfu tu nilielekezwa na mzee mmoja hapa yaani sisikii tena maumivu Niko vzr kabisa hii wiki ya pili Niko vzr.

Ngoja nisubiri Kama mwezi hivi au miezi miliwili ili nione Kama nimepona kweli au vitarudi tena then nitakwambia ukachukue pia hiyo dawa usije kuta ninepigwa nawewe ukapigwa pia.
Mkuu utujuze nasi
 
Kwa hali uliyo nayo inahitaji life style modification pia matumizi mazuri ya ppi.Epuka ushauri wa mtaani maana utapoteza pesa bila mafanikio yeyote.
 
Chakula ni tiba kubwa, chemsha iliki na mdalasini asubuhi weka asali.
Kula kabichi kwa wingi.
kuhusu mdalasini na iliki na asali ambayo sio ya supermarket nakuunga mkono itapunguza tatizo inategemea na vyakula atakavyo endelea kutumia visiwe na asidi. Organic foods ni suluhisho bofya hapa kuvijua.
Kabichi napendekeza isitumike ni GMO na ina acid ya pH kati ya 5.50 - 6.75.

UMETOA MCHANGO MZURI SANA
 
Pole sana mkuu, mwenyewe nilikuwa na tatzo hilo ila kwa sasa nashukuru kwa kweli.

Kama upo mwanza nicheki nikuunge na mjomba angu akupe namba ya mzee mmoja hivi alienisaidia dawa ya mti shamba, kwa maelezo yake ni kutoka Congo. Na bei yake ni elf40 zipo dawa mbili, Unatumia siku 8 tu.

Tiba nyingine ni mchanganyiko wa Asali na samri unatumia kutwa mara 3. Ndani ya siku 7 had 14 utaona matokeo.Hii niliambiwa mwarabu mmoja hivi.

Kitu kingine punguza vyakula vya gesi na Acid, vimiminika vyote vya kiwandani ( soda, juice nk), chps na pilipili.
Pendelea maziwa mtindi zaidi na si freshi, kula mboga za majani.

Tumia bamia mchemsho pekee kama utaweza atleast mara 2 kwa siku, punguza hasira, kula kwa wakati na acha mawazo yasiyo ya lazima. Mwisho kabisa mazoezi ni muhimu kwa Afya yako.

NB:Mie si daktari ni mawazo na ushauri niliopewa kwa madaktari na watu mbali mbali.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom