Msaada: Nina tatizo la kubanwa na mkojo mara kwa mara

wete

Member
Nov 16, 2012
75
125
Nimekua nasumbuliwa na tatizo la mkojo, yani unabana sana nisipowahi kukojoa unaanza kutoka vitone tone hasa unapokaribia choo ndo balaa, Kama asubuh nakua sijala wala kunywa chochote lakin naweza kwenda hata zaid ya mara 2 kwa lisaa choon. Hili tatizo linaninyima hata raha ya kunywa maji asubuh kuhofia kwenda chooni mara kwa mara.

Kuna muda mwingine unaweza kubanwa sana ukifika kukojoa unatoka mkojo mdogo wa kawaida kulinganisha na ulivokua umebanwa unaona Kama kunatatizo.

Nimepunguza Sana unywaji wa maji kutokana na tatizo hilo na mzingira yangu ya kazi na choo viko mbali kidogo.

Naomben ushauri ndugu zangu.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
34,826
2,000
Nimepunguza Sana unywaji wa maji kutokana na tatizo hilo na mzingira yangu ya kazi na choo viko mbali kidogo.
Kupunguza sana kunywa maji ni unasababisha tatizo kubwa zaidi kuliko hilo ulilonalo sasa hivi!Kutokunywa maji mengi husababisha maelfu ya magonjwa kama vile mawe kwenye kibofu,constipation ambayo itakuletea ugonjwa wa bawasiri,presha na kadhalika.kwa kifupi kama umepunguza sana kunywa maji basi jua wewe ni maiti inayotembea!
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
9,913
2,000
Nimekua nasumbuliwa na tatizo la mkojo, yani unabana sana nisipowahi kukojoa unaanza kutoka vitone tone hasa unapokaribia choo ndo balaa, Kama asubuh nakua sijala wala kunywa chochote lakin naweza kwenda hata zaid ya mara 2 kwa lisaa choon. Hili tatizo linaninyima hata raha ya kunywa maji asubuh kuhofia kwenda chooni mara kwa mara...

Nadhani inabidi ukapime sukari katika damu.

Kama ni shida kwenda kupima kutokana na mazingira basi waweza tumia njia ya kienyeji, kojolea mkojo ndani ya chupa mfano chupa ya maji uhai halafu nenda kamwage huo mkojo mahali ambapo kuna nyenyere baada ya muda kama nusu au saa 1 nenda kaangalie ukiona wale nyenyere wameuzingira huo mkojo jinsi wanavyozingira ganda la mua basi ujue hiyo ni dalili ya kisukari, nenda hospitali kwa tiba na ushauri zaidi.
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
41,723
2,000
Mambo mawili yanakuhusu, i.Enlarged prostate
ii.Diabetes mellitus

Kama umri ni zaidi ya miaka 50 huenda una tatizo mojawapo katika hayo
 

Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
25,344
2,000
Bosi pole sana!! hilo tatizo nilikua nalo mimi na sio sukari..usiku naweza amka hata zaidi ya mara 10 au 15...ila kuna mtu kanisaidia naona naendelea vizur!! kwa ushauri njoo PM
Mbona unatubania? Tutakuja wangapi huko pm?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom