Msaada: Nina presha 162/103 umri wangu miaka 33. Je, nianze dawa au nibadilishe lifestyle?

Wakuu habari zenu,

Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?
nenda hospital kwanza
 
Ni mapema sana ku rule out kuwa una Hypertension , inabidi uchukue vipimo mfululizo kama siku 5 hivi kila siku bila kukosa kwa nyakati tofauti , na readings utakazopata zitatoa mwongozo, iwapo itakuwa juu kila mara basi daktari atakuanzishia dawa. Lakini wakati huo huo badili life style yako, iwapo unavuta sigara acha, fanya mazoezi hata kama ni kutembea kama muda wa saa nzima hivi, punguza chumvi , mafuta nk
 
Haya mambo bana hayana fomula kuna wengine tuna digit mbili kila upande na tunadunda tu.

Huwa nasema miili ya wanadamu haifanani.

Ila Mkuu pole sana maana kwa comment zako tu inaonesha wewe ni mtu wakupanic sana, jaribu kuwa una relax Mkuu. More over kama unatumia vileo vya spirit kama K-Vant, Konyagi, Value achana navyo, hvyo vitu vinafanya mtu unakuwa na hasira za ghafla au mbishi mbishi
 
Kupanic huwa napanic Ila situmii kilevi Cha Aina yoyote ile
 
Dawa za kuondoa bad cholestrol ni zipi maana nahisi hio ndio itakuwa inansumbua mimi hata kabla sijaipima tu manaa nakula nyama daily!

Dawa kuu yakuondoa bad cholestrel kaka nikupunguza red meat, saturated and trans fats, bia na mazoezi. by the way pressure yako wala siyo mbaya 133/77 usikimbile madawa
 
Urefu wako? Kuna kitu kinaitwa BMI yaani Body Mass Index. Utefu au kimo chako na uzito wako ndiyo determinants za BMI. Ikizidi mpaka red ni hatari sana.

Kwanza usipaniki kabisa.

1. Anza na maji ya kunywa vuguvugu glass 4 kika asubuhi na mchana kunywa taratibu na jioni kabla ya kulala kunywa maji ya vuguvugu.

2. Acha kabisa refined wanga kama vitokanavyo na Michele, ngano kama chapati, maandazi n.k

3. Acha nyama nyekundu haraka mno.
4. Kula protein za mimes na nafaka zaidi. Na kidogo samani na kuku.

5. Kula mboga za majani kwa wingi sana na matunda ili uwe na space ndogo ya chakula. Kula mboga na matunda nusu saa kabla ya kula. Angalizo: kula mboga zaidi na matunda kiasi kwa kuwa yana sukari. Pia ukiweza punguza matunda yenye sukari nyingi. Google utaona sugar contents za matunda.

6. Kuhakikisha mlo wa mwisho uwe kuanzia saa 1 mpaka 2 usiku na uwe mwepesi.

7. Fanya light exercises kama kutembea taratibu maana kwa sasa presha iko juu hivyo mazoezi magumu yatakuletea shida ya presha kupanda zaidi.

8. Fanya Vipimo vya moyo ECG na ECHO ili kuona hali ya moyo kwa sasa na kama hakuna tatizo Dr atakuandikia vipimo vingine ambavyo vinahusiana na presha.

9. Pima cholestrol yaani wingi wa mafuta kwenye mishipa ya damu.

10. Pima hormones tests TSH, T3, T4 na Cortisol levels.

11. Pima Figo ( Renal Panel) na Sukari hasa fasting glucose. Acha kutumia sukari kwa sasa. Kunywa chai kavukavu au kunywa maji moto asubuhi inatosha.

Nataka nikuhakikishie kuwa Pressure inatibika kwa wewe mwenyewe kufanya maamuzi hasa kama inatokana na life style. Hata kama inatokana na hitilafu ya kwenye moyo bado unaweza kufanya control ya life style ili kupunguza overwork ya moyo.

Narudia pressure ni kubwa kidogo ila usiogope na itarudi haraka tu normal kama hakuna hitilafu kwenye moyo.

Mdogo mdogo kula punje 2 au 3 kitunguu swaumu kila asubuhi. Kunywa limao umelikata vipande na maganda yake ndani ya maji moto kila asubuhi na jioni. Usiweke Tangawizi kwa sasa.
 
Duh kweli mkuu maana kuna mahali niliona wanasema et namba ya juu ikiwa 132+ ni mbaya
 
Nilipima ECG na ECHO mwezi wa kwanza Wala sikuwa na shida yoyote na presha ilikua normal 128/80 Ila uzito ndo nimkubwa
 
Wakuu habari zenu,

Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?
Usianze dawa Kwanza cheki mara tatu ukiwa hauna stress yeyote maana pressure huwa na kasumba ya kupanda kutegemea na mapito yako

Lasix pekee kipindi hiki yaweza kukupa uahueni lkn kacheki Kwanza kujua chanzo ni nn

Vipimo vya moyo
Figo na damu visaidie
 
Nilipima ECG na ECHO mwezi wa kwanza Wala sikuwa na shida yoyote na presha ilikua normal 128/80 Ila uzito ndo nimkubwa
Basi piga mzigo kama nilivyokuekeza hapo na chumvi acha kabisa kwa miezi kama mitatu hivi. Ikishakuwa normal unakula chumvi kidogo kabisa ili usikose Iodine. Au pia ujitahidi kula vya kula yenye iodine kwa wingi ili uache chumvi. Baada ya miezi 3 leta mrejesho hapa ili uwe ni ushuhuda kwa wengine.
 
Vp mazoezi kwahii presha nikiyaanza Itakua shida? Je presha itapanda Zaid pindi nikiwa nafanya mazoezi?
Haiathiri Kabisa maana kukimbia ni zoezi natural ambapo huwezi kukimbia zaidi ya nguvu uliyo nayo ila kwa ushauri wangu anza kwa kutembea haraka kwa mda wa dk 40 -50 kisha unafanya stretch baada ya hapo kimbia taratibu kwa 30dk
Kifupi mazoezi ndio tiba halisi na baada ya mda tatizo linaondoka
Pia marekebisho ya chakula ni muhim sana utakaa poa ila kutembea ni muhim sana
 
Vp mazoezi kwahii presha nikiyaanza Itakua shida? Je presha itapanda Zaid pindi nikiwa nafanya mazoezi?
Watu wanafanya mazoezi na 180 boss na maisha yanaenda na kwa sasa usijikite sana kwenye kupima maana una hofu kwa hiyo utakuta matokeo hayo hayo Fanya mazoezi kula poa songa mbele yenyewe itaamua ikae au iondoke hivyo tu usiache kusali maana siku hizi waswahili nao hutumia nafasi hizo
 
Kwa Umri wako hatutegemei uwe na Pressure.

Na kama umepima mara moja tu ukakuta iko juu unatakiwa urudie walau mara tatu kwa nyakati tofauti, hatuwezi jua ulipopima labda ulikua kwenye Panic/Fear. Namaanisha bila kurudia mara tatu tutabaki kuita WhiteCoat Hypertension(HTN kwa sababu ya woga wa mazingira ya hospitali)

Iwapo itabaki kuwa Juu baada ya kurudia walau mara tatu kwa siku tofauti basi shughulikia mambo yafuatayo.

BMI yako iko je?
Pima uzito wako na Urefu wako nenda Playstore au Appstore tafuta BMI calculator.

Utaitaji check out kubwa ya Figo, Goitre n.k ambavyo daktari wako inabidi akifanyie kunua sababu kwa nini unapata Hypertension udogoni.

Ikumbukwe kuna kitu kinaitwa Secondary Hypertension....Hii hata umeze dawa inaweza isisaidie iwapo hizo dawa hazitibu chanzo husika.

Fika hospitali wanayoweza kuku evaluate...Hypertension ni ugonjwa hatari sio wa kuombea ushauri hata mitandaoni
Chief sorry, kwa faida yetu sisi tusiofahamu.. BMI ni kitu gani? Na nini faida ya kufahamu BMI yako? Na unaisomaje kama hutojali chief
 
BMI ni BODY MASS INDEX yaani ratio kati ya height na weight nayo inatakiwa isizidi 26. Nimesahau jinsi ya kukokotoa ila najuwa waelewa watakuja kutufahamisha.
 
Wakuu habari zenu,

Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?
Ulipima pressure ukiwa katika mazingira gani mkuu ?

Sio unapima pressure ukiwa na stress zako umetoka zako huko umevurugwa una hofu na wasiwasi unaenda kupima pressure hiyo haikubaliki.

Pressure unatakiwa kupima ukiwa umerelax umetulia sio mtu kafiwa na mke wake unaenda kumpima pressure ati kwa kutegemea itakuwa normal.

Kuna mambo ambayo mtu yakimuandama huwezi kuhukumu kuwa hiyo ni pressure yake kwa sababu kuna mambo kikawaida hupandisha ama kushusha pressure.

Mtu katoka kwenye chombo kuendesha pikipiki usiku kapigwa na baridi kaja hospitali unataka umpime body temperature,lazima ikudanganye hapo unatakiwa usubiri upite muda,ukilazimisha kumpima hivyo hivyo utaona tempretaure iko sawa kumbe mwenzio imepanda ila hujagundua kwa sababu mwili una joto kwa wakati ule.

Ushauri wangu mkuu kwanza naomba upime kwenye zile mashine za kupampu kwa mkono kisha unasoma na sio zile za kubofya tu zinajijaza zenyewe upepo kwenye mkono

Yani tumia zile za mkono kuliko zile za umeme,hiyo kwa uzoefu wangu finyu naona zile za umeme kama sometimes siziamini kiivyo

Llakini pili ebu hakikisha unapopima pressure unakuwa umetulia zako tuli hujafanya shughuli yeyote ngumu ama jambo lolote la kukutia wasiwasi zaidi.

Kumbuka kuwa normal body condition inapatikana kwa mtu kuwa katika normal external environment.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom