Msaada: Nimepata dharura nahitaji Mkopo wa milion mbili, nitarudisha baada ya mwezi mmoja kwa riba ya 20%

shetrish

Member
Nov 15, 2017
63
96
Husika na kichwa cha habari.

Mimi ni dada mfanyabiashara, mpambanaji ila nimekwama kidogo nahitaji mkopo wa haraka, nitakupa dhamana ya bodaboda (Mpya Haina hata mwaka) na dhamana ya kiwanja kipo Kigamboni, nimekwama jamani, anayefahamu mtu au taasisi kindly PM.

Asanteni
 
Hiyo bodaboda unamaanisha nitakuwa nikiiyangalia tu au unaniruhusu niitembelee au nakaa na kadi?

Pia nataka kufahamu kama ukishindwa kurudisha je tunataifisha hizo dhamana?!!!
 
Kiwanja hati ipo?? Je ukishindwa kurudisha kwa wakati boda boda na kiwanja namiliki mimi rasmi au vipi.
 
Kama sijakosea riba ya asilimia mbili ktk milioni mbili ni kama laki mbili hivi hiyo kwangu ni ndogo labda ufanye asilimia tano kwa wewe.
 
Iyo bodaboda unamaanisha nitakuwa nikiiyangalia tu au unaniruhusu niitembelee au nakaa na kadi?

Pia nataka kufahamu kama ukishindwa kurudisha je tunataifisha hizo dhamana?!!!

Nitakupatia kadi yake na dhamana means nikishindwa kulipa utaiuza (ingawa nina uhakika sitashindwa mana ni pesa nahitaji kwa ajili ya kureplace machine mojawapo ya ofisini Kwangu) naweza kukupatia pia cash flow records za biashara yangu ili ujiridhishe.
 
waTz kwenye swala la huruma limewakalia kushoto sana

Kaka ngoja nikueleze Mimi Sina hiyo pesa, Ila pia watanzania wengi wazushi tu, angalia hapo maswali yalivyokuwa mengi pasipo kujitokeza hata mtu mmoja ambaye anaweza kukupa hiyo pesa.



Mtanzania yupo lazi amnyime nduguye atumie pesa hiyohiyo akalie Bata
watz tuwe waungwana
 
Kwa bahati mbaya upo mbali na kuaminiana kwenye mitandao ni ngumu kulingana na hali ilivyo kwa sasa. Ningekupeleka kwa mtu ambaye angekusaidia hilo hitaji lako kwa haraka sana.
 
Husika na kichwa cha habari.

Mimi ni dada mfanyabiashara, mpambanaji, ila nimekwama kidogo nahitaji mkopo wa Haraka takupa dhamana ya bodaboda (Mpya Haina hata mwaka) na dhamana ya kiwanja kipo Kigamboni, nimekwama jamani, anayefahamu mtu au taasisi kindly PM.

Asanteni
Mkuu bora kuuza kuliko dhamana.

Utapigwa kijini sahau upoteze kila kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom