Msaada: Nimepotelewa pesa benki ya CRDB ktk mazingira ya utata

mooy

Senior Member
Aug 19, 2014
171
67
Habarini,

Leo nilienda CRDB ya TFA Arusha kuchukua pesa, sasa baada ya kutoa risiti nikagundua kuwa kuna pesa haipo. Nikaamua kuingia ndani nkaomba statement. Nilichokuta, nusura nizimie.

Inaonekana ile pesa imetolewa tareh 8 kwa njia ya simbanking kiasi tofauti tofauti Mara 5 na pesa hiyo iliingia kwenye simu yangu, kitu ambacho sijafanya kabisa, na nilipojaribu kuhoji sijapewa majibu ya kuridhisha.

Naombeni ushauri nifanyaje.
 
Hamna pesa inayoweza kupotea endapo iliyotumika kutoa hela sio simu yako. Ukikwama kabisa nitafte nitakusaidia free na pesa itarudi. Ila hakikisha aliyetoa sio wewe au kama ulimwachia mtu cm asiye mwaminifu. Lazma ijulikane iyo pesa final destination ni IPI!!
 
simu sijamuachia mtu yeyote,ILA cha kushangaza wao wanasema iliingia kwenye no yangu japo Mimi sikutoa pesa yoyote kwa simu yangu,msaada Wako please
 
Nmefikiria labda niende voda na hiyo statement waniambie Ni namba ipi ilitumika kutoa pesa hiyo,Ni 472000 ILA imetolewa tofauti tofauti kwa tarehe 8
 
Habarini,

Leo nlienda CRDB ya TFA Arusha kuchukua pesa, sasa baada ya kutoa risiti nikagundua kuwa kuna pesa haipo. Nikaamua kuingia ndani nkaomba statement. Nilichokuta, nusura nizimie.

Inaonekana ile pesa imetolewa tareh 8 kwa njia ya simbanking kiasi tofauti tofauti Mara 5 na pesa hiyo iliingia kwenye simu yangu, kitu ambacho sijafanya kabisa, na nilipojaribu kuhoji sijapewa majibu ya kuridhisha.

Naombeni ushauri nifanyaje.

Kamripoti demu wako polisi keshakupiga
 
Pole sana... Inaonekana sasa hivi bank sio sehemu salama ya kutunzia fedha!
 
Namba iliyopo on record CRDB ni namba yako? Imienda kwenye simu yajo kivipi?

Unamaanisha M-Pesa? Ingia Mpesa kwenye simu yako vuta statement uone kama iliingia. Kutakuwa kuna mtu katumia SIM card yako wakati ulikuwa umezubaa.

Ninavyoelewa hauwezi kuingia mobile bank acccount ya mtu mwingine unless unatumia simcard yake, ila situmii CRDB.
 
CRDB Nyanza branch mwanza waliniibia laki moja yangu..miezi miwili iliyopita..wapuuzi sn..nilichukia nikachukua pesa nikaweka m-pesa wapuuzi
 
Kuna kipindi watu walikuwa wanalizwa kwenye NMB mobile bila wao kujua. Mchezo ulikuwa unaanzia kwa wafanyakazi wa Airtel (by then Zain). Wanaiblock namba yako temporarily lakini wanampa mtu mwingine kadi mpya yenye namba yako kama vile kuna namba mbili. Wanafanya yao wakati wameiblock yako wakimaliza wanaiachia.
 
Mimi walinilamba 3.5million, baada ya kuwatishia kwamba nitatafuna utumbo wa mtu bila chumvi wala pilipili walirudisha pesa yangu huku wamepiga magoti!
 
Pole sana. Mimi ndiyo maana pesa zangu naweza kwenye account ya Dollar...
 
Back
Top Bottom