Msaada: Nimuambie mke wangu kama nina mtoto nje ya ndoa?

Ni story ndefu na ya kuhudhunisha, ila kwa kifupi baada mke kuambiwa ukweli kuwa mmewe kazaa nje,, ugomvi ukazuka baina yake na mme, visa ndani ya nyumba vikao vya usuluhishi havikufua dafu mwisho yule mke akasepa akaenda kwao, basi jamaa akavuta ndani yule kimada, yule mke aliyeondoka akaenda kazini kwa mme wake akamwaga mboga,

usiniulize jamaa anafanya kazi gani

Mke anayetambulika naye akarudi jamaa akamtimua tena kimada

Ni story ndefu niishie hapa,
Kwahiyo kichwa kimeyumba kinaelekea kusiko julikana?
 
Hata kama hutamwambia hakikisha unamlea huyo mtoto.
Tena usikute kafanana na wewe.
Wanaume tunaacha kutunza watoto wetu huko tulikopita kwa kujifanya tunazipenda familia zetu kumbe tunalea watoto wa wenzetu tulioletewa kwenye ndoa zetu.
 
Habari wakuu,

Kwa kifupi naishi mkoa tofauti na mke wangu kwa sababu za kikazi, sasa katika pitapita zangu kapatikana mtoto. Wife bado hajajua chochote kwa sababu hakai sana hapa ila najua kwa baadaye itakuja kufahamika kwa sababu kuna watu wanajua.

Sasa nataka kupata ushauri au uzoefu wa wadau kama nisubiri aje kujua mwenyewe au nijitutumue nikae naye chini nimueleze ukweli mwenyewe?

Note: Mke wangu hatujawahi kuwa na mgogoro wowote tunaishi vizuri kwa kuaminiana na upendo mkubwa.

Asante

CHAGUA CHAUMA,
CHAGUA HASHIMU RUNGWE SPUNDA.
 
Back
Top Bottom