Msaada; Nina tatizo la kuona na kusikia vyote kwa pamoja

Kwa ww km shida ni nguvu tu mkuu nakushauri tumia Neuro support kwa muda wa miezi 3 mfululizo aisee utarejesha nguvu ya mwili mm ilifika kipindi nilikuwa sina nguvu kabisa but nilitumia kwa muda km huo kiukweli niliona mabadiliko makubwa sana.Dozi ya mwezi ni vidonge 30 ambayo ni 15,000
Mkuu ungeweka na picha ya vidongr hivyo kama unayo ingekua rahisi sana kwa mtu anayeenda kununua.
 
Ni miaka saba sasa imepita tangu nipate tatizo hili la kuona na kusikia,macho yangu hayana maumivu ya aina yoyote, hayawashi, hayachomi wala hayanisumbui kwa chochote isipokuwa kutoona vizuri.

Masikio yenyewe hunipa usumbufu wa kutoa mwangwi ndani yake (yaani nikiongea najisikia) hasa naposimama kwa muda mrefu, napotembea juani sana, ninapokuwa na njaa ila nikikaa chini mwangwi hupotea au ninapogeuza shingo.

Matatizo mengine yanayoambatana na hili ni kupatwa na ganzi ktk ncha za vidole vyote vya mikono, Kukosa balance napokuwa natembea pamoja na kutokuwa na nguvu ya kutosha ya mwili.

TAFADHALI KAMA KUNA MWENYE UELEWA AU DAKTARI BINGWA NAOMBA MSAADA KUJUA TATIZO LANGU LINATIBIKA AU LA.
Mkuu matatizo yako yanafanana sana na yangu.
Mimi mwenyewe pia Nina ugonjwa wa masikio kwa muda mrefu then baadae na macho yakaanza kupunguza nguvu ya kuona.
Baadae nikaanza kutembelea hospitali mbalimbali ikiwemo hiyo uliyotaja ya CCBRT lakini Cha ajabu badala ya kutafuta chanzo wanakimbilia kutoa miwani.
Nikavaa miwani kwa miezi kadhaa nikaona ujinga nikaachana nao.
Sasa miezi kadhaa iliyopita nikawa nasoma posts mbalimbali za mitandao ya ulaya nikaja kugundua kumbe Kuna muingiliano wa mishipa ya masikio na macho.
Kwa hyo kwa vile mishipa yangu ya masikio iliathirika tangu zamani ikapelekea na macho yangu kuwa na uono hafifu.
So macho yangu yanakosa command sahihi from the brain na huwa yana irregular blinking.
So kwa tatizo lako wewe unatakiwa ufuatilie tatizo la masikio kwanza yachunguzwe then badae ndio uende kwenye macho.
Specialists wa masikio wapo TMJ,Agakhan au Muhimbili.
Ukipita sehemu hizo naamini utapata solution.
 
Dah aisee bora tufahamiane walau tusijione wapweke au tuliosahaulika na Mola.

Ipo siku tutarejea kwenye hali zetu za mwanzo naamini
Ndugu mimi nina tatizo hilo la neva, linaweza kunifanya nisisikie kabisa au ubongo uchelewe kupata taarifa. Unakuta namuuliza mtu Unasemaje? Hapohapo najua alimaanisha nini, wengine wabaona nawafanyia kusudi. Kumbe ni tatizo kubwa.

Nilipatiwa hearing aid lakini ilibidi niiache maana inaharibu masikio na mimi sikio ni zima halina tatizo. Ni hizo neva tu
 
Mkuu kama hukuwa kiziwi wkt unazaliwa huwezi ukawa kiziwi ukiwa mkubwa
Ni excess pressure ktk canals,muone dr bingwa
Mdogo wangu alipona completely baada ya kuchukuliwa damu
Mdogo wako alitibiwa hadi akapona katika hospital gani na chini ya Dr gan?
 
Hili suala wakuu tulifungulie group la whatsapp ili tukatane huko mara kwa mara, kule itakuwa rahis zaidi watu kufunguka kwa uhuru.
 
Mdogo wako alitibiwa hadi akapona katika hospital gani na chini ya Dr gan?
Muhimbili hapo,nenda hospital yyt ya wilaya mwambie dr akuandikie rufaa
Ni rahisi tu na pale watachukua tu damu
 
Wanatumia ndio mkuu,km unayo we nenda tu utahudumiwa kama mfalme wako vizuri hamna yale mambo sijui fumba jicho la kulia usome pale.

Pale kila kitu kidigitali unaambiwa weka macho kwenye hii mashine anaset kacha kacha herufi inahamia jicho moja mpaka jingine.
Shukrani mkuu
 
Hili suala wakuu tulifungulie group la whatsapp ili tukatane huko mara kwa mara, kule itakuwa rahis zaidi watu kufunguka kwa uhuru.
Ngoja tuangalie possubility tunawrza kufanya hivyo kwa kweli tukaweza kupeana experience
 
Kwa ww km shida ni nguvu tu mkuu nakushauri tumia Neuro support kwa muda wa miezi 3 mfululizo aisee utarejesha nguvu ya mwili mm ilifika kipindi nilikuwa sina nguvu kabisa but nilitumia kwa muda km huo kiukweli niliona mabadiliko makubwa sana.Dozi ya mwezi ni vidonge 30 ambayo ni 15,000
Unamaanisha vidonge vya Neuroton?
Nilitumia sana hivi ila nikapona macho na ganzi tu.. Ila Masikio na body balance bado vinasumbua
8be0b6299d412d25782a773342617d1d28e91606.jpg
 
Hiyo ni peripheral Neuropathy yaani kama ni kutibu sijui macho au masikio utazunguka hospital zote.
 
Tiba take ndio ipi
Kama ni ya kurithi hakuna tiba

Kama chanzo ni Vitamin B deficiency ndo kuna Neuroton,Neuro support na zingine nyingi

Nina ndugu yangu ana 15+yrs akipambana,kafanya CT Scan,MRI,na vipimo kibao lakini bado kwa sasa hatumii dawa yoyote kakubali matokeo tu.
 
Kama ni ya kurithi hakuna tiba

Kama chanzo ni Vitamin B deficiency ndo kuna Neuroton,Neuro support na zingine nyingi

Nina ndugu yangu ana 15+yrs akipambana,kafanya CT Scan,MRI,na vipimo kibao lakini bado kwa sasa hatumii dawa yoyote kakubali matokeo tu.
nae pia anatatizo la kukosa balance
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom