Msaada: Nimetoa pesa kwenye ATM haikutoka ila salio la awali limepungua

Ni tatizo la kawaida na huwa linawatokea wengi. Pesa yako itarudishwa usihofu kabisa. Ukipata wasaa nenda benk waeleze siku na muda na pesa uliyokuwa unatoa utarudishiwa pesa yako. Mara nyingi huwa wanarudisha wenyewe hata wewe usipokwenda.
 
Mimi niliwahi kutoa laki mbili kwenye ATM na wakati mashine ikihesabu umeme ukakatika. Kadi ilitoka lakini pesa haikotoka na nilijagundua kiasi kile cha pesa kilipunguzwa ktk account yangu na hadi leo sikurudishiwa
 
Mambo kama hayo hutoke TZ tu.
Technological failure inaweza kitokea popote. Hata ndege za mashirika makubwa huanguka due to technical failure. Tuache mentality ya kujidharau sana, hii tabia sio nzuri na imeanza kukua sana nchini ktk miaka ya hivi karibuni.
 
Wakuu nilienda NMB bank kutoa kiasi cha fedha mara ya kwanza ATM machine Ilikuwa inahesabu Lakin pesa haikutoka zaidi ya risiti na kadi pekee

kwenye risiti kunaonyesha Huduma haijakamilika Lakin kiasi kilichopo mwanzo kimepungua

Mara ya Pili haikuhesabu Lakin Pia pesa haikutoka na pesa imepungua tena risiti imeandikwa vilevile Huduma haijakamilika

Je naweza kurejeshewa kiasi kilichoonekana kimetoka Lakin sijafanikiwa kukipokea??au hadi niende kwenye tawi la bank husika
nenda kajaze fomu ya maombi ya kurudishiwa pesa iliyokatwa watakurudishia
 
hapo inategemea kama ww ni mteja wa bank ya NMB Au ni mteja wa bank nyingine lakini ulitumia ATM ya bank ya NMB kama ww ni mteja wa NMB it's easy to refund ela yako baada ya kupitia miamala ya cku hyo ktk ATM husika kama ela aikutoka lazima itakuwa imebaki ktk roller so ukienda ku clame watakurudishia fedha yako nadhani huwa ni baada ya cku 2-7

pia kama ww ni mteja wa bank nyingine ukatumia ATM ya NMB kwanza inatakiwa urudi kwenye branch ya bank yako andika barua kwa manager wa tawi la bank yako elezea situation ilivyo kuwa pia ktk maelezo yako usisahau kuandika tarehe, muda na cku lilipotokea ilo tatizo pia namba yako ya card ya ATM na account number ya iliyokuwa unataka kutoa hzo fedha then bank yako ndo watakuwa responsible kufatilia madai yako kwa NMB kama sheria na taratibu zinavyowataka swala hili uchukua cku14-45 kupata fedha yako
 
Wakuu nilienda NMB bank kutoa kiasi cha fedha mara ya kwanza ATM machine Ilikuwa inahesabu Lakin pesa haikutoka zaidi ya risiti na kadi pekee

kwenye risiti kunaonyesha Huduma haijakamilika Lakin kiasi kilichopo mwanzo kimepungua

Mara ya Pili haikuhesabu Lakin Pia pesa haikutoka na pesa imepungua tena risiti imeandikwa vilevile Huduma haijakamilika

Je naweza kurejeshewa kiasi kilichoonekana kimetoka Lakin sijafanikiwa kukipokea??au hadi niende kwenye tawi la bank husika
Kama benki yako ni hio hio nenda kwenye branch watakurudishia baada ya siku 3-7 lakini kama umetoa ATM ya benki ingine si chini ya siku 30.
 
niliwapa kazi watu nikawambia endelea naenda kuleta pesa sasa hivi,, kufika ATM ikanionyesha salio ni 0, nikahisi wajanja washanikombea tuhela twangu. nikapiga namba zimeandikwa pembeni ya mashine wakaniambia ni mtandao baadae nilipoangalia nikazikuta. Nilowapa kazi nilikuta wamejaa sumu kidogo waninyonye macho.
 
Nimejaribu kuangalia naona bado haijarudishwa Labda nisubiri muda kama niliokwenda jana
 
niliwapa kazi watu nikawambia endelea naenda kuleta pesa sasa hivi,, kufika ATM ikanionyesha salio ni 0, nikahisi wajanja washanikombea tuhela twangu. nikapiga namba zimeandikwa pembeni ya mashine wakaniambia ni mtandao baadae nilipoangalia nikazikuta. Nilowapa kazi nilikuta wamejaa sumu kidogo waninyonye macho.
Haya mambo yanatia unyonge Sana
Subiri masaa 24 angalia tena utakuta mambo sawa.
 
Back
Top Bottom