Msaada: Nina kesi ya wizi baada ya kununua bidhaa Kupatana.com

Tabia ya kupenda kununua electronic equipments au magari kutoka mikononi mwa watu ni hatarishi sana. Kuna rafiki yangu mmoja alidhani kaokota dodo jangwani na kununua Ipad kwa bei poa. Alikuja kuokotwa Mlimani City kama kifaranga cha bata. He had to pay excessively kumaliza lile soo.
Mimi binafsi mwaka huuhuu jamaa nilimkamata kama bwege. Alinunuansimu ya wizi nikamtrack.

Wezi ni watu wabaya sana na wanarudisha maendeleo ya watu nyuma. Sasa na sisi kununua kitu bila ya uhakika na chanzo chake ni kuwasapoti wezi. Lazima watu wajifunze.
Nina uhakika nilichomfanyia yeye na ukoo wake wote hawatarudia makosa yale!
 
Kama una chating na huyo muuzaji basi kesi imekwisha hapo.
Kwa namna ambavyo Jeshi letu linavyofanya kazi zake, hizo chatting hazitasaidia chochote.

Utakuwa na kazi ya kulisaidia jeshi na muda wote utakuwa ndani. Jambo la kuomba ni kuwa hiyo bidhaa isiwe imepatikana kwa makosa ya ujambazi au mtu kudhuliwa mwili.

Vinginevyo inabidi aonyeshe ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kesi iishe vinginevyo anaweza kwenda kupumzika segadansi.

Mungu amsaidie tu kwa kweli.
 
Pole Sana...

Nina rafiki wa mdogo wangu fundi simu kariakoo aliuziwa simu ya mkononi yeye na wenzake wawili..kilichowakuta ni kulala selo siku 3 na fidia juu...vya mkononi gharama.
 
Hahahaa yeye amenunua online inatakiwa mwenye zoom ndio awe anaverify uhalali wa bidhaa na muuzaji,mimi ni mteja tu.
Umeongea kitu ambacho watu wanakikwepa.

Jamaa kanunua kitu Online, kupatana wamesajiliwa wanauza vitu vya wizi.

Kule kupatana unatakiwa ujisajili ili uweze kuuza kitu. Je mwenye makosa ni kupatana au mnunuzi?

Mkuu nenda mahakamani unashinda hii kesi.
 
Kwani
Habari, naomba ushauri juu hili suala.

Nilinunua bidhaa kupitia mtandao wa Kupatana. Sasa nakabiliwa na kesi ya wizi.

Naombeni ushauri juu ya hili.
Kwani hukudai risiti? Uhalali wa mauziano Ni risiti. Kama ungenunua gari kupatana je usingedai kadi? Usingeenda TRA kubadilishana jina?
 
Umeongea kitu ambacho watu wanakikwepa.

Jamaa kanunua kitu Online, kupatana wamesajiliwa wanauza vitu vya wizi.

Kule kupatana unatakiwa ujisajili ili uweze kuuza kitu. Je mwenye makosa ni kupatana au mnunuzi?

Mkuu nenda mahakamani unashinda hii kesi.
Kasome terms and conditions prio kujiunga.
Pia kasome disclaimer
 
Mkuu vitu second hand vya mbongo ni mkosi, utakuja kupata kesi ya kichwa.
fikiria kama iliko ibwa kauwawa mtu, au vyuma vya moto vilitumika.

Only buy what you can afford, if you can't buy direct from the shop because it's expensive, then wait until you can afford it.
. Very well advice
 
Umeongea kitu ambacho watu wanakikwepa.

Jamaa kanunua kitu Online, kupatana wamesajiliwa wanauza vitu vya wizi.

Kule kupatana unatakiwa ujisajili ili uweze kuuza kitu. Je mwenye makosa ni kupatana au mnunuzi?

Mkuu nenda mahakamani unashinda hii kesi.
Sure hajanunua kwa mtu barabarani. Hii inafanya wengine kuogopa kufanya biashara kupitia hiyo kupatana
 
Hawa watu wa kupatana its better wakawa wanawaverify user wao kama ilivo Ebay au Amazon... Itasaidia kwa upande fulani...
 
Umeongea kitu ambacho watu wanakikwepa.

Jamaa kanunua kitu Online, kupatana wamesajiliwa wanauza vitu vya wizi.

Kule kupatana unatakiwa ujisajili ili uweze kuuza kitu. Je mwenye makosa ni kupatana au mnunuzi?

Mkuu nenda mahakamani unashinda hii kesi.
Mwenye Makosa ni Kupatana yeye ndio mwenye authority ya kuverify wauzaji wake kama genuine na wanaweka vitu genuine na ikitokea fraud au sintofahamu yeyote kupatana ndio atoe taarifa wapi muuzaji anapatikana.
 
Mtoa mada tafuta mwanasheria akupe legal opinion.

Hilo suala lako ni dogo sana.

Huku ninaona umekutana na waswahili badala ya kukusaidia wanakuogopesha.

Hawa wamezoea mipasho.

Kimsingi suala lako linamalizika kirahisi.

Achana na makanjanja ya jeiefu
 
Back
Top Bottom