Msaada, nimepoteza uwoga, huzuni & hali ya kujihurumia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada, nimepoteza uwoga, huzuni & hali ya kujihurumia

Discussion in 'JF Doctor' started by Donn, Jun 13, 2012.

 1. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kwanza mm si mtumiaji wa kilevi aina yeyote. Ila nahisi nimeathirika kisaikolojia.
  -Nimekuwa si muoga wa hata yale yanayostahili kuogopwa.
  -nimepoteza mpaka hofu ya mungu.
  -sina huzuni hata pale inapotakiwa kuwa na huzuni.

  nimekuwa nikikabiliana nahali hizi kwa kuigiza uzuni na woga katika sehemu ambazo mwanadamu anastahili kuogopa au kuhuzunika.

  tafadhali msaada wa mawazo doctor
   
 2. M

  Msakwa Chimagai Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naenda kaombewe mkuu. Yesu ni jibu!
   
 3. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  yaani hapo ndo kila siku kaka... Maana mm ni mkristo. Ila nimesoma na kupita katika mengi yanayonifanya kupunguza imani.
   
 4. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Nahisi ni kweli tatizo la kisaikolojia mkuu, nenda ukawaone wataalamu wa saikolojia watakusaidia vizuri zaidi
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mmh, labda umejitambua sana.

  Hata Newton alivyouliza kwa nini apple halijaenda juu labda walimwambia ana pepo.
   
 6. double R

  double R JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 1,352
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Nimewahi soma sehemu kuhusu namna ya kukabiliana na baadhi ya behavioral extremity. To solve them mainly psychologiacally.
  Nadhani inaweza ikakusaidia kabla hujaenda kumuona daktari.
  Gestalt therapy.
  1. Live in present, not dream about the past or future or about one who is absent and what you don't have.
  2. Stop imagining, thinking too much and instead experience the real through your senses.
  3. Express your feeling rather than judge and manipulate others to get them to do what you want them to do.
  4. Learn to experience unpleasant feelings unflinchingly as much as pleasant feeling.
  5. Determine your own mor
  – don't blame others.

  6. Accept yourself as you are, not as you think you should be or others wish you to be.
  Kwa habari ya ukristo, imani ni hatua.Inawezekana kuanza upya. Katika kuanza upya kumbuka, maombi ya kikristo hutambua mapenzi ya Mungu kwetu. Uombapo ujue atafanya kwa wakati wake, namna yake na sababu zake ila yote ni mema kwa ajili yako. Usisahau pia kuwa hata sasa He is in control.
  Pole na naamini utapona, kwa sababu umeonesha nia.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Aisee, hofu na huzuni makes u human! Unapoteza ubinadamu! Unahitaji msaada wa kiroho baba!
   
 8. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sometimes people feel that way after a trauma. Kwa kua akili yako inashindwa ku-deal na hali ngumu fulani ilo kutokea, inajifunga kabisa na unakua detached.

  Unaishi maisha kama sio yako vile, bila ku-develop emotional bound na maisha yako. uoga, interest, sadness etc. Jaribu kurudi nyuma kidogo uone ni kuanzia mwezi/mwaka gani, na what key event happened to youe life then.

  Inaweza kua ni kitu cha kawaida tu ila impact yake ikawa kubwa kwako ki-psychologia. Kama unaweza onana na therapist, au hata ongea na rafiki wa karibu. Kama unaamini, sali.

  Jaribu pia meditation mbali mbali, all the best.
   
 9. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  ahsante... Itabidi nifuate ushauri wako
   
 10. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  ahsante ndugu kwa ushauri. Nimejaribu kukumbuka na kutafakari. Nadhani chanzo ni mambo ya Dini. Nimesoma makala na vitabu vinavyoitazama imani ya kidini na juu ya maisha yetu. Mfano wa kitabu ni ''The secret''by Rhodham Byre. Kwa ataye weza kupata edition yoyote ataona, japokuwa ni hadimu sana.

  Ila nitaenda kumuona mtaalamu wa psychology kwa ushauri zaidi.
   
 11. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,492
  Likes Received: 5,967
  Trophy Points: 280
  pengine uko frustrated, ambayo ni hali ya kukosa kile ulichotarajia. sasa watu wanareactions mbalimbali wakikosa kitu walichotarajia, wengine wanakuwa agressive na wakatili, wengine wanafanya rationalization(sizitaki mbichi hizi) na nyingine ni apathy ambapo mtu anakuwa amekata tamaa na kusema liwalo na liwe yaani anaacha destiny yake kwa wengine na akuwa na huzuni na kukosa feelings (emotions) nahisi upo katika kundi la apathy sasa cha kufanya tafuta hicho ulichokosa au kinachosababisha hali hiyo alafu kitu wanaita compasation mfano msichana amekutenda tafuta msichana mwingine au fanya kitu kingine mbacho unahisi kitaendana value na ulichokosa. au kama tatizo lilianzia utotoni pengine ulikuwa victim wa child abuse so umejenga kitu kinaitwa learning heplessness (tusizame sana huko). kama uko dar pale ubungo kuna kakitabu kanaitwa why me kanazungumzia nafasi ya dini katika matatizo yakisaokolojia. good lucky
   
Loading...