Msaada: nimenunua kitu online ninahitaji kujua hapa TZ unapokelea wapi?

Habar enu, kwa wale wote mulochangia mada hii na kutuelimisha ninawashukuru na ule mzigo wangu nimeshaupokea kwa njia ya posta. Pia napenda kuwashukuru wafanyakazi wa posta kwa kuonyesha umakini na kazi zao.
Tuiombee Tz yetu tuendelee kuwa waamifu ili tuwe na hadhi katika ulimwengu. Ahsanteni
 
na hapo hapo pesa zako unazikuta zisharudi katika account yako na mzigo pia unaupata bureee.

Sasa hapo urudisiwe pesa zako na mzigo uupate bure! Huo si ni wizi ndugu yangu. Kwa nini usiwe mwaminifu?!
 
Ia posta, nimesikia baadhi ya wateja wakilalamika humu JF kuwa wafanyakaz wao sio waaminifu, hawafikishi mzigo. Jaribu kucheki pia shipping companies kama DHL na Fedex. hapa Tz wapo. Everbuying.com, anawatumia hawa. Ni safe na reliable.
 
wee ndio poyoyo kabisa. unaanzaje kununua kabla ya kujua utapataje unachokinunua??

Hata hilo nalo unataka JF ikusaidie kufaham??
Hiyo hela umeokota nini au umekwiba??

Naomba uanzishwe utaratibu wa kulipia maswali ya kijinga kama haya maana vinginevyo tunafuga ubovu.

Unafanya matakataka yako huko ukitegemea JF itakusaidia...nyambafu kabisa.

Muanze kulipia ili mkiona gharama ndio mtaacha kukurupuka tu......maana wabongo tunapenda sana ku- missuse vitu hasa vinapokua vya bure.
 
1.naomba kuchangia maada, tuanze na suali la wizi katika internet kwa kupatikana details za kadi yako siku hizi ni vigumu, unless mtu awe na BILLING ADDRESS YAKO other wise hata akilipia kama ataweka details za billing address tofauti na mwenye card alivyojaza bank basi malipo yanakuwa declined hata by paypal.
2. hakikisha katika ebay ama paypal unajaza shipping address kama mfumo huu hapa
Ali Juma Ali
Livingstone/Nyamwezi street, house or block #44567
Appartment # 123.
Dar es salaam, Tanzania. 00255
katika address line 2 ndio weka p.o.box
P.O.Box 1234, Dar es salaam
Tanzania.
0777444888

huwo ni mfano tu ila hakikisha hizo address ziwe sawa na ulivyojaza bank ulipo apply hiyo card kuwa itumike online, vyenginevyo ukikutana na wauzaji ambao wanapokea malipo ambayo zimeandikwa ONLY VERIFIED AND CONFIRMED PAYPAL ADDRESS ARE ACCEPTED utapata mtihani wa kuonekana kuwa ni scam kumbe ni uzembe wako mwenyewe.

3. Kuhusiana na shipping bei huwa zinatofautiana kwa kila muuzaji especialy wa ebay ya marekani. Ila hata kama muuzaji hasafirishi africa basi unaweza kumuomba kwa kumuinbox, au unacommit to buy then katika shopping cart yako kuna kitu request total hapo ndio atakutumia invoice ya shipping,
Ili uweze kupatana katika shipping usije kupachikwa bei za ajabu hata kama muuzaji ameweka mfano USPS PRIORITY MAIL FLAT RATE BOX INTERNATIONAL PARCEL basi kwanza hakikisha hiyo bei kupitia hapa Postage Price Calculator then unaweza kupatana nae.
Na hapo ukiwa mjanja unaweza kununua kitu na kikichelewa kufika kwa mujibu wa tarehe za ebay estimation delivery basi unaweza kufunguwa case ya item not received na kutokana wauzaji wengi wanaogopa usije ukampa negetive feedback na kumuharibia point zake basi huwa anakurejeshea pesa zako kupitia paypal ndani ya siku 14 unapata pesa zako ama unakwenda bank na kuwapa paypal refund unique transaction id na hapo hapo pesa zako unazikuta zisharudi katika account yako na mzigo pia unaupata bureee.
Usijaribu kufanya hii kama sio mzoefu wa kununua, mimi ni mzoefu huwa nawabamiza sana maana kuna siku nyengine tracking numbers zinakuwa hazipo uptodate katika usps website wala posta.co.tz so hapo kama mjanja unapata mzigo bure.

4. Kuhusu suali la posta katika kupokea mzigo sina uzoefu na posta ya dar ila ZANZIBAR mzigo wowote ule lazima ufunguliwe na watu wa customs kukaguwa ili ulipe ushuru unless iwe computer na vifaa vinavyofanana na computer kama tablets ndio wanakuachia ila lazima ulipie HANDLING CHARGES ambayo ni tsh 1,770 tu kwa mzigo wowote ambao umekuja kwa njia ya express mail ama priority mail, ila mizigo ambayo inakuja kupitia registered mail ambazo kwa mfano USPS FIRST CLASS MAIL INTERNATIONAL, ama njia yeyote ile ambayo inachukuwa kuanzia siku 24-40 kufika tokea siku ilotumwa, basi huo mzigo haufunguliwi wala haupitii kwa watu wa customs wala hulipii hata HANDLING CHARGES.

5. Kwa wale ambao wanatumia DHL ama carrier yeyote ile ambayo mzigo huendi kupokea posta basi huwezi kuepuka kodi maana mara nyingi huwa wanakupigia simu kuwa uwende airport ukalipie ushuru wa mzigo wako, mimi nilipogundua hilo niliamua kuiamini POSTA YA TANZANIA moja kwa moja mizigo yangu naituma ipitie posta maana unaepusha gharama za kwenda airport hata mzigo uwe mkubwa kiasi gani, tra wapo posta utamalizana nao huko.
Ila zingatia kwamba mizigo yote ambayo imezidi zaidi ya dola 100 na ambayo sio ile ambayo hailipiwi ushuru, kwa mfano mashine fulani basi, utalipia INCOME TAX, HANDLING CHARGES, IMPORT CHARGES NA VAT ambayo zote hizo ukizijumlisha basi utalipia 49% ya bei ya mzigo, so hakikisha kama una mzigo wa aina hiyo basi muombe alokuuzia kuwa auandike GIFT ama aandike bei NDOGO zaidi ili kuepuka gharama zote hizo, NAZUNGUMZA HAYA KWA EXPERIENCE.

NADHANI WENGI MUTANUFAIKA NA MAELEZO HAYA KAMA UMESOMA KUANZIA MWANZO MPAKA MWISHO.[/QUOTE

nadhani sasa mnayo majibu kamili kwa nini wauzaji wengi ukiondoa wachina hawatumi vitu africa.
 
Mkuu ukijiunga na ebay utatakiwa kujaza mailing address yako ili ukinunua vitu wanakutumia kwa box yako.
Mie nipo ebay na nanunua kwa mwaka wa tatu sasa na vitu vyote nachukua posta,
kama kuna ishu yoyote huelew ni pm nitakusaidia.

mkuu malipo yanafanyika kwa mastercard au visa na ni process rahisi sana...
mie natumia crdb mastercard na ukijiunga na ebay kuna sehemu unajaza details za namna utalipa....waweza kuwa unalipa moja kwa moja kwa kukatwa kwenye visa/mastercard yako au kwa kupitia account yako ya paypal.
kujiunga na paypal ni bure na wao ndio wanakuwa na na access na card yako ya visa/master....pindi ukinunua kitu ebay then una authorize malipo yafanyike kwa paypal.....wakishakata hela kutoka kwenye akaunti yako unapata email ya kuthibitisha malipo kuwa yamefanyika na yule mtu ulienunua kwake anakutumia mzigo haraka iwezekanavyo kupitia ile mailing address uliyojaza kwenye ebay.
hakuna usumbufu wowote toka posta kukupa mzigo wako hata kidogo....mie natumia ebay ya marekani na mara zote naona wauzaji wanatumia USPS(United States Postal Services) kama njia yao ya kutuma mzigo na kama nilivyosema hapo awali kuwa ni mwaka wa tatu sasa nanunua vitu toka ebay na vyote vimefika kwa wakati kwa posta hii hii tuijuayo....
for reference yangu
 
Back
Top Bottom