Msaada: Nimesajili line ya simu kwa kufuata kanuni zote, ila natumiwa ujumbe na Kampuni ya Tala kuwa wananidai

900 itapendeza

Senior Member
Nov 17, 2017
110
225
Nianze kwa salamu ziwafikie wanajamvi wooote, nimatumaini yangu muwazima wa afya njema!

Nirudi kwenye maada, takriban siku 20 zimepita toka nisajil laini yangu ya simu katika mawakala wa moja kati ya makampuni ya simu hapa nchini. Usajil huo ulifuata kanuni na taratibu zote kama ilivyo ada. Tatizo lililopo nikwamba baada ya wiki moja kupita nilianza kutumiwa jumbe kutoka kampuni ya tala wakidai marejesho ya mkopo wao.

Kiukwel hapo awali nilipuuzia lakini kadri jumbe hizo zilivyo zidi nilichukua hatua ya kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja kupitia kampuni ya mawasiliano ya simu husika, lakini sikuweza kupata ufafanuzi wa kueleweka kuhusu tatizo hili ,chaajabu leo nimetumiwa ujumbe na hao watu wa tala wakidai nirejeshe mkopo wangu wa tala kabla ya dec 17,

Kituambacho sikifahamu na wala sijui mkopo huo unapatikana vipi, pia kama kuna mtu anaufahamu juu ya kampuni hii naomba anipe uelewa juu ya menyu zake iliniweze kutatua tatizo tajwa,

ahsanteni
 

guzman_

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,064
2,000
mkuu kalipe tu deni lao..inavoonekana kuna mtu alichukua mkopo akatupa lain so wewe ukasajili mana kama lain haitumiki muda mrefu wanafunga
 

Mushi92

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
3,909
2,000
Wapigie simu....wakuelekeze walipo nenda na kitambulisho chako....wape ufafanuzi. Maana picha haiwezi kufanana

Huyo mtu alikopa na akaitupa hiyo lain... Baada ya muda ukasajili ukaipata.
 

900 itapendeza

Senior Member
Nov 17, 2017
110
225
Kama ingekuwa nikutupwa kwa lain hii hapo awali wasingekuwa wanaanbatanusha jina langu pindi wanitumiapo msg zao
 

mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
25,561
2,000
Sasa unachoogopa ni nini? Waambie wakukopeshe tena. Ukipata utawalipa zote kwa pamoja.
 

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
19,250
2,000
Naona Tala inapigiwa promotion kwa namna nyingine kama ng'ombe alishawahi kuzaa mbuzi hapa tutajua tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom