Msaada: Nimempa mtaji wa Tsh. milioni 1.5 ila ndani ya wiki 2 tu kabakiza 500,000

Kikubwa hapo mfukuze kabisa kwako na mwambie iliyobaki ndio mtaji na chakula...ukute kanywea pombe huyo
 
Biashara ina hasara usimpe mtu hela kwa manyanyaso

Unadhani kwenye biashara unaingia tu na kupata faida
 
Attention

Napenda kuthibitisha mkuu Ushimen amenitumia muamala mnono tu wala sikujua jamaa ni real kihivyo, ebwanaa Ushimen nimekuelewa sana, Asante mkuu kwa kuing'arisha jioni yangu, blessed up brother πŸ˜‡πŸ€£πŸ€£

Nimekusafisha rasmi. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Habari zenu

Jamani hawa madogo wanaomaliza vyuo ni pasua vichwa bora sisi wenye la 7 zetu. Dogo kamaliza masomo kaomba mtaji wa kulangua dagaa na kuuza ila kaenda takriban trip 3 tu mtaji umeisha.

Nisaidieni nimuongeze pesa au niache apambaniye hiyo hiyo?

Itakua kabetia mtaji huyo
 
Attention

Napenda kuthibitisha mkuu Ushimen amenitumia muamala mnono tu wala sikujua jamaa ni real kihivyo, ebwanaa Ushimen nimekuelewa sana, Asante mkuu kwa kuing'arisha jioni yangu, blessed up brother πŸ˜‡πŸ€£πŸ€£

Nimekusafisha rasmi. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
SAFI SANA KIUTANI TU,ila angalia sehemu zako za kati zikitumbuliwa we leta mrejesho tu hasa ukiwa KE.
Ukiwa ME mi simo ushimen atajua la kufanya na wewe
 
Nathibitisha na mimi kama bwana chongchung nimepokea mkwanja mrefu kutoka kwa Mkuu Ushimen tuishi humo ngoja niingie kwa Pisi yangu tukale ya nchi na sisi mijuakali sikumojamoja tufaidi.
 
Habari zenu

Jamani hawa madogo wanaomaliza vyuo ni pasua vichwa bora sisi wenye la 7 zetu. Dogo kamaliza masomo kaomba mtaji wa kulangua dagaa na kuuza ila kaenda takriban trip 3 tu mtaji umeisha.

Nisaidieni nimuongeze pesa au niache apambaniye hiyo hiyo?
Mkuu,
Kwanza; nakupongeza Kwa kuwa na moyo wa kumsaidia ndugu yako. Ni jambo jema, la kheri na la kuigwa.

Pili; nikukosoe
Changamoto za biashara hazina kuwa mwanachuo wala kumaliza chuo, kwenye biashara changamoto zipo zinakusubiri ktk kila unalofanya
Kumlaumu mtu kwa kupoteza pesa kwasababu tu ana elimu ya darasani si sahihi, ulipaswa umuongoze kufanya utafiti wa kina kwa biashara anayotaka kufanya kwa kutumia mtaji mdogo mf: 100,000 tu

Kama unataka kuuza chochote na huna uzoefu, hata kama una milioni 200 bank...anza na laki 1, jichanganye na watu wa chini wanaofanya biashara husika kaa nao,kula nao saidiana nao mpaka wakuone ni mwenzao, ukishawaelewa/wakishakuelewa utajua na utaona namna wanavyopata na wanavyopoteza, uwezo na udhaifu wao, uzuri na ubaya wa biashara husika, nani wa kushirikiana naye na nani hafai, wakati gani wa kuongeza mtaji kwenye biashara na wakati gani wa kupunguza nk. (Halafu wekeza zaidi* kwenye udhaifu wao)
Kabla ya kuingia /kufanya biashara yoyote wekeza kwanza kujifunza, wekeza MUDA wa kutosha kabla ya kuwekeza Fedha.


Tatu; Angalia passion ya mtu
Si kila mtu anaweza kufanya biashara, wengi wanajifunza na wanaweza sawa lakini kuna mwingine hawezi kufanya biashara haijalishi ana elimu ya kiwango gani.

Nne; Kujiamini na kusimama na kitu kimoja
Kwanza ujiamini kwamba unaweza, pili uamini kwamba unafanya kitu sahihi, hata kama hakikupi matokeo chanya leo basi kesho na usimame na kitu kimoja bila kuyumbayumba au kuyumbishwa.


Mwisho; Uaminifu
Tusiamini sana kwenye pesa kama nyenzo pekee ya kuendesha biashara
Somo la uaminifu linapaswa kumtawala mfanyabiashara/mjasiriamali yeyote anayetaka kufika mbali kiuchumi na kijamii.

Usiku mwema!
 
Back
Top Bottom