Msaada: Nimuambie mke wangu kama nina mtoto nje ya ndoa?

Mshenzi mkubwa wee. Hivi unakuwaje na roho mbaya kiasi hicho kwa mtu uliyewahi kumpenda? Unachofanya ni conspiracy to murder.Utamletea maradhi mkeo.
Unatakiwa ushitakiwe kwa kuhatarisha maisha yake. Unapitapita mkavu mkavu? Huko unakopita pita unajua na hao wamepitiwa na nani na wanapita wapi? Kama umechoka maisha si ujirushe mwenyewe, yanini uhatarishe na maisha ya mwenzio? Hopefully, hamna watoto na mkeo ningemjua ningemwambia, akapime afya.

Acha ubinafsi, mueleze umalaya unaoufanya ili achukuwe tahadhari dhidi yako.
Wewe ni me au ke?
 
Kwa mwanamke mwenye akili na mwenye uwelewa atajua kuwa mwanaume kuzalisha mtoto nje ni rahisi sana na ni jambo la siku moja

Hivyo mpime kwanza mkeo kama kifua au uvumilivu moyo anao? Then umwambie lkn pia badili mfumo wa maisha yako yako kuishi na mkeo mbali sio vyema hasa kwa muda mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimwambia, akija kujua mwenyewe vyote sawa. Ukishajua mwanaume unayemuamimi, unayempenda, kumthamini sio mwaminifu upendo huisha na yanabaki maigizo. Mnapenda kujidanganya wanawake wanasamehe usaliti huwa sio kweli wanabaki na tahadhari za kiuchumi, na kuigiza mno. Ndio maana watoto wakikua atawahadithia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usimwambie kabisa.. Maana ataumia na uaminifu utakua hamna tena. Subiri ajue mwenyewe ili upate mwanya wa kujitetea mbona simple tuu
 
Habari wakuu,

Kwa kifupi naishi mkoa tofauti na mke wangu kwa sababu za kikazi, sasa katika pitapita zangu kapatikana mtoto. Wife bado hajajua chochote kwa sababu hakai sana hapa ila najua kwa baadaye itakuja kufahamika kwa sababu kuna watu wanajua.

Sasa nataka kupata ushauri au uzoefu wa wadau kama nisubiri aje kujua mwenyewe au nijitutumue nikae naye chini nimueleze ukweli mwenyewe?

Note: Mke wangu hatujawahi kuwa na mgogoro wowote tunaishi vizuri kwa kuaminiana na upendo mkubwa.

Asante
Una uhakika gani huyo ni mwanao?

Kuna hatari na ww kati ya wale wanao uliozaa naye mkeo akakwambia mwanao wa kwanza si wa kwako utajiskiaje?

NB: natabiri ndoa yako itayumba indapo utatoa hyo habari kwa mkeo,,
 
Ilikuaje? ?

Vovote vile Lakini itabaki kua damu yake tu. Na mwisho wa siku itamhukumu

Cc Smart911
Inategemea huyo mke wake atalichukuliaje?

Kuna ishu kama hii nimeishuhudia,

Yule mtoto mapaka sasa naongea tayari RIP (mtoto ametangulia mbele ya hakhi)

Kwa sasa ni vita juu ya vita jamaa kazini moto umewaka nyumbani moto umewaka,,

Navoongea jamaa ni mlevi kupindukia
 
Ilikuaje? ?

Vovote vile Lakini itabaki kua damu yake tu. Na mwisho wa siku itamhukumu

Cc Smart911

Ni story ndefu na ya kuhudhunisha, ila kwa kifupi baada mke kuambiwa ukweli kuwa mmewe kazaa nje,, ugomvi ukazuka baina yake na mme, visa ndani ya nyumba vikao vya usuluhishi havikufua dafu mwisho yule mke akasepa akaenda kwao, basi jamaa akavuta ndani yule kimada, yule mke aliyeondoka akaenda kazini kwa mme wake akamwaga mboga,

usiniulize jamaa anafanya kazi gani

Mke anayetambulika naye akarudi jamaa akamtimua tena kimada

Ni story ndefu niishie hapa,
 
Habari wakuu,

Kwa kifupi naishi mkoa tofauti na mke wangu kwa sababu za kikazi, sasa katika pitapita zangu kapatikana mtoto. Wife bado hajajua chochote kwa sababu hakai sana hapa ila najua kwa baadaye itakuja kufahamika kwa sababu kuna watu wanajua.

Sasa nataka kupata ushauri au uzoefu wa wadau kama nisubiri aje kujua mwenyewe au nijitutumue nikae naye chini nimueleze ukweli mwenyewe?

Note: Mke wangu hatujawahi kuwa na mgogoro wowote tunaishi vizuri kwa kuaminiana na upendo mkubwa.

Asante
MNAISHI KWA KUAMINIANA?
 
mwambie mkishaanza kuota mapengo, sasa hivi bado mapema. mkishafikia levo ambayo unaona huyu mwanamke hata aje kujua nini kuhusu mimi hawezi kunikimbia, ndo umwambie.
 
Ivi wakati ule una zini hukujisikia vibaya wakati umesema hamkua na migogoro kama unavyosema,au uliamua tuu kutaka kuonja,pole ila result yake sio nzuri sana muombe sana mwenyezi mungu ampe mkeo subra na uwezo wa kuhimili kwani sio rahisi kujua hilo hasa mtu akiwa ana
kuamini anakuheshimu.
 
Duhhhhh! Balaa hilo. .

Cc Smart911
Ni story ndefu na ya kuhudhunisha, ila kwa kifupi baada mke kuambiwa ukweli kuwa mmewe kazaa nje,, ugomvi ukazuka baina yake na mme, visa ndani ya nyumba vikao vya usuluhishi havikufua dafu mwisho yule mke akasepa akaenda kwao, basi jamaa akavuta ndani yule kimada, yule mke aliyeondoka akaenda kazini kwa mme wake akamwaga mboga,

usiniulize jamaa anafanya kazi gani

Mke anayetambulika naye akarudi jamaa akamtimua tena kimada

Ni story ndefu niishie hapa,
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom