Msaada: Nimuambie mke wangu kama nina mtoto nje ya ndoa?

Piga kimya, supply material kwa mtoto, hama mtaa unaoishi kama umepanga,mtafutie mtaji huyo mwanamke wa nje
 
Kosa halihalalishi kosa. Na yeye akiamua, kusema kosa lake, hakika utakufa kwa presha.
 
Imebidi nicheke tu

Sent using Gun Trigger
Misimamo muhimu mm mke wangu ananijua vzr sitaki masihara mimi.....mimi nimemuoa yy yupo chini yangu nikikosea mda mwingine uwa sikubali kama nimekosea namuonesha umwamba wangu tuu ukoroni tuu ila inategemea na kosa gani kama kosa kubwa sna najishusha namwambia samahani mke wangu nilitelez mara moja tuu aelewi anaendelea leta ngebe namtia vibao tuu ila nachompendea nikimwambia samahani ananielewa maisha yananda ndoma tuna miaka 13 kwny ndoa mwanaume unatakiwa uwe mkoronu mda mwingine wanawake co watu wakuwachekea chekea........

121.
 
Habari wakuu,

Kwa kifupi naishi mkoa tofauti na mke wangu kwa sababu za kikazi, sasa katika pitapita zangu kapatikana mtoto. Wife bado hajajua chochote kwa sababu hakai sana hapa ila najua kwa baadaye itakuja kufahamika kwa sababu kuna watu wanajua.

Sasa nataka kupata ushauri au uzoefu wa wadau kama nisubiri aje kujua mwenyewe au nijitutumue nikae naye chini nimueleze ukweli mwenyewe?

Note: Mke wangu hatujawahi kuwa na mgogoro wowote tunaishi vizuri kwa kuaminiana na upendo mkubwa.

Asante
Mshenzi mkubwa wee. Hivi unakuwaje na roho mbaya kiasi hicho kwa mtu uliyewahi kumpenda? Unachofanya ni conspiracy to murder.Utamletea maradhi mkeo.
Unatakiwa ushitakiwe kwa kuhatarisha maisha yake. Unapitapita mkavu mkavu? Huko unakopita pita unajua na hao wamepitiwa na nani na wanapita wapi? Kama umechoka maisha si ujirushe mwenyewe, yanini uhatarishe na maisha ya mwenzio? Hopefully, hamna watoto na mkeo ningemjua ningemwambia, akapime afya.

Acha ubinafsi, mueleze umalaya unaoufanya ili achukuwe tahadhari dhidi yako.
 
Habari wakuu,

Kwa kifupi naishi mkoa tofauti na mke wangu kwa sababu za kikazi, sasa katika pitapita zangu kapatikana mtoto. Wife bado hajajua chochote kwa sababu hakai sana hapa ila najua kwa baadaye itakuja kufahamika kwa sababu kuna watu wanajua.

Sasa nataka kupata ushauri au uzoefu wa wadau kama nisubiri aje kujua mwenyewe au nijitutumue nikae naye chini nimueleze ukweli mwenyewe?

Note: Mke wangu hatujawahi kuwa na mgogoro wowote tunaishi vizuri kwa kuaminiana na upendo mkubwa.

Asante
Kabla sijakushauri naomba kufahamu
Je una mtoto na hiyo mkeo?

Kama ndiyo hao watoto wa wife na huyu wa kichehe wanafanana?

Je wewe ni muislamu?


Kama muislamu fanya toba kwanza kabla ya yote
Kisha ensure huko mbali na yule kicheche ( backup).

Kisha sasa subiria yeye aje ajue kwa sababu itamuuma sana yeyè kama yeye na atawaka ila hatojua ukweli especially kama hufanani na huyo mtoto. Amgalau kuna self defensive kwa sababu atahisi ni maneno ya watu tu. So usimwambie

Chonde chonde usimweleze hicho kitu
Japo jambazi anapojisalimisha kwa polisi amejiweka pahala salama asiuliwe ila bado atapandishwa kizimbani kujibu mashtaka!
 
The world is not fair. ... Jiandae kulea mtoto ambaye sio wako ..mkeo lazima alipize hilo... Tena wanawake jinsi wanavyo penda kulipiza ..daahh imekula kwako mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unajua ugumu wa kuishi kwa wasiwasi?! Hapo anawaza lazima mkewe atajua tuu, sasa kwa nini asimwambie mgogoro uwepo baada ya siku kadhaa maisha yawe kawaida?!
Hakuna kitu kinaitwa maisha ya kawaida tena Kama atamwambia kazaa nje ya ndoa. Hapo ni kupiga kimyaa tu na kukataa moja kwa moja.
 
Miongoni mwa mambo yanayohitaji busara basi ni pamoja na hili, kiujumla napenda nikuusie kwamba usimwambie.. Maana utakapomwambia tu ndipo utakapopoteza udhibiti kwake kwa visingizio kibao. Wanawake wengi huwa na tabia ya kutaka kulipiza visasi kwa yale yasiyofaa kwao kutendewa na waume zao. Kama mtoto bado ni mdogo mwache akae na mama yake hadi hapo atakapokua kwani wanawake wengi huwa hawapendi kulea watoto wa kambo. Pia kuwa na mahusiano mazuri na huyo uliyezaa nae usije ukamkorofisha kiasi kwamba akamleta mtoto kwa mke wako.
Ni afadhali aje kujua mtoto akishakuwa mkubwa haitomuumiza sana kwa vile pia na yeye mkeo atakuwa kishasogeza miaka walau atakuwa na busara kama mzazi kuliko kujua mtoto akiwa bado mdogo.

ᵃʳᵉᵉᵐ
 
huu uzi umenipa fursa ya kutafakari ndoa yangu kwa namna nyingine. Mungu atusaidie sisi wanaume. Hatupendi haya yatokee lkn dah!! Dunia ngumu sana hii.
 
Ni dhahiri wewe si mkweli/ mwaminifu kwa mkeo. Kukaa bila ya kumwambia, ni kuthibitisha hayo. Ukimwambia, inategemea, ni ili kukiri na kujutia ulilofanya au ni kumtaarifu tu?
Kuna unalohofia juu ya hili jambo?
Ingekuwa ni mimi, ningechukulia kuwa maji yameshamwagika, shurti niyaoge, ningemweleza, kama atanisamehe au la, ni matokeo.
Hapo ni utaishi wako mwenyewe wa lipi zuri la kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom