Msaada; Nina tatizo la kuona na kusikia vyote kwa pamoja

Ni miaka saba sasa imepita tangu nipate tatizo hili la kuona na kusikia,macho yangu hayana maumivu ya aina yoyote, hayawashi, hayachomi wala hayanisumbui kwa chochote isipokuwa kutoona vizuri.

Masikio yenyewe hunipa usumbufu wa kutoa mwangwi ndani yake (yaani nikiongea najisikia) hasa naposimama kwa muda mrefu, napotembea juani sana, ninapokuwa na njaa ila nikikaa chini mwangwi hupotea au ninapogeuza shingo.

Matatizo mengine yanayoambatana na hili ni kupatwa na ganzi ktk ncha za vidole vyote vya mikono, Kukosa balance napokuwa natembea pamoja na kutokuwa na nguvu ya kutosha ya mwili.

TAFADHALI KAMA KUNA MWENYE UELEWA AU DAKTARI BINGWA NAOMBA MSAADA KUJUA TATIZO LANGU LINATIBIKA AU LA.
Pokea uponyaji kwa jina la Yesu
 
Yes,mimi nina usikivu mdogo na macho yangu hayaoni vizuri nikisoma,kwahiyo navaa miwani.Ukweli maisha haya yana changamoto nyingi sana,kuna wakati inabidi uwe mpole na kukaa kimya kwani unaweza kujikuta unachangia kitu kisichokuwepo,vitu kama mitandao vimenisaidia sana kuniondolea upweke especially inapotokea kuna watu wanaongea jambo na mimi siwasikii...
Ni kweli mkuu cha msingi ni kujikubali tu,changamoto ni nyingi sana mwenzio nimeshawaamkia sana watoto kwa kutokuwaona vizuri basi hadi nimekuwa siamkii tena hadi nijiridhishe km huyu mtu ni mkubwa kuliko mm ndo naanguka shikamoo.

Bora hata ww miwani inakusaidia mm mwenzio hakuna miwani inayonisaidia so sina namna
 
Pole sana mkuu kweli dunianu kuna changamoto sana kuna binadamu hawajua kabla ujafa haujsumbika.

Embu jaribu kupitiapitia makala za Dr Boaz mkumbo kuhusu athari za sukari na wanga zinaweza kukusaidia pia labda mfumo wa mwili haupo sawa sehemu.
 
Asante sana mkuu,ni kweli ukishapata changamoto ndio unajua watu na aina zao.

Kiukweli nyakati za mwanzo nilipata shida sana nilikuwa naishi hapo Mapipa mtaa wa dossi basi kwenye kuvuka barabara ilikuwa ni kwa kukimbia hata km gari ndo ilikuwa imevuka tu taa maana nilikuwa sioni umbali halisi but nowdays nashukuru sana Mungu kunipa namna ya kukabiliana na hali yangu ili niweze kuyamudu mazingira mpaka sasa nina uwezo wa kuendesha chombo cha moto bila shida but speed ya kistaarabu.

By the way huyo dr. Boaz mbona simfahamu na hizo makala zake zinapatikana wapi?
 
Ni miaka saba sasa imepita tangu nipate tatizo hili la kuona na kusikia,macho yangu hayana maumivu ya aina yoyote, hayawashi, hayachomi wala hayanisumbui kwa chochote isipokuwa kutoona vizuri.

Masikio yenyewe hunipa usumbufu wa kutoa mwangwi ndani yake (yaani nikiongea najisikia) hasa naposimama kwa muda mrefu, napotembea juani sana, ninapokuwa na njaa ila nikikaa chini mwangwi hupotea au ninapogeuza shingo.

Matatizo mengine yanayoambatana na hili ni kupatwa na ganzi ktk ncha za vidole vyote vya mikono, Kukosa balance napokuwa natembea pamoja na kutokuwa na nguvu ya kutosha ya mwili.

TAFADHALI KAMA KUNA MWENYE UELEWA AU DAKTARI BINGWA NAOMBA MSAADA KUJUA TATIZO LANGU LINATIBIKA AU LA.
Daaah huyu mimi kabisa huyu,tuna tatizo moja mkuu hujaacha wala hujaongeza kitu ni mulemule kabisa.
 
Kizunguzungu hapana ni ile kukosa tu balance ya mwendo mfano uniambie nitembee huku natazama nyuma au naangalia juu yaani utadhani kidogo nimeonja kinywaji yaani natembea zigzag.
Ndio ndio mkuu mimi kabisa aisee....hata nikijifuta jasho ile kupitisha kitambaa usoni ni shida.

Miguu kama unailazmisha halafu haina nguvu kabisa.
 
Mkuu pole sana!
Tatizo kama hili lilimpata mdogo wangu na tulihangaika sana lkn ikaja gundulika baadae na matibabu yake ni simple mno!
Nadhani tatizo lako ni chemical imbalances,nenda LAB wakupime so called blood biometric.
Wataalam wapine madini yote mwilini mwako na blood plasmas
Sisi dogo walikuta kakosa madini Magnesium na Dr akasema ukosefu wa madini wengine huwafanya hadi wawe mental unstable!
Pole sana na please kapime blood biometric nina imani watagundua una ukosefu wa madini fulani,ukianza matibabu unapona completely
Mkuu ni kiasi gani hki kipimo
 
Asante sana mkuu,ni kweli ukishapata changamoto ndio unajua watu na aina zao.

Kiukweli nyakati za mwanzo nilipata shida sana nilikuwa naishi hapo Mapipa mtaa wa dossi basi kwenye kuvuka barabara ilikuwa ni kwa kukimbia hata km gari ndo ilikuwa imevuka tu taa maana nilikuwa sioni umbali halisi but nowdays nashukuru sana Mungu kunipa namna ya kukabiliana na hali yangu ili niweze kuyamudu mazingira mpaka sasa nina uwezo wa kuendesha chombo cha moto bila shida but speed ya kistaarabu.

By the way huyo dr. Boaz mbona simfahamu na hizo makala zake zinapatikana wapi?
Pole sana mkuu ndio changamoto kila jaribu lina mlango wa kutokea uwezi pewa mtihani usiohumudu, ndio maana umeshayazoea maisha hayo.

Dr Boaz anapatikana sana youtube, instagram na facebook. Kwa sababu ya tatizo la kusikia nashauri mfatilie sana facebook au instagram

Pia ana blog yake.
 
Aisee tupo wengi yani Mimi kunachosumbua sana ni mishipa ya masikio kuvuta mpaka kwenye utosi unasikia Kama hali ya kuchanganyikiwa Kisha kupepesuka ndio tabuuu asee
Ndio ndio mkuu mimi kabisa aisee....hata nikijifuta jasho ile kupitisha kitambaa usoni ni shida.

Miguu kama unailazmisha halafu haina nguvu kabisa.
 
Hili tatizo la mishipa ya fahamu linawakuta watu wengi saana nowdays.

Mimi pia lilinipata.. Uoni ulikua hafifu ganzi ilinikamata pia nikapatwa na half of hearing yani masikio unasikia mivumo mda wote

Pia balance ilishuka ni kizunguzungu muda wote haswa nikiwa gizani

Nilikuja kutumia Neuroton tablets tatizo la macho likaisha, ganzi pia ikapungua, ila kizunguzungu na kutosikia vizuri kukaendelea
 
Mkuu pole sana!
Tatizo kama hili lilimpata mdogo wangu na tulihangaika sana lkn ikaja gundulika baadae na matibabu yake ni simple mno!
Nadhani tatizo lako ni chemical imbalances,nenda LAB wakupime so called blood biometric.
Wataalam wapine madini yote mwilini mwako na blood plasmas
Sisi dogo walikuta kakosa madini Magnesium na Dr akasema ukosefu wa madini wengine huwafanya hadi wawe mental unstable!
Pole sana na please kapime blood biometric nina imani watagundua una ukosefu wa madini fulani,ukianza matibabu unapona completely
Mkuu mlitumia kiasi gani kupima hicho kipimo?
 
Hili tatizo la mishipa y a fahamu linawakuta watu wengi saana nowdays.

Mimi pia lilinipata.. Uoni ulikua hafifu ganzi ilinikamata pia nikapatwa na half of hearing yani masikio unasikia mivumo mda wote

Pia balance ilishuka ni kizunguzungu muda wote haswa nikiwa gizani

Nilikuja kutumia Neuroton tablets tatizo la macho likaisha, ganzi pia ikapungua, ila kizunguzungu na kutosikia vizuri kukaendelea
Ulikua unapepesuka??
 
Daaah .

Yah.. Kama Nikitembea gizani au kufumba macho

Daaah Mimi napepesuka tuuh ata nisipo fumba macho yani nikiwa natembea tuuh kawaida nakoswa balance.
Sasa Kuna jamaa mmoja ananitisha Apa ananiambia labda uvimbe kwenye ubongo duuuh
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom