Msaada: Nimempa mtaji wa Tsh. milioni 1.5 ila ndani ya wiki 2 tu kabakiza 500,000

Chakwanza kabla hujampa mtu mtaji wa pesa hakikisha hana madeni na kama anayo basi ni vyema kuyamaliza kwanza hayo madeni, la pili usimpe mtu mtaji ilihali ana njaa kwa hiyo ni vyema kwanza kumsaidia kuitoa hiyo njaa yake akiwa sawa ndio umuwezeshe. Hiyo 1.5m mwenzako ndio alikuwa anachomoa ya kuendeshea harakati zake.
 
Duh! Noma asee! Mkuu pole.

Tatizo aliforce kila kitu kiwe kama anavyotaka kwa muda mfupi. Haya ndio matatizo sasa. Mwache na laki iliyobaki mwambie aibunie shughuli nyingine na mwambie kwa sasa huna.

Nahisi atakuwa anaona utaongeza tu ikipungua kwa jinsi unavyosema hapa ndo maana hana wasiwasi, we kataa tu.

Uone iliyobaki anaifanyaje.

Milion ni parefu sana wapo wanaoanza na elfu 20 tu kwenye dagaa na kupanda stage.

Mwache huyo.
 
Mkuu umeandika mawazo mazuri sana, nayeye anapambana kwenye dagaa but naona yeye shida hajapata soko tu. Kama unaweza kunipa neno kwahyo biashara karibu boss

Mkuu biashara ya dagaa sina uzoefu nayo na sijawahi ifanya ila nina ufahamu kidogo, utafiti ni muhimu soko lipo sana kwa watu wa vijijini sababu ndio mboga kuu mara nyingi wanaweza kununua vipimo vikubwa kama stock ya wiki n.k. mjini ni kilo kidogo kidogo.

Na dogo anahitaji kujikomit kidogo, kama ananunua gunia kwa nini asilitembeze mwenyewe au degree inampa kiburi.

Niseme tu ili biashara yoyote ile iende vizuri haitaki "Watu watanionaje" attitude.
 
Sawa sawa mkuu umenena vyema, ubarikiwe sana
 
Habari zenu,

Jamani hawa madogo wanaomaliza vyuo ni pasua vichwa bora sisi wenye la 7 zetu. Dogo kamaliza masomo kaomba mtaji wa kulangua dagaa na kuuza ila kaenda takriban trip 3 tu mtaji umeisha.

Nisaidieni nimuongeze pesa au niache apambaniye hiyo hiyo?
Muache apambane na hio
 
Back
Top Bottom