Msaada: Nina tatizo la kubanwa na mkojo mara kwa mara

wete

Member
Nov 16, 2012
85
58
Nimekua nasumbuliwa na tatizo la mkojo, yaani unabana sana nisipowahi kukojoa unaanza kutoka vitone tone hasa unapokaribia choo ndo balaa, Kama asubuhi nakua sijala wala kunywa chochote lakini naweza kwenda hata zaidi ya mara 2 kwa lisaa choon. Hili tatizo linaninyima hata raha ya kunywa maji asubuhi kuhofia kwenda chooni mara kwa mara.

Kuna muda mwingine unaweza kubanwa sana ukifika kukojoa unatoka mkojo mdogo wa kawaida kulinganisha na ulivokua umebanwa unaona Kama kuna tatizo.

Nimepunguza Sana unywaji wa maji kutokana na tatizo hilo na mzingira yangu ya kazi na choo viko mbali kidogo.

Naombeni ushauri ndugu zangu.
 
Nimepunguza Sana unywaji wa maji kutokana na tatizo hilo na mzingira yangu ya kazi na choo viko mbali kidogo.
Kupunguza sana kunywa maji ni unasababisha tatizo kubwa zaidi kuliko hilo ulilonalo sasa hivi! Kutokunywa maji mengi husababisha maelfu ya magonjwa kama vile mawe kwenye kibofu, constipation ambayo itakuletea ugonjwa wa bawasiri, presha na kadhalika. Kwa kifupi kama umepunguza sana kunywa maji basi jua wewe ni maiti inayotembea!
 
Nimekua nasumbuliwa na tatizo la mkojo, yani unabana sana nisipowahi kukojoa unaanza kutoka vitone tone hasa unapokaribia choo ndo balaa, Kama asubuh nakua sijala wala kunywa chochote lakin naweza kwenda hata zaid ya mara 2 kwa lisaa choon. Hili tatizo linaninyima hata raha ya kunywa maji asubuh kuhofia kwenda chooni mara kwa mara...

Nadhani inabidi ukapime sukari katika damu.

Kama ni shida kwenda kupima kutokana na mazingira basi waweza tumia njia ya kienyeji, kojolea mkojo ndani ya chupa mfano chupa ya maji uhai halafu nenda kamwage huo mkojo mahali ambapo kuna nyenyere baada ya muda kama nusu au saa 1 nenda kaangalie ukiona wale nyenyere wameuzingira huo mkojo jinsi wanavyozingira ganda la mua basi ujue hiyo ni dalili ya kisukari, nenda hospitali kwa tiba na ushauri zaidi.
 
Mambo mawili yanakuhusu, i.Enlarged prostate
ii.Diabetes mellitus

Kama umri ni zaidi ya miaka 50 huenda una tatizo mojawapo katika hayo
 
Bosi pole sana!! hilo tatizo nilikua nalo mimi na sio sukari..usiku naweza amka hata zaidi ya mara 10 au 15...ila kuna mtu kanisaidia naona naendelea vizur!! kwa ushauri njoo PM
Mbona unatubania? Tutakuja wangapi huko pm?
 
Acha kupiga punyetto
Ndugu yangu amefanyiwa uchunguzi Muhimbili, wakakosa chanzo cha tatizo.
ila kuna kipimo Muhimbili kimeharibika, wamemwambia aende CCBRT.
Hivyo na wewe nenda hukohuko CCBRT labda utapata vipimo kwa haraka zaidi.
 
Mimi nina tatizo la kutokojoa mara kwa mara na maji nakunywa zaidi ya lita tatu kwa masaa 12 lakini ninaweza kojoa mara moja ama nisikojoe kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom