Msaada nimepoteza ladha ya chakula na harufu

Mwili unachemka mara nyingi usiku
*Nakohoa ila sio Sana
*Sina maumivu yeyote
Tatizo Ni joto kupanda na kukosa harufu na taste viungo viko sawa ila mwiri haujachangamka
Ndugu yangu wewe huwa husomi habari za Corona? Hebu pambana na tiba asili na wahi hospitali upate tiba Yao ya Covid. Utapima na X-ray.
 
Baada ya kupata dawa nashukuru naendelea kupata nafuu ila kwa Sasa nikiwa naongea na cm au mtu kwa mda mrefu nabanwa na pumzi Sasa naomba msaada wa namna ya kufanya mazoezi ya pumzi
Uko serious na Afya yako kweli? Ngoja pia nikupe Moja ya bicarbonate of soda itakusaidia haraka. Nitairusha hapa
 
Hii kitu ni hatari wakuu na mm nina dalili kama hizo yapat siku ya pili sasa sinusi harufu mwili unachoka viungo kuuma na kichwa
Hii hali ilishanitokea tena yapata miezi mitano iliyopita sasa imenirudia tena
 
Mwili unachemka mara nyingi usiku
*Nakohoa ila sio Sana
*Sina maumivu yeyote
Tatizo Ni joto kupanda na kukosa harufu na taste viungo viko sawa ila mwiri haujachangamka
UVICO 19
 
Ndugu zangu takriban nina siku mbili Sasa nimekosa kuhisi harufu Wala laza ya chakula ingawa leo kidogo laza imekuja kwa mbali snaa ila harufu bado sijaweza kuhis nitumie dawa gan?
Una Sinusitis inayopelekea kupoteza harufu na ladha ya chakula
Use Intranasal streroid spray-FLUTICASONE OR MOMETASONE
Paracetamol +/- Ibuprofen kwa fever
Nenda hospital check
SARS-COV2 PCR
ESR
ASOT
 
Mkuu hii vitamin c si ndo umetaja kama machungwa na malimao au kuna nyingine
kuna vitamin c suppliment (vidonge) vinauzwa, vimeshameng'enywa toka kwenye matunda huko. ukila chunga hadi mwili ukambeng'enye na kutenganisha ni kesho.
 
Ndugu nawashukuru wote mliochangia mawazo hakika ilikua wiki ngumu kiigodo kwangu ila nashukuru naendelea vyema kabisa kwasasa changamoto zote za harufu ,na zinginezo zimeacha Asanten Sana
 
Poleni sana wote miliokutana na changamoto mbambali Mungu ni mwema siku zote.
 
Ndugu nawashukuru wote mliochangia mawazo hakika ilikua wiki ngumu kiigodo kwangu ila nashukuru naendelea vyema kabisa kwasasa changamoto zote za harufu ,na zinginezo zimeacha Asanten Sana
mkuu ww kifua kilikuwa hakiumi?
 
Pole sana ndugu endelea kupambana hata mimi nilipata hilo sekeseke kikubwa usiwe na hofu piga zoezi+nyungu+dawa siku 7 tu utakuwa road unadunda
Now namshukuru Mungu niko poa bado harufu tu, kwakweli nyungu, malimao, tangawizi, kitunguu saumu ndiyo dawa mujarabu.
 
Mkuu nimesoma thread nzima sijaacha comment hata moja, mimi ni muhanga wa kukosa harufu na ladha week ya tatu sasa.

Mwanzoni nilipata mafua makali sana na kifua naposema mafua makali ieleweke hivyo ni makali naweza sema mafua kama hayo nilipata mwaka juzi mwezi Nov. Mafua haya (niliyopata week tatu zilizopita) na kifua viliambatana na homa, viungo kuuma na kichwa pia.

Nilipima maralia, UTI, typhoid na majibu yalikuwa negative nikapewa dawa ya kifua na mafua. Pumzi haikua inabana ila mafua yalifanya nyakati za usiku napolala nipate shida kupumua kimsingi nilikuwa napumua kwa shida kiasi ila imani kwamba inaweza kua Covid haikumea akilini mwangu.

Nilirudi tena hospitali kwa habari ya kukosa harufu na kutopata ladha, Dr akaniambia itaisha taratibu akawa ameniandikia dawa zinaitwa Azithromycn, cetrizin long, emina sol nasal spray na dawa nyingine nimesahau jina. Hizi dawa zote nilitumia week mbili mfululizo ila shida ya kukosa ladha na harufu iko pale pale. Kwa sasa imebaki hiyo nasal spray nayo inaendea mwisho.

Kwa namna ambayo pua hazinusi wala sipati ladha hata kama napita mahali kuna mzoga sinusi wakuu... Ila nimemshangaa mleta thread anasema hakupata kunusa kwa siku mbili mimi sinusi week kadhaa. Ushauri wenu unahitajika wakuu.
 
Mkuu usiache mafusho, malimao, tangawizi na kitunguu saumu zinasaidia sana hata kama huna covid hali itakaa sawa tu.
 
Asante nieleweshe mafusho ni nini? Toka mwanzo wa uzi nakutana na neno mafusho ni nini hiki mkuu. Hapo kwenye malimao tangawizi kitunguu saumu nachanganya na blendi nakunywa kama juice ama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom